Kama una mpango wa kuja South, zingatia mambo haya sita kabla ya kuanza safari yako

Kama una mpango wa kuja South, zingatia mambo haya sita kabla ya kuanza safari yako

Habari zenu wanaJF wenzangu, ama baada ya salam ningependa kuendelea na mada yangu hapo chini.

Nianze kwa kusema kuwa dunia ina mengi, na kamwe hauwezi kuyajua kama haujaambiwa au kuyaona. Ndio maana waswahili wanamsemo wao unaosema "tembea uyaone". Hii haimaanishi kwamba utembee uyaone magorofa, magari au barabara, bali uone mambo mapya ambayo hapo kabla ya kutembea ulikuwa haujawahi kuyaona au kuyasikia popote.

Sasa leo ningependa nije na mada inayowatahadharisha ndugu zangu wabongo, ili kuwafungua macho na akili ya kujua yale ambayo hapo kabla walikuwa hawajayajua kuhusu South Africa, Dzonga, Afrika borwa, Afrika kusini, bondeni, Kaburu na kila jina linalotambulisha taifa hili.

Ni mambo sita tu ambayo ningependa kukutahadharisha nayo, uyazingatie kabla ya safari. Ila kama kuna mengine ya kuongezea basi wenzangu ambao wako humu pia wataongezea mengine katika comment. Na uzi wangu wa leo unajikita katika mambo yaliopo ndani ya mipaka ya South tu. Kuhusu changamoto zingine za njiani kabla ya kufika South nk, hizo sintozizungumzia kwa sasa. Maana thread za changamoto hizo zipo nyingi na mimi nishawahi kuandika moja.

Tuendelee hapo chini na yale unayotakiwa kuzingatia.

1. Hakikisha una document zote muhimu zinazohitajika safarini. Na kama uliambiwa kuwa gharama ya safari ni laki tatu, basi uandae angalau laki nne, ili moja uiweke pembeni itakusadia mbele ya safari. Kumbuka kuna dharura njiani, dola au rand kupanda nk.

2. Wakati unapanga safari, jitahidi kwanza ujue kingereza. Na kama una kichwa kizito cha kujifunza ngeli, basi upambane ujue hata salam, kuomba kitu au kuaga. South ni nchi inayoongea lugha 11. Ambapo lugha 9 ni za wenyeji na 2 za wazungu. Lakini lugha ya taifa na ambayo inapewa kipaumbele zaidi ni English.

Sasa ukijua English, hata kama hauna elimu ya maaana, uwezekano wa kupata kazi ni mkubwa ukilinganisha na wale ambao hawajui English. Ndomaana wazimbabwe wamedhibiti kazi nyingi na haswa zinazomilikiwa na wazungu, maana wao English kwao ni kama maji na mtungi, halafu wanaongea British safi kuliko waafrika wengine. Kutokujua English kumewanyima watu wengi (haswa kutoka bongo) fursa za kazi, hivyo kusababisha wengine kuamua kufanya deal hatari, halali na zisizo halali ili mradi mtu aishi.

3. Kabla ya kuanza safari hakikisha una address au contacts za wenyeji wako zaidi ya mmoja. Nchi hii kuna watu wengi wameuwawa, wameibiwa, wamekamatwa na kurudishwa nyumbani kwa sababu ya kukimbiwa au kuzimiwa simu na wenyeji wao kabla ya kuingia au baada ya kuingia South. Na hii sio kwa wabongo tu, bali ni nchi zote za East Africa watu wana tabia za kuwaingiza maboya ndugu, jamaa na marafiki zao kwamba waje tu watawapokea na kuwafanyia mpango wa kuishi, lakini ndugu, jamaa au marafiki hao wanapoingia tu mwenyeji huzima simu, hubadili namba nk. Hivyo ukiwa na address au namba za sim zaidi ya 3, itakusaidia ku deal na mwingine baada ya mmoja au wawili wa mwanzo kukuzimia simu.

4. Usiwaze kwamba utafanya kazi fulani tu, bali wewe ujiandae kufanya kazi yoyote (ya halali) kujiingizia kipato. Hili swala la watu kuja huku wakiandaa akili, na saikolojia zao za kichwa kwamba anakuja kufanya kazi fulani tu. Ndio limesababisha baadhi ya wabongo kupoteza mwelekeo wa maisha, na kujikuta wanajitupa katika biashara hatari na zisizokuwa halali.

