reymage
JF-Expert Member
- Aug 5, 2021
- 12,467
- 29,403
Okay nakucheki brooAsante sana Kiongozi.
NIko serious na hii business. Kama hutajari naomba tuwasiliane kwa 0764980843. Nahitaji kujifunza zaid.
Okay nakucheki brooAsante sana Kiongozi.
NIko serious na hii business. Kama hutajari naomba tuwasiliane kwa 0764980843. Nahitaji kujifunza zaid.
Ulifikia wapiNataka fanya utafiti nikijiridhisha nianze mchakato japo kwa udogo wake. Nataka ikibidi niwapigie simu nione kama bado wananunua na terms zao zipoje? Nitakapowasikia na nikajiridhisha na mchakato basi niende kondoa machakani huko nako nikajifunze. Wadau mm ni msakatonge tuu nipo morogoro mjini hapa. Tushirikiane kutafiti hili alilotupa mwezetu. Ikishindikana kupata simu zao itabidi niende physically.
Ambacho nimegundua katika biashara hii,fanya uwezavyo hakikisha gharama za usafiri unazipinguza na pia hakikisha mbuzi utakao nunuzia wawe bei rahisi.Ulifikia wapi
Sawa kaka. NakusubiriOkay nakucheki broo
Shukrani tupo pamoja sikiliza tafuta 2m za kuanzia mbuzi 20 tuu!!!usianze juu!!!ukihitaji chochote kwenye hyo sekta haswaa kwa Dodoma nicheki maana ndo minada yangu hapa August mwisho naenda Insha Allah kucheki situation kama imeanza kurudiReymage, Mungu akubariki sana unatema madini mazito sana ,ninaomba Kwa mtu yoyote ambaye anafahamu jinsi ya kufanya cost minimization katika biashara hii atujuze ,kwani faida kubwa ukicheza vibaya inamalizwa na issues za usafiri.
Usafiri huwezi punguza maana bei ipo fixed ,cha kufanya mbuzi nnua vzr yaani hakikisja unajua bei ya Kiwandani ya hyo siku then nnua vzr,ili ukiweka gvt charges upate pesaAmbacho nimegundua katika biashara hii,fanya uwezavyo hakikisha gharama za usafiri unazipinguza na pia hakikisha mbuzi utakao nunuzia wawe bei rahisi.
Swali la msingi ni je unawezaje kutatua changamoto ya usafiri ikiwa wewe unaanza Biashara Kwa mtaji mdogo wa mbuzi 30 au 50??
Asante sana Kaka ,tuko PamojaShukrani tupo pamoja sikiliza tafuta 2m za kuanzia mbuzi 20 tuu!!!usianze juu!!!ukihitaji chochote kwenye hyo sekta haswaa kwa Dodoma nicheki maana ndo minada yangu hapa August mwisho naenda Insha Allah kucheki situation kama imeanza kurudi
Asante sana Kwa ushauri kaka,0718884570 tuwasiliane ndugu yanguUsafiri huwezi punguza maana bei ipo fixed ,cha kufanya mbuzi nnua vzr yaani hakikisja unajua bei ya Kiwandani ya hyo siku then nnua vzr,ili ukiweka gvt charges upate pesa
Mimi nshannua mbuzi 6 nkapata 150k
Na nshanunua mbuzi 30 nkapata 30
Hvyo yaani
Kikubwa usifate mkumbo ndo kanuni ya hii biashara na unnue kwa wakulima tu,kuna watu wanaitwa magaragaja wao wanannua pale pale na kuuza hao ndo wanapandisha bei na wako wengi kuliko matajiri,ukiwa mgeni ukikutana nao utafurahia watakubamiza,wengi wanakuja mnadani wanakutana na garagaja wanapigwa hawarudi,mimi pia mwanzoni nilikutana nacho balaa!!unakata pesa balaaaa!!kule kuzuri uende na mtu akushike mkono,akikuambie usinnue ,usibishe ndo utatoboa kama wiki hivi ,na akupe dos and donts ,unless unakata pesa brother,nipo huko ,na ntaendelea kuwep wala siondoki mpk nitimize malengo yangu.
