Kama una ndoto ya kwenda Ulaya, Marekani, Canada n.k, pitia uzi huu

Chief nahitaji South Korea gharama kiasi gani kwa tourist visa
 
Tuwatambuwe na wale wadada wenye ndoto zao za kuolewa na ngozi nyeupe😉 kama njia moja wapo wa kupata nafasi ya kwenda majuu.
Ndugu mleta uzi naomba kuwasilisha🙏
Hii wanaiweza wanawake wa kenya tu sana sana.. na wanakuja mpaka huku tz , znz kutafuta wazungu. Wanwake wa kibongo wakipata tu mzungu au bwana wanaanza kutangaza njaa na dhiki..

Hebu fikiria kwa akili za kawaida tu. Unataka kumtoa mrembo out aje umlishe umnyweshe kwa fedha zako lakini bado atakudai kuwa umtumie nauli hana ..? Hakuna mzungu atakaye deal na hizi non sense atahisi kabisa anachunwa.

Madem wa kibongo wakitoka date na mzungu akiambiwa wa split the bill wataweza.??

Wapunguze kuonesha njaa ,na dhiki kwanza .watafanikiwa
 
Ahaaaa embu sema si wote maana michakato ishaanza. Ila wakenya loh!!
 
Hapo sharjah Dubai port kuna Kazi nyingi Sana za meli.
Deiwaka zipo za kutosha, kufanya usafi kwenye meli, nk.
Kazi ambazo ni rahisi sana kupata nje ni za ubaharia, udereva, usafi, mashambani, kulisha mifugo, hizi Kazi wazawa sijui watoto wa kizungu au kiarabu hawafanyi hizi kwao ni cheap.
 
Jiandae kwa maisha ya upweke na kazi tu.

Kaka acha kabisa, Maisha ya Ulaya ni ya upweke wa balaa kwa mtu aliyetoka Africa, huwezi kwenda ka jirani wala sehemu kwamba nikale nipige soga na watu, Pesa sio kila kitu ila ukiwa na furaha ndio kila kitu.

Nilikua nawaza home mpaka nakonda, chakula nacho magumumashi hakina ladha, miezi 3 ya mwanzo nilipata tabu sana aisee.

saivi nakata mitaa kama sina akili nzuri
 
Hapa bongo ni rahisi sana kutajirika kuliko huko lakini ni hadi uwe na macho.

Tanzania unatajirikaje? mbona watu wapo vile vile tu?
tunakimbia nchi sio kama hatuna hela ya kula HAPANA bali hatutaki watoto wetu waishi maisha yetu na kuhangaika ukubwani

Kama unaweza kusomesha mtoto IST bila stress basi baki Bongo. ila kama ada ya Feza boys inakutoa jasho basi wewe huna tofauti na mzamiaji

Elimu atayopata mwanangu ni 100% sawa na elimu anayolipia mtu IST m74 kwa mwaka, sasa bora nini
 
IST na FEZA wanapelekwa kukua na sio kusoma Ili waajiriwe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…