Kama una ndoto ya kwenda Ulaya, Marekani, Canada n.k, pitia uzi huu

Kama una ndoto ya kwenda Ulaya, Marekani, Canada n.k, pitia uzi huu

SEHEMU YA PILI.

Namna kufika Germany na UAE na shughuli za kufanya.

Germany- Kwanza kwa asiyefahamu, Ujerumani ni nchi inayoongozwa na maneno ya Paulo Mtume aliyowaandikia Wathesalonike katika barua ya 2; 3:10. “Asiyefanya kazi na asile”.
Ukiwa Germany ni mwiko kuishi bila kufanyakazi yoyote. Sijui kama sera imeshabadilika lakini wakati naenda kupiga kazi wakati wa kiangazi, ilikuwa mhamiaji akikamatwa anazurula....anakamatwa na kupewa kazi yoyote ili ale chakula kwa kukifanyia kazi. Kuombaomba na kupewa bure katika nchi hii ni dhambi. Napendekeza mtu kwenda katika nchi hii kwani kupata kazi ni rahisi.
Kwa Ulaya au nje ya nchi hakuna kitu cha muhimu Kama kuwa na kazi. Hii ndo sababu nashauri sana kuangalia nchi ambazo itakuwa rahisi kupata kazi.
-Namna ya kufika Germany. Nchi hii ni mojawapo ya nchi zinazounda Umoja wa Ulaya(European Union).
-Kwa hiyo ukiweza kupenya mojawapo ya taifa linalounda umoja huu basi inakuwa rahisi sana kuingia Germany.
-Unaweza kwenda kama mtalii wa nchi mojawapo ya taifa la EU kisha ukazamia Germany kusaka sega la asali.
NB: Ukikamatwa Germany na passport lazima urudishwe nchini mwako mara moja kwa gharama zao. Sera hii ipo pia Switzerland and Netherlands.
-Kwa hiyo cha kufanya, ukifika nenda Ubalozi wa Tanzania nchini Ujerumani, wapatie passport yako halafu utakapoamua kurejea nchini tena itakubidi kuifuata ubalozini.
-Germany pia inatoa nafasi za masomo kwa hiyo unaweza kujaribu bahati yako kuomba udhamini.
-Kiingereza kinaongelewa lakini ukifahamu Kijerumani utakuwa katika nafasi nzuri sana.
(Nakumbuka namna nilivyopata chance ya kuwa naenda kupiga kazi Germany, ni baada ya siku moja kuwa na mazungumzo na Mjerumani mmoja ambaye alikuwa ni visiting lecturer chuoni kwetu. Aliponiuliza natokea wapi nikamjibu Tanzania halafu nikaongezea, moja ya nchi iliyotawaliwa na babu yako...nilifanya hivyo in an amazing casual way kiasi kwamba aliniona mtu cheerful nisiye na resentments. Tulitokea kuwa mabest sana na hata kuwa ananifanyia michongo ya kazi zenye malipo matamu).
Mwisho ukiwa Ujerumani-fanya kosa lolote lakini siyo kuchelewa chelewa. Uchelewaji ni kitu Mjerumani hawezi kuvumilia. “Be obedient to Kantian punctuality”.

UAE [emoji1256] (United Arab Emirates)
Kwa asiyefahamu, unaposema [emoji1256] una maanisha muunganiko wa vinchi saba ambavyo makao makuu yake yapo Abu Dhabi. Kiongozi Mkuu pia yupo Abu Dhabi huku msaidizi wake akiishi Dubai.
Abu Dhabi ndiyo imeshikilia uchumi mkubwa kwa sasa ikifuatiwa na Dubai kisha Sharjah.
Umoja huu, mbali na Abu Dhabi, Dubai na Sharjah, unajumuisha pia Ajman, Umm Al Quwain, Fujairah na Ras Al Khaimah.
-Wale vijana wa Ilala wanaofuata spea za magari Dubai, chimbo lao lipo Sharjah.

