Kama una mtaji fanya biashara ya Mbuzi, utakuja kunishukuru

Kama una mtaji fanya biashara ya Mbuzi, utakuja kunishukuru

[emoji1787][emoji1787][emoji1787] Mziki mziki hasa. Siku zote hesabu za kuandika ni nzuri na zinatia matumaini sna. Ila uhalisia ni tofauti na kilichoandikwa. Labda kipindi anapiga hizo mishe yy mambo yalikuwa rahisi. Sasa hivi bei pasua kichwa afu mbuzi bua. Ukiwa na lak 8 ukapata faida ya 20k unashukuru Mola.
Seriously?
 
Mimi swali langu ni kuwa unalipwa kwa idadi ya kilo za nyama tu?? Vipi kuhusu ngozi? Makongoro, kichwa nk? Maana kwenye ngozi lazima wana subsidiary business. Kama vipi wakishangilia nyama watuite tukachukue hayo masafa mengine tukapige biashara mtaani wasitufanye wajinga, eboo (utadhani nishawapelekea hata mtoto wa mbudhi )
 
Hivyo vyote havikuhusu, yani wanachopima ni nyama pekee baada yakutoa hivyo ulivyotaja pamoja na vitu vya ndani kama maini, utumbo n.k jamaa wahuni sana

Sent from my TECNO-C8 using JamiiForums mobile app
 
Wazo zuri. Ila nadhani ukitaka kufanya hiyo biashara ni lazima uwe na eneo hapa Dar ambalo litakusaidia kuwaweka hao mbuzi ili kuwabust kidogo.
Mfano kuwapa chakula bora wale wenye uzito mdogo japo kwa wiki moja ili wastani.

Kuwatibu wale ambao wanamagonjwa ambayo hukuyafahamu na kuwanunua wakiwa wagonjwa.

Ki biashara Mbuzi ana soko sehemu yoyote ile.
Watu wanapenda kuanzia Supu yake hadi nyama choma yake na hata mboga majumbani.

Ni biashara nzuri ukiipangilia.
 
Kwa mahitaji ya mbuzi kipindi hiki Cha sikukuuu tafadhali naomba tuwasiliane napokea Oda za mbuzi na ng'ombe pia

AiSee nmegundua Kitu kwako baada ya uzi hapo juuu nmekuwa nikifatilia comment zako Na kugundua tayal usha fanya kitu juu ya uzi

Kuna sehem ulionesha tayal upo mnadan ukitafuta mbuzi
Na Tayal ushafaham msumu gan mzur wa kuchukua mbuzi

Na Mpaka sas una toa oda za mbuzi

Hakika umejitahd sana hongera kwa kuthubutu na hatua ulio Fikia naamin wewe n mwalimu mzur kweny hii field [emoji1376][emoji1376][emoji1376][emoji1376]
 
Ahsante mdogo mdogo tu kwa Sasa biashara Ina changamoto sio rahisi kihivyo yapaswa ujikatili sio kidogo brohh..

Km mtumishi wa serikali hutaweza kabisaa yaani kukata mtaji ni dkk sifuri tu nowdays (waliofanya miaka 2 nyuma wameinjoi Sana )
Kwanza mbuzi hakuna sio wengi Kama mwanzoni,mkikutana matajiri wengi ndo shida mbuzi zinapandaga balaa tupu.
Kwa wanaopeleka kwa msomali huko ndo majanga[emoji4][emoji16],wapo wanaofanikiwa Ila kukata Pesa nako kawaida tu,au kurudisha Pesa yako,faida pia ipo lakini kwa msomali wapo wanaopata pia.
Shida ya msomali Yule wa mwanzo na wasasa naona tofauti wa Sasa msanii Sana,wengi wamehama au wameacha maana wamekata Pesa,unless uwe Nawewe mjanja mjanja au mtata Kama wao.
Wengi walio kwa msomali ni wale wa muda mrefu ameanza nao kazi anawapa mpk 100m per month wananuna then wanamuuzia..
Bei za mbuziii kwa Sasa sio za zamani ukija huku usitarajie faida ya elf15 au elf10 per head,iwe tu bahati yako,kwa Sasa faida ya elf2,3 mpk tano is normal yaani..

Ukija huku pia minada uitoee maana waeza enda mnadani ukarudi na mbuzi wawili au watano au Mmoja[emoji4][emoji4][emoji4][emoji16] it depends na soko lako.
Mimi niliingia kwa lengo kuuza kwa msomali lakini wadau baadhi wakanambia niende Pugu so napeleka Pugu ingawa Pugu nako Kuna changamoto Ila at least kuliko kwa Msomali.
Shida ya msomali Bei zake hazieleweki afu Ana divide and rule ,Bei Ina weza kua 7700 kwa wale wanyonge afu wale malijendi 8000 au 8300 (wale anaowapa Pesa zake yaani)

So Kama Kuna anaetaka kuingia achoose wisely,then before sijasahau Kuna mhindi pia anachinja hapa Dom pia.
Ni hayo tu akili kichwani meako
 
Kuna wakenya nawaonaga wananunua mbuzi kwenye masoko hapa Arusha na wananunuaga Bei ghali sana. kiasi wakiwa sokoni wabongo husubiri mpaka wamalize kununua.je Kuna yeyote humu kwenye ufaham na solo la kenya?
 
Back
Top Bottom