Nimecheka sana baada ya kuona uzi huu.Hauko kwenye ndoa halafu unasema walioko kwenye ndoa hawana furaha!!That is assumption.
Niko kwenye Ndoa,mimi na familia yangu tuna furaha.Nimeridhika na mke wangu,natafuta pesa kwa ajili ya familia yangu,mke wangu nampanulia biashara mbalimbali huku na mimi nikizidi kupanua wigo wa pesa.Tukiamua kutanua na kuinjoi maisha tunainjoi kama familia na sio kibinafsi.Mtangulize Mungu kwenye Ndoa yako,penda kuonyesha upendo kwa vitendo na sio kutaka wewe pekee upokee huo upendo.Mnaotaka kuingia kwenye ndoa,wekeza nguvu na akili kufanya chaguo sahihi ili usije kujilaumu baadaye.Ambao hamna mpango wa kuingia kwenye ndoa,huo Ni mtazamo wenu kwasababu binadamu hatufanani na kila mtu anaishi maisha yake.Nainjoi maisha ya Ndoa...kabla sijaoa nilikuwa hatua moja ya maendeleo lakini baada ya kuoa nimepiga hatua mara kumi zaidi katika nyanya ya personal income na furaha binafsi.MAISHA HAYAFANANI!KILA MMOJA AISHI MAISHA YAKE AISEEE TUSILAZIMISHANE KUCHUKIA NDOA WAKATI WENGINE NDOA ZIMETUFANYA TUPIGE HATUA.