Kama una mtaji hizi ndio Ajira mkononi

Nakataa nakataa
 
We nae Mpesa nayo ni biashara ya kumshauri mtu kufanya? Any way inawezekana wewe unafanya na unapiga mkwanja mrefu ebu twambie wewe unaingiza kias gan kwenye M-PESA ili nasi to be motivated.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Biashara kichaa hii. Real estate sio biashara ya kujibana kwa hela za jasho, ni biashara ya kuwekeza hela ambazo hukutarajia na hukuwa na plan nazo. Mfano mafisadi, wauza madini wakiotea, ukishinda tuzo, au ukiwa na biashara inalipa sana kwa mfumuko lakini unajua kuna siku itaanguka.

Huwezi hangaika na mishahara kisha ukafanya real estate
 
Wewe unaamini degree inaandika mashairi. Kile ni kipaji sio elimu, hakuna vyuo cha kufundisha kipaji bali cha kuinua vipaji. Mtu amegraduate na gamba la Logistics unamwambia aandike mashairi ya kina Kondeboy yale ya nataka kutooo...totoo... unahisi kuna elimu inamuelekeza uko
 
Level MUST tunaanzia small scale kwa target [emoji457][emoji457][emoji457] wakuu mm nmelima vitunguu swaumu kwa SIMU ntawapa mrejesho though natumiwa FOTO ya kila stage navuna wa 9.. INSHALLAH
Umelima kwa simu? Mara mwezi wa 9 unaenda kuvuna hukuti shamba lenyewe[emoji848]
 
Isije kuwa photos zinapigwa kwenye shamba la mtu mwingine[emoji23][emoji23][emoji23]
Nilishawahi kunusurika kufa kwa presha Ruaha Mbuyuni baada ya kukuta shamba ninalojua tumelima likiwa vichaka tupu huku kwenye simu kuna ekari 5 za vitunguu.
 
BIG IQ
 
Huwa nashauri mtu asifanye chochote ambacho ni rahisi kuigwa eneo alilopo. Lakini endapo atafanya aweke iwe tofauti sana na wengine. Mihogo ile ile ila kachumbari yake sasa iwe tofauti sana.
 
Aliyekwambia stationery ni business nyepesi amekudanganya! Mm nafanya biashara ya stationery toka nimeanza haijavuka hata miaka miwili, kwa Sasa napata faida ya 300,000/= kwa mwezi, ambayo naigawa sehemu3.
1. Kijana wa kazi
2. Mm mwenyewe
3. Stationery yenyewe.

Naomba usiwakatishe tamaa vijana waliomua kuzama ktk biashara hii yenye faida kubwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…