Kingine never ever trust mtu yoyote kule
Nakupigia hapa,usiogope kikubwa kupambana tuA
Asante sana Kwa ushauri kaka,0718884570 tuwasiliane ndugu yangu
Asante kiongozi.Bei ya sasa hv sokoni ni 12500 per piece
Pamoja sana kakaJumamosi iliyopita nilifanikiwa kufika Tanchoice. Asante Reymage, Sley na wengine wote kwa kutiana moyo. Kwa swala la upokeaji wa mzigo hadi upimaji sikuona shida yoyote. Nilikabidhi mzigo wangu alfajiri j.mosi. Utambuzi wa mifugo kulingana na alama za kila Supplier ulianza mida ya saa 1 ,Uchinjanji ukaanza mida ya saa 2:30 asubuhi , mbuzi wangu walifikia foleni mida ya saa 6 mchana hadi upimaji. Baada ya kuwapima nikapewa risit yangu nikaondoka. J.pili mida ya saa4 asubuhi nikapokea malipo yangu.
KAzi kubwa kwako Supplier ni kujua mbuzi unayemnunua atayoa kilo zitakazokupa faida?. Hapo ndo penye mtihani unaweza kukadria mbuzi kuwa atatoa 7kg akatoa 5kg.
Mbuzi wanaohitajika ni wenye afaya njema niliona mbuzi wakubwa waliotoa 17kg wengi 12-16 kg , huyu wa 17kg nilimwona mmoja, niliuliza juu ya 7-9kg wakasema wanachukua mbuzi wa uzito wowote ispokuwa asiwe amekonda au kuzeeka. Wana daktari anayechunguza nyama ya kila mbuzi kama atakua ameathirika hawachukui hiyo nyama, watakutumia taarifa na picha ya mbuzi husika. Kama ameathirika sehemu tu ya nyama, wanaondoa kipande kilichoathirika wanapima kile kilichosalia.
Swali ambalo sikulidhishwa majibu yake ni juubya vichwa, matumbo na ngozi kwa nini havipimwi ili kuongezanpato la supplier. Mjibu ni kwamba wao wananunua nyama, wale wanao nunua kwa physical weight ndio hufanyia kazi hivyo vingine. Zaidi sana upimaji ni wa kawaida na mzuri.
Hili nalo nenoHabarini Waungwana!
Leo nimeona nitoe mchongo wa biashara ambayo binafsi nimewahifanya kabla sijapata ajira na natarajia kuendelea kufanya baada ya ajira kuisha.
Uzuri wa biashara hii, pamoja na kuwa na faida nzuri, soko lake ni la uhakika sana na changamoto zake ni chache sana na zinakabilika kwa mtu ambaye ameamua kwa dhati kutafuta.
BIASHARA YENYEWE NI KUNUNUA MBUZI NA KWENDA KUUZA KIWANDANI.
A. Upatikanaji wake
Upatikanaji wa mbuzi. Pamoja na mambo mengine ambayo Tanzania tumejaliwa ni mifugo hasa mbuzi. Kuna upatikanaji wa uhakika wa mbuzi na kondoo katika mikoa ya Dodoma (Urangini), Singida, Tanga na Tabora. Kwa kule KONDOA kuna Warangi wazuri sana madalali ambao ni waaminifu sana tofauti na madalali ambao tumewazoea katika jiji la Dar.
Kwa ushauri wangu, sehemu nzuri zaidi ya kununua mbuzi kwa bei nzuri, wenye ubora (Uzito) na faida nzuri, urahisi wa upatikanaji wake na hata urahisi wa usafirishaji ni KONDOA (Urangini). Huku kuna minada ya mbuzi kila siku na hivyo kwa siku unaweza kununua hadi mbuzi 50 na zaidi kama una mwenyeji mzuri.
B. Soko lake
Binafsi ningependekeza kupeleka kiwandani hasa kiwanda cha TanChoice kilichopo Soga, wilani Kibaha mkoa wa Pwani. Hapa utaweza kuuza idadi yoyote ya mbuzi japo huwa wanapenda walau uwe na mbuzi kuanzia 20 (hii ni idadi wakati mimi napeleka inawezekana kukawa na mabadiliko kwa sasa).
Sehemu nyingine ni Longido-Arusha katika kiwanda cha Eliya Food Ltd japo kwa Arusha kuna wanunuzi wengi hasa Wakenya wanatoa bei nzuri sana.
C. Bei ya mbuzi
Kwa kuwa mbuzi hununuliwa vijijini bei yake siyo kubwa kwani ina range kati ya 30-70 elfu. Mbuzi wa 30 elfu anaweza kukadiriwa kuwa na uzito wa kilo 7 au 6.5. Mbuzi wa 70 elfu anaweza kufikisha hadi 12Kg au 13Kg. Kiwandani hawapendelei sana mbuzi wakubwa sana kwa hiyo ni vema kuwa makini katika selection ya mbuzi wa size ya kati ili upate faida nzuri na soko la uhakika.
