Kama una mpango wa kuja South, zingatia mambo haya sita kabla ya kuanza safari yako

Kama una mpango wa kuja South, zingatia mambo haya sita kabla ya kuanza safari yako

Ukikaa mbele uwe mzoefu, uwe unajua hesabu na pia uwe na hela nyingine mfukoni ili zisipoenea kama haujui kuuliza kwa kizulu, ki xhosa, ki sotho nk basi ujazie mwenyewe kimya kimya na kumkabidhi dereva zikiwa zimeenea.

Otherwise maji utaita mma na baba utaita papa 🤣🤣🤣
kumbe wa south sio wajanja sasa hiyo ni upuuzi kwanini wasiajili mtu yani vitu vyengine vimekaa kifala sana!
 
Habari zenu wanaJF wenzangu, ama baada ya salam ningependa kuendelea na mada yangu hapo chini.

Nianze kwa kusema kuwa dunia ina mengi, na kamwe hauwezi kuyajua kama haujaambiwa au kuyaona. Ndio maana waswahili wanamsemo wao unaosema "tembea uyaone". Hii haimaanishi kwamba utembee uyaone magorofa, magari au barabara, bali uone mambo mapya ambayo hapo kabla ya kutembea ulikuwa haujawahi kuyaona au kuyasikia popote.

Sasa leo ningependa nije na mada inayowatahadharisha ndugu zangu wabongo, ili kuwafungua macho na akili ya kujua yale ambayo hapo kabla walikuwa hawajayajua kuhusu South Africa, Dzonga, Afrika borwa, Afrika kusini, bondeni, Kaburu na kila jina linalotambulisha taifa hili.

Ni mambo sita tu ambayo ningependa kukutahadharisha nayo, uyazingatie kabla ya safari. Ila kama kuna mengine ya kuongezea basi wenzangu ambao wako humu pia wataongezea mengine katika comment. Na uzi wangu wa leo unajikita katika mambo yaliopo ndani ya mipaka ya South tu. Kuhusu changamoto zingine za njiani kabla ya kufika South nk, hizo sintozizungumzia kwa sasa. Maana thread za changamoto hizo zipo nyingi na mimi nishawahi kuandika moja.

Tuendelee hapo chini na yale unayotakiwa kuzingatia.

1. Hakikisha una document zote muhimu zinazohitajika safarini. Na kama uliambiwa kuwa gharama ya safari ni laki tatu, basi uandae angalau laki nne, ili moja uiweke pembeni itakusadia mbele ya safari. Kumbuka kuna dharura njiani, dola au rand kupanda nk.

2. Wakati unapanga safari, jitahidi kwanza ujue kingereza. Na kama una kichwa kizito cha kujifunza ngeli, basi upambane ujue hata salam, kuomba kitu au kuaga. South ni nchi inayoongea lugha 11. Ambapo lugha 9 ni za wenyeji na 2 za wazungu. Lakini lugha ya taifa na ambayo inapewa kipaumbele zaidi ni English.

Sasa ukijua English, hata kama hauna elimu ya maaana, uwezekano wa kupata kazi ni mkubwa ukilinganisha na wale ambao hawajui English. Ndomaana wazimbabwe wamedhibiti kazi nyingi na haswa zinazomilikiwa na wazungu, maana wao English kwao ni kama maji na mtungi, halafu wanaongea British safi kuliko waafrika wengine. Kutokujua English kumewanyima watu wengi (haswa kutoka bongo) fursa za kazi, hivyo kusababisha wengine kuamua kufanya deal hatari, halali na zisizo halali ili mradi mtu aishi.

3. Kabla ya kuanza safari hakikisha una address au contacts za wenyeji wako zaidi ya mmoja. Nchi hii kuna watu wengi wameuwawa, wameibiwa, wamekamatwa na kurudishwa nyumbani kwa sababu ya kukimbiwa au kuzimiwa simu na wenyeji wao kabla ya kuingia au baada ya kuingia South. Na hii sio kwa wabongo tu, bali ni nchi zote za East Africa watu wana tabia za kuwaingiza maboya ndugu, jamaa na marafiki zao kwamba waje tu watawapokea na kuwafanyia mpango wa kuishi, lakini ndugu, jamaa au marafiki hao wanapoingia tu mwenyeji huzima simu, hubadili namba nk. Hivyo ukiwa na address au namba za sim zaidi ya 3, itakusaidia ku deal na mwingine baada ya mmoja au wawili wa mwanzo kukuzimia simu.