5. Usilete usela mavi usiokuwa na maana. Vijana wengi waliotaka kuleta usela wa Mbagala, Mburahati, Manzese, Temeke, Tandika nk tumewazika wakiwa bado wadogo. Hii ni kwa sababu huku watu hawana muda wa kukimbizana na mwizi wajichoshe. Ukileta usela mavi, watu wanakutafutia target, wanafumua ubongo, kazi imekwisha. yumbani watu wanarudisha nguo au maiti na kesi hamna. Pia usije kwa lengo la kutafuta na kufanya starehe kupitiliza mpaka ukasahau kilichokuleta. Maana kama starehe hata bongo zipo na umeziacha, kama mademu bongo wapo na umewaacha, kama tungi pia bongo lipo umeliacha. So focus kwa kile kilichokufanya utafute nauli uje. Sio kuendekeza kulewa na chupi za Kaburu utapotea mazima na hakuna mtu atakaekurudisha katika chanel yako tena.

6. Ukifika hapa kama wewe ni mpya usikimbilie kukaa kiti cha mbele katika daladala (tax), hata kama imejaa na imebaki siti moja ya mbele, ni bora usubiri nyingine alafu ndio upande. Hii ni kwa sababu huku majimbo mengi daladala zao hakuna kondakta anaezunguka ndani ya daladala kuomba nauli. So ukisema unakimbilia mbele kukaa na dereva, utashangaa watu wanakusanya hela zote huko nyuma, alaf wanakutupia wewe ndio uhesabu na kama kuna mtu ametoa hela kubwa umrudishie chenji, na ikiwa pungufu uhakikishe waliokupa wanazieneza. Dereva yeye hupokea nauli ambayo imeshahesabiwa tayari na iwe imetimia. Ikipungua hata sh hamsini basi ataanza na wewe uliepokea hela kabla ya kuendelea na waliopo ndani ya gari. Pia asilimia kubwa ya madereva wa hapa wana silaha mbali mbali ndani ya gari zao, kama sio bunduki basi fimbo inayofanana na mkia wa taa. So hela yake isipoenea na wewe ndo New comer (mpya) haujui lugha, basi imekula kwako. Hata ujitetee kwa English yako ya kuunga unga hatokuelewa. Naomba niishie hapa.
Hili la kukaa siti ya mbele kwenye daladala, limeniacha mdomo wazi. 😀😀😃😁
 
Kila mtu anakusanya pesa mnampatia dreva? Sijaelewa mkuu
Kuna usafiri wa aina tatu, metro train, town bus kama za Udart wanatumia card za wiki hadi mwezi na Tax ambazo Bongo tunaita vipanya au Hiace.

Sasa kipanya kinaeleweka kinabeba watu wangapi level seat, kwahiyo mkiwa njiani dreva anatanga mtowe nauli unaanza mstari wa nyuma, unakuja unaofuata hadi wa mwisho wewe uliyekaa siti ya mbele na dereva.

Lakini kwakuwa ni nchi ya kibabe hilo zoezi wala siyo gumu kila anayepanda anapanda na nauli kamili, mara chache sana mtu kuhitaji change.

Kwa mtu anayejielewa úsafiri wa metro bus ndio mzuri na salama kabisa unacheza na kadi tu, nadhani changamoto kubwa ni route za yale mabasi yanapita zaidi location za wazungu.
 
Sana aisee siku napanda basi kutoka cape kuja Pretoria ku clear mambo ya passport nilisema Asante Mungu maana mikononi mwa patrol ya police nimenusurika mara tatu
Mikononi mwa gangs mara mbili mbaya Moja haikuwa mbaya sana
Usiku mbaya Woodstock kwa walioko Cape town wanapajua
Pretoria yenyewe amanusura nizichange vibaya aliniokoa jamaa mmoja m colored kwa kunipa info late sana nikala bus kwenda Joz kulala park station three days
Park station penyewe ilibidi nipigane na wamalawi vibaya sana wao wakijua mi mmalawi na watz wanajua mi mrundi basi tafrani kwa kweli kurudi tz nilishukuru na yes lilikuwa tanuru la moto
Hope ulitoa sadaka on arrival
 
Kuna usafiri wa aina tatu, metro train, town bus kama za Udart wanatumia card za wiki hadi mwezi na Tax ambazo Bongo tunaita vipanya au Hiace.

