Kama una mtaji fanya biashara ya Mbuzi, utakuja kunishukuru

Hii mada nzuri sana. Lakini ili angalau upate faida inakubidi angalau uwe una uwezo wa kuuza mbuzi hata 100
Yaaah ni kweli kwa nia ya kupata faida kubwa! Kitu cha kuangalia kwenye biashara yoyote ni kile kiitwacho "BREAK EVEN POINT". Wafanyabiashara mnajua ninachosema yaani angalia POINT au SEHEMU unapopatia FAIDA. Ukipafahamu then idadi siyo hoja kwani utakuwa umeshajua break even point yako na faida yako itakuwaje!
 
Tatizo wanachinja usiku na huwa mbuzi ni wengi sana labda zaidi ya elfu 5 na wanakuwa wamechanganywa kutoka sehemu mbali mbali ni ngumu kuingia kiwandani kusubiria mbuzi wako wachinjwe na in short utaratibu wao uko hivyo, lakini they are reliable.
Hakuna kitu hapo. Watakuwa wanawapiga watu Sana
 
Kwa nn usingefungua uzi wenye hili tangazo lako? Mpk udandie kwenye uzi wa watu?
Huoni inaleta mashaka hata kwa ss wateja kujua km kweli wewe ndo mtoa huduma au umedandia kazi za watu....
 
Kutokununua mzigo mnadani kuna muda inakua na changamoto nakumbuka kuna kipindi nafanya biashara ya kuku nikawa naenda mlango kwa mlango. Niliingia hasara sana kwanza ilichukua mda mrefu kujaza mzigo, pili nilinunua kwa bei kubwa sababu siku ya mnada kuku walikua wengi bei ikashuka maradufu zaidi ya ile nilinunua door to door
 
Mleta mada hongera Sana kwakutufumbua

Na tumaswali tuchache mkuu

Mnappsafirisha mbuzi malipo yapoje mnalipa kwa idadi ya mbuzi au makadirio tu?

Naomba kujua idadi ya vibali ambavyo unatakiwa kuwa navyo kwa ujumla ili usisumbuliwe toka kununua had kufikisha mzgo sokoni

Je katika mwezi unaweza kufanya mizunguko mingapi yaan tripu ngapi kupeleka mbuzi kiwandani?

Asante mkuu tumaini langu nitapata majibu mkuu





Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 

Maswali mazuri ndugu.

Kila mbuzi unamlipia ushuru 1000Tsh kwa kila mbuzi halafu kibali kinakuwa ni kimoja ambacho ili kupunguza gharama mbuzi wote wanakuwa chini ya kibali kimoja kama vile mwenye mzigo ni mtu mmoja, kama mzigo ni mkubwa basi sisi tulikuwa tunakata vibali viwili basi.

Kuhusu mara ngapi unaweza kupeleka mzigo itategemeana na mtaji wako na uchakarikaji wako katika kutafuta mzigo. Upande wa mtaji Nina maana kwamba unaweza kuagiza mzigo kiwandani labda wa 3M halafu kama una balance ukabakia unakusanya mzigo mwingine wakati unasubiria mzigo ufike kiwandani, mbuzi wachinjwe na pesa utumiwe. Kuna wakati inaweza kuchukua hadi siku 3 au 4 kutoka mchakato wa kusafirisha mbuzi kutoka vijijini hadi kiwandani hadi kupata pesa kwa hiyo ndani ya siku hizo unajikuta una andaa mzigo mwingine, unafanya rotation. Wenye mitaji mikubwa walikuwa walifanya hivi.

Sijui kama kuna swali nimesahau kujibu mkuu
 

Nauli ya mbuzi mnalipa kwa idadi ya mbuzi lakini hao madreva kutoka Kondoa kwenda Dodoma mjini kama gari ni la kuungaunga huwa hawahesabu idadi ya kila mbuzi mnamkadiria tu.

Kama wewe ni mwepesi na unajua kuongea vema na watu utapata mzigo kiurahisi sana kuliko wale watoto wa mama
 
Kwa mwezi kiongozi ulikuwa na uwezo wa kufanya mizunguko mingapi, yani ununuzi na uuzaji wa mzigo

Aise mimi mtaji wangu haukuwa mkubwa kwa hiyo nilikuwa nasubiria malipo kwanza kwa hiyo kwa week nilikuwa nafanya trip moja au mbili. Lakini niseme ukweli nilikuwa sikosi faida nzuri kabisa kwa sababu nilikuwa napigania maisha siyo ukwasi kama wa MO
 

Ndugu yangu yangu sijui nia yako ya kuuliza maswali haya kwa sababu nimetoa maelezo yote haya kweli uzi, kiwanda kilipo nimetaja kijiji, wilaya hadi mkoa, nimesema mbuzi unaweka alama kwa kukata manyonya kwa kutumia mkasi na mzigo nimeshasema kila siku wanapokea. Upande wa order ukishapeleka mara ya kwanza basi unasajiliwa na alama yako inatunzwa kwa hiyo siku nyingine hata huhitaji kwenda na gari kiwandani wewe unapakia mzigo unaenda kiwandani halafu unasubiria notification ya idadi ya kilo na mtonyo wako.
 
Soga kipo kibaha upande upi mkuu kibaha pana kidgo
 

Kweli mkuu kwa maelezo yako ni dhahiri umewahi fanya biashara hii, lakini sasa hiyo sehemu ya mwisho ya kwenda nyumba kwa nyumba ni ngumu sana, utapata taabu sana kufikisha mzigo na bei itakuwa kubwa sana. Ukibahatika mnadani wanunuzi wakawa wachache na mbuzi wakawa wengi, unapata mbuzi wa kuchagua wewe mwenyewe, bei ndogo na faida inakuwa nzuri.

Halafu kingine kwa sasa iko hivi; kuna wenyeji kule ambao ni Warangi wenzao, wanaojua kila kichaka na kila nyumba, kwa hiyo huwa wananunua mbuzi kutoka kwenye nyumba za watu kisha kuwapeleka minadani kuwauuza, hawa jamaa wanapiga faida nzuri pia kwa sababu unaweza kukuta kwa kila mbuzi anapiga zaidi ya 5000/= akiwa na mbuzi 50 anaondoka zake na 250,000/= kwa siku. Kwa hiyo hawa wenyeji huwezi kushindana nao kwani wao wanaongea lugha moja.
 
Umejibu vizuri Sana mkuu shukrani Sana

Ngoja nijichange angalau nipate mtaji wa mbuzi 100 kwa makadirio yangu naona hapo ndyo faida kidogo naweza iona

Kwa ushauri Zaid nitakuwa nazama pm mkuu ili uwe MENTOR WANGU kwenye hii bizness

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 

Karibu sana mkuu. Ni katika kutoa nasi tunapokea. Binafsi mawazo ya watu yamenisaidia sana kufika sehemu nilipo kwa sasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…