4. Usiwaze kwamba utafanya kazi fulani tu, bali wewe ujiandae kufanya kazi yoyote (ya halali) kujiingizia kipato. Hili swala la watu kuja huku wakiandaa akili, na saikolojia zao za kichwa kwamba anakuja kufanya kazi fulani tu. Ndio limesababisha baadhi ya wabongo kupoteza mwelekeo wa maisha, na kujikuta wanajitupa katika biashara hatari na zisizokuwa halali.

5. Usilete usela mavi usiokuwa na maana. Vijana wengi waliotaka kuleta usela wa Mbagala, Mburahati, Manzese, Temeke, Tandika nk tumewazika wakiwa bado wadogo. Hii ni kwa sababu huku watu hawana muda wa kukimbizana na mwizi wajichoshe. Ukileta usela mavi, watu wanakutafutia target, wanafumua ubongo, kazi imekwisha. yumbani watu wanarudisha nguo au maiti na kesi hamna. Pia usije kwa lengo la kutafuta na kufanya starehe kupitiliza mpaka ukasahau kilichokuleta. Maana kama starehe hata bongo zipo na umeziacha, kama mademu bongo wapo na umewaacha, kama tungi pia bongo lipo umeliacha. So focus kwa kile kilichokufanya utafute nauli uje. Sio kuendekeza kulewa na chupi za Kaburu utapotea mazima na hakuna mtu atakaekurudisha katika chanel yako tena.

6. Ukifika hapa kama wewe ni mpya usikimbilie kukaa kiti cha mbele katika daladala (tax), hata kama imejaa na imebaki siti moja ya mbele, ni bora usubiri nyingine alafu ndio upande. Hii ni kwa sababu huku majimbo mengi daladala zao hakuna kondakta anaezunguka ndani ya daladala kuomba nauli. So ukisema unakimbilia mbele kukaa na dereva, utashangaa watu wanakusanya hela zote huko nyuma, alaf wanakutupia wewe ndio uhesabu na kama kuna mtu ametoa hela kubwa umrudishie chenji, na ikiwa pungufu uhakikishe waliokupa wanazieneza. Dereva yeye hupokea nauli ambayo imeshahesabiwa tayari na iwe imetimia. Ikipungua hata sh hamsini basi ataanza na wewe uliepokea hela kabla ya kuendelea na waliopo ndani ya gari. Pia asilimia kubwa ya madereva wa hapa wana silaha mbali mbali ndani ya gari zao, kama sio bunduki basi fimbo inayofanana na mkia wa taa. So hela yake isipoenea na wewe ndo New comer (mpya) haujui lugha, basi imekula kwako. Hata ujitetee kwa English yako ya kuunga unga hatokuelewa. Naomba niishie hapa.
Usela mavi, duh hatari sana..
 
Mtoa mada umenena vyema kabisa, tena ukiambiwa laki 3 beba 6, na zifiche kwa kugawa makundi, tafuta kipensi cha jinsi shonea mifuko migumu kwa fundi cherehani wako then zigawe hela, pili epuka mazoea kisa tu umemsikia mtu anaongea kiswahili, wengi wao sio watu tena, wanafosi maisha so mswahili mwenzio kukuua ni chapu sana.
Epuka watu haswa waswahili wasijue mfumo wa maisha yako.

Kuhusu tax ama daladala hakunaga konda so jitahidi sana ukae siti za katikati kama bado hujapazoea. Uwe na uwezo mkubwa wa kukariri mazingira, hili ni muhimu sana.

Nimeingia south kupitia beitbridge, (Zimbabwe na south border, Kopfontein/Tlokweng, Botswana na south, Martin drift, Botswana na south, ktk boda hizo nashauri pitia za Botswana na south, Beitbridge ukiingia tu unaanza kukutana na usela mavi wa wasouth pale misina.

Kiufupi south kila mtu ana stress, anatamani maisha mazuri ya shortcut.

Usimuamini askari au polisi mia kwa mia nao no wezi wakubwa sana tu. South ya leo nenda kibiashara utoke sio pa ku hustle tena.

Mwaka mpya kuingia 23 saa 10 jioni nilipigwa visu vitatu mkononi na pajani kimoja kisa simu tu.

Kiufupi sio salama kabisa na napachukia sana, kama huendi kibiashara eti ni ku hustle aisee nashauri hustle hapahapa bongo.
Aisee , Ile nchi imeharibiwa na ANC na Sera zao za uhamiaji holela .
Criminals wakaanza kukimbilia huko.
South ilikuwa nchi nzuri sana , mimi nina Bro wangu alikuwa huko tangia mwaka 2003 , mwaka 2020 akarudi Bongo na hajarudi huko mpaka leo .
Anasema pia nchi ile imeharibika kabisa ,crimes everywhere , Yaani kuna mahayawani hayaoni kuua kwa kitu kidogo tu .
 