D. Bei ya nyama kiwandani
Wakati mimi napeleka mbuzi katika kiwanda cha TanChoice, walikuwa wakinunu kwa Tsh 7000/Kg kwa mbuzi na Tsh6800/Kg. Kwa Arusha inasemekana bei iko juu kidogo ila Arusha niseme ukweli sana information za kutosheleza kwani nilienda trip moja tu.
E. Kadirio la faida
Kama mbuzi amenunuliwa kwa kwa Tsh 50,000/= halafu akatoa Kg 9 za nyama ambazo ni sawa na Tsh 63,000/= faida yake itakuwa karibu 6,000Tsh hadi 7,000Tsh kwa mbuzi mmoja. Hapa unakuwa umetoa Gharama zote kuanzia usafiri kutoka Dar nimetumia kwa wakazi wa Dar hadi Kondoa, kulala guest, usafiri kwenda minadani, kuwasafirisha kutoka minadani hadi Kondoa mjini, ushuru wake na vibali, usafiri kwenda Dar kiwandani, chakula na mengineyo.
F. Changamoto zake
Kusema ukweli kila kazi ina changamoto zake na hasa inapokuja suala la biashara, basi changamoto haziepukiki. Biashara hii kama zilivyo biashara nyingine ina makandokando yake kama ifuatavyo;
-Mbuzi kukosa uzito wa kutosha. Hapa ndo sehemu ya kuwa makini sana. Mbuzi wanaotoka Tabora kwa mfano, uzito wake ni mdogo sana wanapochinjwa tofauti na mbuzi wa Kondoa. Kwa hiyo ukinunua mzigo Tabora kwa bei kubwa kuna uwezekano ukaingia loss na kurudi hapa kunitukana na kunilaumu. Naomba kwa atakayekuwa interested aulize maswali ya kutosha na ikiwezekana afike Kondoa kufanya preliminary investigation and research. I do recommend Kondoa kwa warangi.
- Kuna wakati kunakuwa na wanunuzi wengi wa mbuzi kwa hiyo competition inakuwa kubwa sana na kupelekea wauzaji kupandisha bei na hivyo faida kukuachia kidogo sana
- Usipokuwa makini madalali ambao wameshawahi kufika Dar basi lazima watakulalia katika ununuzi wa mbuzi. Binafsi kwa mara ya kwanza nilijikuta kwa kila mbuzi mmoja napigwa 2000-3000Tsh. Yaani mbuzi anamununua 40,000Tsh halafu ananiambia amemchukulia 43,000Tsh.
- Kuna wakati upatikanaji unakuwa mgumu hata kama wanunuzi siyo wengi. Baadhi ya siku unakuta wanaoleta mbuzi minadani ni wachache sana na hivyo unaweza kutumia siku nyingi kupata mzigo mzuri.
- Uwezekano wa kuibiwa mbuzi. Kumbuka munapowanunua mbuzi kutoka mnadani basi munawahesabu na kila mnunuaji anaweza label ya kwake kwenye mbuzi kwa kutumia mkazi. Mimi ilikuwa nachora herufi K ambayo ni herufi ya kwanza ya jina la wife. I love her and she knows that. Baada ya hapo munawaweka mbuzi pamoja na kumkabidhi kijana anayewaswaga kutoka mnadani(minada ipo maporini sijui kwanini) hadi kuwafikisha mjini. Baada ya hapo mbuzi wote wanawekwa kwenye gari na kupelekwa kiwandani. Wakati mwingine mnaweza kupata gari linaloishia Dodoma na kulazimika kuunganisha na wanunuzi wengine wanaofikishia mzigo wao Dom mjini na kisha kutumia gari moja kupeleka kiwandani. Sasa inaweza kutokea au kijana anayewaswaga kutoka mnadani akapiga pande mbuzi mmoja au vijana wanaowaangalia na kuwapeleka malishoni kama unanunua mzigo mkubwa kwa siku kama tatu au zaidi.
G. Malipo
Unapofikisha mzigo kiwandani unaandikisha idadi ya mbuzi, na label uliyowawekea. Kisha unawaachia bank account au namba ya simu kama utapenda malipo yafanyike kwa njia ya simubank. Baada ya siku moja au mbili maximum unatumiwa kiasi cha uzito uliopatikana baada ya kuchinja mzigo wako na kisha account yako inasoma. Hapa kwenye malipo mara nyingi hakuna usumbufu japo binafsi nilifikiria sana reliability yake yaani wanakwambia umepata KG 500, kwa mfano, inakuwa ni hiyo hiyo au inawekana ilikuwa zaidi?
