Kama una mtaji fanya biashara ya Mbuzi, utakuja kunishukuru

Kama una mtaji fanya biashara ya Mbuzi, utakuja kunishukuru

Hapana mkuu, hii inautofauti sana, kuna competition sana ya kununua mbuzi ukizingatia kiwanda ni kikubwa sana wanauwezo wa kuchinja mbuzi wengi sana, lakini pia kumbuka kuna soko la mbuzi pale Pugu na bar pia.
Pugu kubwa mkuu
 
Hapo kweny kuchinjwa wkt mm cko nitajuaje wakti cpo waiz na wez wale tanchoice haiwezekan eti kilo Mia tano wat if Ni kilo 550 kilo hmzin wazile ..kaka ulipata hasar sana
Ukitaka kula lazima ukubali kuliwa(in JK's voice).

Unajua maana ya hasara mkuu?
 
Ahsante sana kwa kua muazi mkuu japo umesema baada ya wewe kupata kazi nyingine. Ila mtririko wa wa biashara ni mzuri, ila hiki kipanda ndo kimeharibu hiyo biashara bepari an exoploit hapa kwa nini asiwe muazi?

"......Unapofikisha mzigo kiwandani unaandikisha idadi ya mbuzi, na label uliyowawekea. Kisha unawaachia bank account au namba ya simu kama utapenda malipo yafanyike kwa njia ya simubank. Baada ya siku moja au mbili maximum unatumiwa kiasi cha uzito uliopatikana baada ya kuchinja mzigo wako na kisha account yako inasoma....."

Bepari anapata faida ×3 ya muangaikaji polini hapo ngozi ya mbuzi ni sh 7000 kwa open market, utumbo wa mbuzi unakausha na kutegeneza chakula cha [emoji241] kilo gharama ni 5000, kama mzani ni wake mpimaji niyeye mnunuzi niyeye duh hiyo sio fair play. Ata akipunguza 0.5kg kwa kila mbuzi ni faida kubwa sana.... wanyonge tutabaki hivo hivo paka pale tutakapo pigania fair trade na matajiri. Hiyo biashara ni nzuri kwa kujikimu ila kutajirika ujenge apartment au mall sio.
Ndo mana inabidi tupambane kufika juu.
 
Tujuze ulichokigundua kwa Eliya Food Ltd mkuu, maana kuna watu soon tunataka kuanza kupeleka mbuzi huko. Kama ni mapichapicha tuache.
Kitu kikubwa nilichokiona kwenye hiki kiwanda(nafkiri hata hiyo tanchoice ni hivyo), yani unapeleka mbuzi/kondoo wako alaf wao wanawachinja, wanawachuna nakutoa vitu vyote vya ndani, kwaiyo nyama ndo inapimwa kwenye mizani yao alaf kilo zinazopatikana ndo unalipwa sasa. kwa mbuzi kilo ni elf8. sasa kitu kibaya zaidi nlichokiobserve ni hicho kitendo cha wao kupima nyama pekee na huku material yote ya ndani hayajumuishwi na wala haupewi undoke nayo. sasa kwaiyo wao ile ngozi pamoja na material yote ya ndani ni mali yao(nafkiri unaweza kuona wanavyopata super profit kupitia wewe mletaji). kwaiyo ukinunua mbuzi kwa kufanya makadirio ya buchani haiwezekani
 
Tujuze ulichokigundua kwa Eliya Food Ltd mkuu, maana kuna watu soon tunataka kuanza kupeleka mbuzi huko. Kama ni mapichapicha tuache.
Alaf pia ununuzi wa Eliyafood huwa unategemea na order ya siku husika kutoka kwa Wateja wao kwasababu hao Jamaa wanaexport nyama kwenda nje ya nchi. kwamfano unaweza kupeleka mbuzi100 alaf wakachinjwa60 hao40 ukaaendelea kubaki nao mpaka siku inayofuatia. Au unaweza kupeleka mbuzi na kondoo alaf ukakuta order ya Wateja wao skuiyo ni mbuzi tuu kwaiyo inabidi ukae na wale kondoo mpaka order ya kondoo ije, yani unaweza ukakaa na mifugo hata siku3 hawajachinjwa, kwamfano mimi nlikaa siku2 ndo mbuzi wangu wakachinjwa, pia nlishuhudia watu wenye kondoo wamekaa pale zaidi ya siku nne kwaiyo muda wote huo unatakiwa kumuajiri kijana wakuwasimamia wapate malisho katika maeneo nje yakiwanda huku wewe ukihitajika kulala lodge kwa siku zote hizo pale border Namanga. kwenye hicho kiwanda ili kuepuka usumbufu inatakiwa upeleke aina moja tuu ya mifugo yani kama ni kondoo iwe kondoo tuu na kama ni mbuzi iwe mbuzi tuu ili kuepuka usumbufu lasivyo utakaa na wale wamasai mpaka ujue kimasai bila kupenda. kwaiyo hiyo ndio hali halisi ya Eliyafood
 