Namna ya kufika- Wepesi wa kufika Dubai ni kwamba kama unatokea Tanzania unaweza kwenda bila visa na ukakata visa on arrival. Kwa maana hii Mtanzania yeyote anaweza kutinga Dubai bila shida yoyote.
-Unaweza kwenda kama mtalii kwa kukata visa ya miezi3 au 6 na kishafika kule ukaprocess working na resident permit. Visa hii utahitajika kukata ticket mbili yaani go and return lakini kwa sasa technology itakusaidia kwa kukata ticket moja ya go na return unaweza kupata “DUMMY TICKET”.
-Pamoja na kuwa [emoji1256] una vinchi saba, binafsi napendekeza Dubai kwa sababu zifuatazo;
  • Mchanganyiko wa watu wa mataifa mengi
  • Ni mji ambao ni very westernized
  • Uchumi ni mzuri na kazi bado zipo japo competition ni kubwa sana kutokana na kuzungukwa na labor-zone states yaani Africa, India, Pakistan, Afghanistan, Srilanka, Bangladesh, Lebanon, n.k.
  • Gharama ya maisha ipo chini sana ukilinganisha na nchi nyingi zilizoendelea
  • Thamani ya pesa ni nzuri sana (1AED=630Tsh)
  • Ni karibu sana hivyo panafikika(nauli inafika hadi chini ya laki5 za Kitanzania)
  • Ni rahisi sana kutuma pesa nyumbani kutokea Dubai
  • Kuna sehemu za kuabudi za wahindi ambapo wanatoa breakfast, lunch na dinner bure kabisa hivyo kwa mzamiaji unaweza kuishi kwa kuvizia mlo sehemu hizo.

    -Ukiwa Dubai unaweza kufanya kazi za kuajiliwa kama vile Ulinzi, Usafi, Ujenzi n.k au unaweza kujiajili mwenyewe kwa kufanya shughuli zifuatazo

    -Unaweza kuingia mjini kati yaani Deira City Centre na ukapiga kazi ya kupakia na mizigo kwenye magari.
    -Unaweza kufanya kazi ya kusukuma toroli la mizigo katikati ya mji hasa hasa Deira
    -Unaweza pia kujiajili kuuza nguo, mikoba ya wanawake, Viatu nk, ambapo itakubidi ujue machimbo ya wachina unapoweza kupata mzigo kwa bei nafuu...sehemu kama Baniyan Square shughuli hii inapigwa sana na waafrica.
    -Kuna wa Wabongo wengi pia maeneo kama Etisalat wanapiga shughuli ya kuuza mishikaki, vitumbua nk.
    -Kama wewe ni risk taker unaweza pia kupiga deal la kuuza pombe; kikubwa ni kujua chimbo la kupata mzigo zaidi Sharjah na sehemu ya kuuzia. Hii kazi inalipa sana.

    Mwisho kwa mtu anayewaza kutoka nje ya nchi Dubai ni sehemu ya kufikiria kuanzia kabla ya kuwaza kwenda kuishi katika taifa kubwa kama [emoji631].
    Maisha ya Dubai na Bongo binafsi sikuuona utofauti mkubwa sana.

    Next time nitakuelezeeni namna ya kufika USA na naamini kila mtu anapenda sana. Kwa kila mwaka huwa nasaidia walau watu 2 kufika USA na huu ni mwaka wa 3 nafanya hivyo.

    “Aquila non capit muscas”
Mkuu angalia inbox yako
 
Korea kuna jamaa yangu ameenda juzi tu.hii ni mara yake ya pili,huwa anatumiwa hela ya tiket ya kwenda na kurudi,kule kuna kazi za shamba ,upandaji wa miche ya matunda na uvunaji wa matunda.

Alisema kule ni kazi kazi na kama wewe ni lele mama hutapaweza.Mana wanaenda na mda vibaya mno .Mda wa kulala usiku panawahi sana kukucha na mda wa mchana masaa hayaendi kabisa .

Sehemu ambayo huwa anafikia ni sehemu iliyo tengwa kwa ajiri ya wazee,hivyo kuona msichana au mu mama ni ngumu hadi uende mjini.

Huwa ana sema kule kupata mtu wa kibarua ni kazi kweli kweli,na hata mwenyeji wake huwa anamwambia asije akamkacha akiwa kule,mana vibarua ni adimu mno hasa waafrika mana ndo wachapa kazi tofauti na race zingine.

Malipo yake ni mazuri sana ila mziki wake ni wa moto mana unaweza kaa miezi sita hujaona binti wala mu mama.Ni wewe na kazi kazi na wewe ,ni kujitoa hasa.mana ni upweke wa [emoji817]%


Jamaa ni dereva wa lori ila huwa anaacha kazi huku anafata mkate wa kule .
 
