Kama una ndoto ya kwenda Ulaya, Marekani, Canada n.k, pitia uzi huu

Binafsi nataka nizame nje( US/UK) kama Professional baada ya miaka miwili.

Kwa sasa natafuta uzoefu kwanza.
 
Mkuu malizia basi na USA maana hawa ndio giant wa dunia pale nafikiri ndio nchi pekee yenye idadi ya wagwni wengi kushinda yoyote embu tumalzie na marekani basi bila ya USA huu uzi hautanoga
 
Nchi bado ina mapori mengi, mngetafutana vijana kadhaa, then mkaiombe serikali iwakatie sehemu ya mapori ili muweze kufanya shughuli za kilimio mngeweza sana kusaidia kuinua uchumi wa taifa na kusaidia kupunguza wimbi la vijana kukimbia nchini
 
Utaendaje nje kuuza supermarket na mtu una elimu yako? Afadhali ukomae hapa, akina MO na Bakhresa huwa wanatoa sana ajira
 
Sasahivi Ulaya kumejaa Wahamiaji wa nchi zenye VITA mpaka wenyeji wameanza kuwachukia Wahamiaji. Nchi nyingi za Ulaya kwa sasa zinaangalia namna gani ya kudhibiti wimbi la wahamiaji na kuweka masharti magumu zaidi. Kuna baadhi ya nchi zimeanza kujadili kwenye mabunge yao namna ya kudhibiti hadi Wanafunzi wanaoingia Ulaya kwa ajili ya masomo.

Kutokana na wingi wa wahamiaji, kuna baadhi ya nchi za Ulaya Magharibi (kunakodhaniwa ndiko kwenye Ustaarabu zaidi) vijana wahamiaji wameanza tabia za kukaba watu kama ilivyo Panya Road kwa Bongo. Wenyeji wanachukizwa sana na hii tabia ya watu wa wakuja na kuwaharibia Ustaarabu wao.

Vyama vinavyounga mkono masuala ya kuleta wahamiaji vimeanzwa kupigwa chini na vinaingia vilivyo na mtizamo hasi dhidi ya wahamiaji. Maisha ya Ulaya kwa sasa yameanza kuwa magumu na upatikanaji wa vibarua umeanza kuwa adimu. Yote kwa yote bado Ulaya huwezi linganisha na Afrika.
 

Ok
 
Kuna conference ya kanisa U.S unapata invitation letter. Conference IPO mwezi wa 8 Missouri, nitatoza gharama kidogo kwa mwenye uhitaji.
Including supporting Documents
Hiyo invitation letter
Filling visa form na ku book appointment.
Karibuni sana.
Mwongozo tafadhaliii
 
Ni mkutano wa kanisa wa Wasabato, unafanyika kila mwaka Marekani. Unajumuisha mataifa kutoka sehemu mbalimbali za dunia kushiriki kongamano hilo.
 
Ni mkutano wa kanisa wa Wasabato, unafanyika kila mwaka Marekani. Unajumuisha mataifa kutoka sehemu mbalimbali za dunia kushiriki kongamano hilo.
Kama hutojalii tupe gharama zote tuone tunafanyeje
 
Marekani ukikosa kazi ni umetaka, labda uwe teja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…