Sasa kipanya kinaeleweka kinabeba watu wangapi level seat, kwahiyo mkiwa njiani dreva anatanga mtowe nauli unaanza mstari wa nyuma, unakuja unaofuata hadi wa mwisho wewe uliyekaa siti ya mbele na dereva.

Lakini kwakuwa ni nchi ya kibabe hilo zoezi wala siyo gumu kila anayepanda anapanda na nauli kamili, mara chache sana mtu kuhitaji change.

Kwa mtu anayejielewa úsafiri wa metro bus ndio mzuri na salama kabisa unacheza na kadi tu, nadhani changamoto kubwa ni route za yale mabasi yanapita zaidi location za wazungu.
Asante mkuu.
 
Yaani eti nikabidhiwe nauli kisa nimekaa karibu na davoo nimpe zisipungue hata kumi?
Navyoijua kichwa angu Kila siku kungetokea fujo
Njombe kuna mzee anauza Asali barabarani ukifika hapo hukuti mtu, unatowa pesa unachukuwa asali unaondoka, kama ni chenji unachenji hapohapo wala hakuna wa kukusimamia mbona haibiwi?

Kila sehemu kuna utaratibu wake wa maisha.
 
Vitoto vya miaka ya 2000 ni shida hamuambiliki, endelea kukaza fuvu Msangi yupo kuwasifirisha kwenye box, unakwenda mzima unarudi cargo Swissport.
Humu tunatumia IDs fake mdogo wangu kwahiyo usichukulie vitu serious utakufa mbwa wewe! Acha tuchangamshe genge siku ipite. Naona id yangu imekuchanganya mwenyewe!!
 
Kweli mkuu, kujua lugha nyingine ni kichwa tu na kujituma. Kuna mtu anajua lugha zaidi ya nne. Na zote amejifunzia ugenini. Kuna wabongo wanaongea kiganda, kirundi, lingala, shangani, shona nk.

Nina mwana wa kitaa bongo, tena mzaramo pure lkn anachapa kichewa mpaka Passport ya Malawi alipata.
Hivi mkuu kuna kitu kuhusu passport huwa sijapata majibu kabisa... mtu mwenye passport ya nchi nyingine anawezaje kuitumia kama alishawahi kuwa na passport ya TZ? finger prints si zitaleta shida wakati wa kuvuka?
 
Humu tunatumia IDs fake mdogo wangu kwahiyo usichukulie vitu serious utakufa mbwa wewe! Acha tuchangamshe genge siku ipite. Naona id yangu imekuchanganya mwenyewe!!
Unajichanganya nakuonya, usidanganywe habari za namba, hayo ni mambo ya jela kwa Warden.

Kama una malengo ya kwenda kujaribi bahati yako la kwanza ni hili la namba achana nalo kabisa utapigwa risasi za kichwa bado mdogo na hakuna case.

Pili umri wako bado mdogo jifunze kwanza ujuzi, watu wengi wanaotaabika nje na hata Tanzania ni watu wasiokuwa na ujuzi, nenda veta kasome ndio uwaze kutoka.

Usipoweza kujifunza honestly hivi kupitia watu wenye experince kubwa ya maisha basi utajifunza kwa njia ngumu sana.

Sipendi kosa nililofanya mimi nione mtoto mdogo anataka kulifanya nisikuonye au kukushauri, majuto ni mjukuu kama huna macho ya kusoma ninachokiandika basi wala hamna shida, Dar mpaka Johannesburg ni kilommeters 5000 tu kwa bus go ahed, nauli laki 4 tu.
 
Kwa akili zako umeshusha waraka wa Hamani mrefu hivi unamuamini mtu aliye nyuma ya keyboard! Narudia tena kwenye maisha ukiyachukulia mambo serious hivi utakufa mdogo wangu. Huo ushauri wa makosa uliyoyafanya wewe SA kawape wadogo zako wanaotaka kwenda!. Yaani kabisa mishipa ya shingo imekutoka kisa 26! Watu mna hatari! We kama ulikuwa kindwara huko SA kimpango wako
 
Back
Top Bottom