Kama una mpango wa kuja South, zingatia mambo haya sita kabla ya kuanza safari yako

Jamaa ni mshamba sana. Kuna wabongo hatari wapo hadi kwenye systems za nchi jirani wanakula na wakuu wa huko. Wengine hadi NIDA za huko wanazo hawasumbuliwi.
Tuelekezane tu wazee mtufumbue macho msituite washamba bhana ingawaje hatujui kitu...
RPC wa Hwange hapo Zimbabwe ni Mtanzania na anajivunia utanzania wake na anajulikana kama Mtanzania mdogo wake yupo SA jeshini...
 
Sio kweli ulichoongea mtu yeyote mwepesi kujua lugha atajua tu hata akijua lugha ingine..
Kweli mkuu, kujua lugha nyingine ni kichwa tu na kujituma. Kuna mtu anajua lugha zaidi ya nne. Na zote amejifunzia ugenini. Kuna wabongo wanaongea kiganda, kirundi, lingala, shangani, shona nk.

Nina mwana wa kitaa bongo, tena mzaramo pure lkn anachapa kichewa mpaka Passport ya Malawi alipata.
 
Uko SA kwa miaka mingap? Labda nikutahadharishe ukirud bongo pia Kuna mambo kadhaa yamebadilika
 
We ni mshamba alafu unaona kuishi sauzi ni ujanja sana
Konda msafi amesema kuna kazi formal kuzipata ni ngumu kama udoktar kwenye hospital za serekali, uhasibu achana na hizo huko hotelini
Naona umeamua kutumia ID nyingine kutetea ulichoandika. Tatizo unakurupuka bila kujua unachoandika.

Mimi kule juu niliandika kwamba ukijua English itakusaidia kupata kazi kiurahisi, ila sikuandika aina ya kazi kama ni ya serikali au ya private. Kikubwa nilichomaanisha ni kupata kazi maana huku mtu anakuja kwa lengo la kutafuta kazi haijalishi hiyo kazi ni ya aina gani. Kama ulitumia akili kusoma utakuta nimefafanua vizuri kuwa ukija hautakiwi uweke akilini kuwa ni kazi ya aina gani utakayofanya. Yani yoyote utakayopata ndio riziki yako hiyo.

Sasa mtu anakuja tena kudai ooh hauwezi kupata kazi serikalini sijui wazimbabwe wanafanya kazi za hovyo. Sasa ni wapi nilipoandika kuwa utapata kazi serikalini? Au wapi nilipoandika kuwa wazimbabwe wanafanya kazi serikali? Muwe mnasoma kwanza vizuri na muelewe kabla ya kukimbilia ku comment upuuzi.
 
Id nyingine ipi angalia nyuzi zangu na zake kama zinaendana acha ushamba wewe sio wakwanza kuishi south africa na sio ujanja
 
Uko SA kwa miaka mingap? Labda nikutahadharishe ukirud bongo pia Kuna mambo kadhaa yamebadilika
Mimi nina miaka zaidi ya 20. Nilikuja nikiwa kijana mdogo, ila kwa sasa umri umesogea. Bongo nilikuwa nakuja sana. Tofauti na baadhi ya wabongo wengine ambao toka wafika hapa hawajawahi kurudi bongo.

Mara ya mwisho kuja bongo ilikuwa ni 2019 kabla ya corona. Toka kipindi hicho mpaka leo sijakanyaga bongo, japo nina mpango wa kuja mwisho wa mwaka.
 
Huyo kijana anaonekana hajui chochote kinachoendelea nje ya Tanzania achilia mbali SA. Ni kijana anaeonekana hajatoka. Hawa ni wale vijana wa Tunduma pale mpakani ambao wengi wao hupewa story mbili tatu na watu wanaotoka SA, kisha wao huichukua hiyo story na kuwasimulia wenzao kama hivi bila kujua kwamba katika wasimuliwaji kuna wale ambao wanafahamu kindaki ndaki kile wanachosimulia pengine zaidi yao wao. So mtu kama huyo ni wa kumuelewa na kumpuuza tu.
 
Id nyingine ipi angalia nyuzi zangu na zake kama zinaendana acha ushamba wewe sio wakwanza kuishi south africa na sio ujanja
Vijana wa tunduma mpakani mkisha hadisiwa story mbili tatu na watoka SA tayari na nyinyi mnakuja jukwaani kujifanya mnajua. Nimekuuliza maswali ni wapi niliposema kuwa mtu ukifika South utafanya kazi za maana wanazofanya wasouth afrika umeshindwa kunijibu na kuishi kulalamika tu.
 
Kila kazi ya maana ilimradi umelizika nayo haya maswala color job na physical hayana maaana kabisa, mbona mwanvita alikuwa sa anafanya kazi voda na alikuwa anavuta kibunda kwani hakuna wsa wanaoweza kufanya?
 
Mkuu me nataka kujua hivi uki over stay si ndo inabidi uishi kwa kujificha ili uepuke kamata kamata ya askari wa migration mitaani? Au hii imekaaje kwa uelewa wako
 
Tupe michongo nasisi tuje kaka huku maisha magumu na kuna watu wasiojulikana wanapoteza watu
 
Dah aisee hongera sana bingwa. Ni kama vile umejitoa katika tanuri la moto mkuu.
Sana aisee siku napanda basi kutoka cape kuja Pretoria ku clear mambo ya passport nilisema Asante Mungu maana mikononi mwa patrol ya police nimenusurika mara tatu
Mikononi mwa gangs mara mbili mbaya Moja haikuwa mbaya sana
Usiku mbaya Woodstock kwa walioko Cape town wanapajua
Pretoria yenyewe amanusura nizichange vibaya aliniokoa jamaa mmoja m colored kwa kunipa info late sana nikala bus kwenda Joz kulala park station three days
Park station penyewe ilibidi nipigane na wamalawi vibaya sana wao wakijua mi mmalawi na watz wanajua mi mrundi basi tafrani kwa kweli kurudi tz nilishukuru na yes lilikuwa tanuru la moto
 
Tuelekezane tu wazee mtufumbue macho msituite washamba bhana ingawaje hatujui kitu...
RPC wa Hwange hapo Zimbabwe ni Mtanzania na anajivunia utanzania wake na anajulikana kama Mtanzania mdogo wake yupo SA jeshini...
Hata mwanza border ya Malawi na Mozambique Kuna migration officer nilimkuta ni mtz jamaa ni alikarim sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…