Kitu kikubwa nilichokiona kwenye hiki kiwanda(nafkiri hata hiyo tanchoice ni hivyo), yani unapeleka mbuzi/kondoo wako alaf wao wanawachinja, wanawachuna nakutoa vitu vyote vya ndani, kwaiyo nyama ndo inapimwa kwenye mizani yao alaf kilo zinazopatikana ndo unalipwa sasa. kwa mbuzi kilo ni elf8. sasa kitu kibaya zaidi nlichokiobserve ni hicho kitendo cha wao kupima nyama pekee na huku material yote ya ndani hayajumuishwi na wala haupewi undoke nayo. sasa kwaiyo wao ile ngozi pamoja na material yote ya ndani ni mali yao(nafkiri unaweza kuona wanavyopata super profit kupitia wewe mletaji). kwaiyo ukinunua mbuzi kwa kufanya makadirio ya buchani haiwezekani
Kumbe ni matapeli, hapo kunufaika labda upeleke mbuzi wengi Sana 1000+
 
Kutokana na comments kadhaa inaonesha kbsa hii biashara isn't profitable anymore kama zamani... Over
 
Kumbe ni matapeli, hapo kunufaika labda upeleke mbuzi wengi Sana 1000+
Ndio hivyo kaka hata ukienda pale utaona wanaoleta mzigo/wanaohimili game ni wale wenye mitaji mikubwa kidogo ila hawa wenye mitaji midogo akipeleka mara1 harudi tena, ila wangeondoa huo ujanja ujanja basi hii ni biashara nzuri sana na pia wenye mitaji midogo na mikubwa wote wataweza kunufaika na hivi viwanda. tofauti na hapo huu tunaweza kuuita unyonyaji wa wahindi kwa wafugani na wafanyabiashara wa Tz
 
Nilikuwa natumia gari ndogo mkuu, sana sana kirikuu
Nawakusanya kwa siku kama mbili au tatu halafu napiga simu Mwanza wanaleta gari

Changamoto unaweza ukanunua nguruwe kwenye nyumba kumi maeneo tofauti gari ikija mnaanza kupita nyumba moja mpaka ya mwisho tunapakia tunaondoka
Pia ukishawalipia wakati unasubiri usafiri
mwenye mji anakwambia gharama za kuwalisha ni zako mpaka utakapokuja kuwachukua.

Kirikuu inakaa wastani wa nguruwe 12 wodogo na 9 wakubwa

Kibali ilikua tunakata Buselesele
kila nguruwe Tsh1000

Kila nguruwe nilikuwa naweza kupata faida ya Tsh 50,000 ila sehemu kubwa ya faida inaliwa na usafiri.
Hivi hao mbuzi au nguruwe hawawezi ruka kutoka kwenye gari wakakimbia eh??
 
huko wanakopatikana hao mbuzi ni Kondoa kijiji/mtaa gani? Au ukifika tu kondoa ukiulizia mnada wa mbuzi utapelekwa? Naomba details zaidi jinsi ya kufika huko wanakonunua mbuzi na gharama zakr za usafiri.

Na unazungumziaje uhakika wa soko huko kiwandani? Mana nisije kuchukua mbuzi wa kutosha hlf nafika kiwandani..naambiwa wanastock ya kutosha hawahitaji tena...au inabidi nifike hapo kiwandani kwnz kuona kama wanao uhitaji?
Je ulifanya hii biashara?
 
Ulifanikiwa kwa hii biashara?
 
Umejibu vizuri Sana mkuu shukrani Sana

Ngoja nijichange angalau nipate mtaji wa mbuzi 100 kwa makadirio yangu naona hapo ndyo faida kidogo naweza iona

Kwa ushauri Zaid nitakuwa nazama pm mkuu ili uwe MENTOR WANGU kwenye hii bizness

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Je ulifanya hii biashara?
Karibu sana mkuu. Ni katika kutoa nasi tunapokea. Binafsi mawazo ya watu yamenisaidia sana kufika sehemu nilipo kwa sasa.
 
Back
Top Bottom