Hitimisho
Kila biashara ina changamoto kama nilivyosema mwanzoni lakini biashara ambayo soko lake ni la uhakika na mzunguko wake ni wa uhakika basi daima huwa ni biashara nzuri. Kwa yeyote anayependa kujaribu biashara hii, nashauri afanye utafiti wa kutosha na kisha aanze na mzigo kidogo hata wa 1M kwanza aone faida yake, changamoto zake n.k.
ASANTENI KWA MDA WAKO NAKUTAKIENI MAFANIKIO KWA KAZI UFANYAYO.
Shukrani kakaJumamosi iliyopita nilifanikiwa kufika Tanchoice. Asante Reymage, Sley na wengine wote kwa kutiana moyo. Kwa swala la upokeaji wa mzigo hadi upimaji sikuona shida yoyote. Nilikabidhi mzigo wangu alfajiri j.mosi. Utambuzi wa mifugo kulingana na alama za kila Supplier ulianza mida ya saa 1 ,Uchinjanji ukaanza mida ya saa 2:30 asubuhi , mbuzi wangu walifikia foleni mida ya saa 6 mchana hadi upimaji. Baada ya kuwapima nikapewa risit yangu nikaondoka. J.pili mida ya saa4 asubuhi nikapokea malipo yangu.
KAzi kubwa kwako Supplier ni kujua mbuzi unayemnunua atayoa kilo zitakazokupa faida?. Hapo ndo penye mtihani unaweza kukadria mbuzi kuwa atatoa 7kg akatoa 5kg.
Mbuzi wanaohitajika ni wenye afaya njema niliona mbuzi wakubwa waliotoa 17kg wengi 12-16 kg , huyu wa 17kg nilimwona mmoja, niliuliza juu ya 7-9kg wakasema wanachukua mbuzi wa uzito wowote ispokuwa asiwe amekonda au kuzeeka. Wana daktari anayechunguza nyama ya kila mbuzi kama atakua ameathirika hawachukui hiyo nyama, watakutumia taarifa na picha ya mbuzi husika. Kama ameathirika sehemu tu ya nyama, wanaondoa kipande kilichoathirika wanapima kile kilichosalia.
Swali ambalo sikulidhishwa majibu yake ni juubya vichwa, matumbo na ngozi kwa nini havipimwi ili kuongezanpato la supplier. Mjibu ni kwamba wao wananunua nyama, wale wanao nunua kwa physical weight ndio hufanyia kazi hivyo vingine. Zaidi sana upimaji ni wa kawaida na mzuri.
Wapo mkoa gani ofisi zao?Jumamosi iliyopita nilifanikiwa kufika Tanchoice. Asante Reymage, Sley na wengine wote kwa kutiana moyo. Kwa swala la upokeaji wa mzigo hadi upimaji sikuona shida yoyote. Nilikabidhi mzigo wangu alfajiri j.mosi. Utambuzi wa mifugo kulingana na alama za kila Supplier ulianza mida ya saa 1 ,Uchinjanji ukaanza mida ya saa 2:30 asubuhi , mbuzi wangu walifikia foleni mida ya saa 6 mchana hadi upimaji. Baada ya kuwapima nikapewa risit yangu nikaondoka. J.pili mida ya saa4 asubuhi nikapokea malipo yangu.
KAzi kubwa kwako Supplier ni kujua mbuzi unayemnunua atayoa kilo zitakazokupa faida?. Hapo ndo penye mtihani unaweza kukadria mbuzi kuwa atatoa 7kg akatoa 5kg.
Mbuzi wanaohitajika ni wenye afaya njema niliona mbuzi wakubwa waliotoa 17kg wengi 12-16 kg , huyu wa 17kg nilimwona mmoja, niliuliza juu ya 7-9kg wakasema wanachukua mbuzi wa uzito wowote ispokuwa asiwe amekonda au kuzeeka. Wana daktari anayechunguza nyama ya kila mbuzi kama atakua ameathirika hawachukui hiyo nyama, watakutumia taarifa na picha ya mbuzi husika. Kama ameathirika sehemu tu ya nyama, wanaondoa kipande kilichoathirika wanapima kile kilichosalia.
Swali ambalo sikulidhishwa majibu yake ni juubya vichwa, matumbo na ngozi kwa nini havipimwi ili kuongezanpato la supplier. Mjibu ni kwamba wao wananunua nyama, wale wanao nunua kwa physical weight ndio hufanyia kazi hivyo vingine. Zaidi sana upimaji ni wa kawaida na mzuri.