Sina roho ya kitanzania. Nina roho ya kiwest, kusaidiana nazimwaga hapa soon watu wakapambanie kombe wenyewe.
Ntaku quote
nimeongelea kidogo hili suala kwenye uzi wangu huko jukwaa la kazi,.hii ni muhimu kutujuza Watanzania wenzio maana hizi fursa zimekuwa za kufichana utadhani mtu akifika kule atafunga ridhiki zako. Naamini haya maisha kila mmoja Mungu humgawia kwa namna yake ni yeye kujibidiisha kupambania anachohitaji. Watanzania linapokuja suala la kwenda nje hawana habari njema wataleta habari za kutishana ilihali, majority ya wanataka kutoka nje ni Vijana wa Kiume,ambapo kwa mtazamo wangu mwanaume ana kila sababu ya kupambania kesho yake iwe njema haijalishi ndani au nje. Mwanaume kiasili ni mlishi hivyo kutafuta ni lazima. Watanzania hata forex walificha lakini wakati ulipofika kila mtu alijua mambo ya forex na wengine imewatoa. Hata sahivi mawakala wa kazi za nje Tanzania wanafanya dili kimya kimya lakini natabiri siku si nyingi zijazo job recruiters wa kazi za nje watakuwa wengi tu mjini hapa kama Nairobi na watu watachagua waende wapi na kwa kazi gani. Watu watiririke tu hapa namba za mawakala na ofisi zao,kila mtu aende kwa wakati wake.

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
 
nimeongelea kidogo hili suala kwenye uzi wangu huko jukwaa la kazi,.hii ni muhimu kutujuza Watanzania wenzio maana hizi fursa zimekuwa za kufichana utadhani mtu akifika kule atafunga ridhiki zako. Naamini haya maisha kila mmoja Mungu humgawia kwa namna yake ni yeye kujibidiisha kupambania anachohitaji. Watanzania linapokuja suala la kwenda nje hawana habari njema wataleta habari za kutishana ilihali, majority ya wanataka kutoka nje ni Vijana wa Kiume,ambapo kwa mtazamo wangu mwanaume ana kila sababu ya kupambania kesho yake iwe njema haijalishi ndani au nje. Mwanaume kiasili ni mlishi hivyo kutafuta ni lazima. Watanzania hata forex walificha lakini wakati ulipofika kila mtu alijua mambo ya forex na wengine imewatoa. Hata sahivi mawakala wa kazi za nje Tanzania wanafanya dili kimya kimya lakini natabiri siku si nyingi zijazo job recruiters wa kazi za nje watakuwa wengi tu mjini hapa kama Nairobi na watu watachagua waende wapi na kwa kazi gani. Watu watiririke tu hapa namba za mawakala na ofisi zao,kila mtu aende kwa wakati wake.

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app

Fursa za kazi ughaibuni na mtazamo wangu

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
 
Mnasema mnabaguliwa ila bado mnaongozana kwnda kwa wabaguzi km makondoo

Kua maskin au umaskini ni kitu kibaya sana yan ukiwa maskin ujui nn unataka na kwa jinsi gan unataka na ni jinsi gan utapata

Watu weusi kla sku tunasema wazungu wabaguzi ila ss ndo kla sku tunakufa kwenye maboti tukienda ulaya na wengne utoa pesa kibao kupata vibal vya kwenda ulaya na marekani
 
Tuwatambuwe na wale wadada wenye ndoto zao za kuolewa na ngozi nyeupe[emoji6] kama njia moja wapo wa kupata nafasi ya kwenda majuu.
Ndugu mleta uzi naomba kuwasilisha[emoji120]
Niko hapa ngozi nyeupe pee ndani ya Thailand niliye na ndoto za kuwowa PISI KALI toka Africa kama wewe Luckyline, tafadhali unikumbuke katika ufalme wako Murembo [emoji1787]
 
Hii wanaiweza wanawake wa kenya tu sana sana.. na wanakuja mpaka huku tz , znz kutafuta wazungu. Wanwake wa kibongo wakipata tu mzungu au bwana wanaanza kutangaza njaa na dhiki..

Hebu fikiria kwa akili za kawaida tu. Unataka kumtoa mrembo out aje umlishe umnyweshe kwa fedha zako lakini bado atakudai kuwa umtumie nauli hana ..? Hakuna mzungu atakaye deal na hizi non sense atahisi kabisa anachunwa.

Madem wa kibongo wakitoka date na mzungu akiambiwa wa split the bill wataweza.??

Wapunguze kuonesha njaa ,na dhiki kwanza .watafanikiwa
Tabia haiigizwi na siku zote mlamba asali hakomi kulamba.
 
Back
Top Bottom