Jumamosi iliyopita nilifanikiwa kufika Tanchoice. Asante Reymage, Sley na wengine wote kwa kutiana moyo. Kwa swala la upokeaji wa mzigo hadi upimaji sikuona shida yoyote. Nilikabidhi mzigo wangu alfajiri j.mosi. Utambuzi wa mifugo kulingana na alama za kila Supplier ulianza mida ya saa 1 ,Uchinjanji ukaanza mida ya saa 2:30 asubuhi , mbuzi wangu walifikia foleni mida ya saa 6 mchana hadi upimaji. Baada ya kuwapima nikapewa risit yangu nikaondoka. J.pili mida ya saa4 asubuhi nikapokea malipo yangu.
KAzi kubwa kwako Supplier ni kujua mbuzi unayemnunua atayoa kilo zitakazokupa faida?. Hapo ndo penye mtihani unaweza kukadria mbuzi kuwa atatoa 7kg akatoa 5kg.
Mbuzi wanaohitajika ni wenye afaya njema niliona mbuzi wakubwa waliotoa 17kg wengi 12-16 kg , huyu wa 17kg nilimwona mmoja, niliuliza juu ya 7-9kg wakasema wanachukua mbuzi wa uzito wowote ispokuwa asiwe amekonda au kuzeeka. Wana daktari anayechunguza nyama ya kila mbuzi kama atakua ameathirika hawachukui hiyo nyama, watakutumia taarifa na picha ya mbuzi husika. Kama ameathirika sehemu tu ya nyama, wanaondoa kipande kilichoathirika wanapima kile kilichosalia.
Swali ambalo sikulidhishwa majibu yake ni juubya vichwa, matumbo na ngozi kwa nini havipimwi ili kuongezanpato la supplier. Mjibu ni kwamba wao wananunua nyama, wale wanao nunua kwa physical weight ndio hufanyia kazi hivyo vingine. Zaidi sana upimaji ni wa kawaida na mzuri.