Aisee , Ile nchi imeharibiwa na ANC na Sera zao za uhamiaji holela .
Criminals wakaanza kukimbilia huko.
South ilikuwa nchi nzuri sana , mimi nina Bro wangu alikuwa huko tangia mwaka 2003 , mwaka 2020 akarudi Bongo na hajarudi huko mpaka leo .
Anasema pia nchi ile imeharibika kabisa ,crimes everywhere , Yaani kuna mahayawani hayaoni kuua kwa kitu kidogo tu .
Noma sana aisee
 
kumbe wa south sio wajanja sasa hiyo ni upuuzi kwanini wasiajili mtu yani vitu vyengine vimekaa kifala sana!
Swala la kuajiri mtu ili amlipe, hilo ndo hawataki kulisikia. Kunakuwa na wapiga debe kwenye kituo kikuu cha daladala. Hao ndo wanaita watu kariakoo kariakoo, au ubungo ubungo. Abiria mkishaingia na kuanza safari, yule mpiga debe anabaki kujaza daladala lingine.

Sasa pale dereva anakuwa ashajua idadi ya abiria kupitia viti vyake. Hivyo anajua ni kiasi gani cha hela ambacho atapata kupitia nauli yake. Mfano nauli ni sh100 hivyo kila siti mkikaa watano ni 500. Na kama gari zima lina siti 15 atapata 1500.

Hakunaga cha watu kusimama na kubanana kama bongo, hivyo ni lazima ajue udadi yenu tu, na kiasi cha fedha atachopata. Ni vigumu sana mtu akose kulipa maana mnachangishana wenyewe kila siti halaf mnazipeleka kwa jamaa aliekaa siti ya mbele ya dereva. Nae anazihesabu, kama kuna mtu au watu wametoa hela kubwa anawarudishia chenji zao, zinazibaki anamkabidhi dereva ambae nae anazihesabu akiona zimetimia anazichimbia chimbo lake. Na zisipotimia kimbembe kwako mpokeaji na muhesabuji.
 
Sio msimuliaji mzuri ila mleta mada kafafanua Yale Yale yaliyonipa changamoto mfano hela nilichukua kidogo sana
Documents zilinisaidia sana maana Musina nilikamatwa
Border ya Zambia waliambia hujui kingereza na unaenda SA!?
Nikiwa cape town nilipanda tax nikakaa mbele same situation ikatokea na driver akaniuliza "are you new in town!?"huku akicheka akanipa hiyo knowledge aliyotoa mleta mada
Labda kuongezea ni usitembee usiku na kuwa na mahusiano hovyo hovyo
 
Swala la kuajiri mtu ili amlipe, hilo ndo hawataki kulisikia. Kunakuwa na wapiga debe kwenye kituo kikuu cha daladala. Hao ndo wanaita watu kariakoo kariakoo, au ubungo ubungo. Abiria mkishaingia na kuanza safari, yule mpiga debe anabaki kujaza daladala lingine.

Sasa pale dereva anakuwa ashajua idadi ya abiria kupitia viti vyake. Hivyo anajua ni kiasi gani cha hela ambacho atapata kupitia nauli yake. Mfano nauli ni sh100 hivyo kila siti mkikaa watano ni 500. Na kama gari zima lina siti 15 atapata 1500.

Hakunaga cha watu kusimama na kubanana kama bongo, hivyo ni lazima ajue udadi yenu tu, na kiasi cha fedha atachopata. Ni vigumu sana mtu akose kulipa maana mnachangishana wenyewe kila siti halaf mnazipeleka kwa jamaa aliekaa siti ya mbele ya dereva. Nae anazihesabu, kama kuna mtu au watu wametoa hela kubwa anawarudishia chenji zao, zinazibaki anamkabidhi dereva ambae nae anazihesabu akiona zimetimia anazichimbia chimbo lake. Na zisipotimia kimbembe kwako mpokeaji na muhesabuji.
Na dunia iliyoendelea Ulaya na marekani hakuna conductor mkusanya hela ni unalipia kwenye mlango kwa driver kwa kadi au cash japo wengi ni kwa card tena unakuta ni ya mwezi mzima (kama kwenye train au hizo bus za town ) hii ya konda na abiria ni huku kwetu
 
Back
Top Bottom