Kama una panic, huu ni ugonjwa na unatibikaa

Kama una panic, huu ni ugonjwa na unatibikaa

mwanaupepo

Member
Joined
Apr 5, 2013
Posts
98
Reaction score
22
Panic attack(jazba..waswahili mtanisaidia) 550px-Understand-and-Care-for-Your-Sister-As-a-Brother-Step-.jpg

Hii ni ile hali ya kuingiwa na hofu au uwoga ghafla ingawa kiuhalisia hakuna kitu chochote kibaya kinachotokea au kitacho tokea. Hofu hii inampelekea mtu huyu kupata mfazaiko (anxiety)

Hali hii hua inadalili zifuatazo kwa mgojwa;
kutokwa na jasho (sweating),
pumzi kupungua (shortage of breath),
mapigo ya moyo kwenda mbio,
kuhisi maumivu ndani ya kifua (chocking sensation),
kutetemeka kwa hofu (trembling),
Nazingine nyingi kwa walio wagonjwa wanazo.

Wagojwa wa tatizo hili mara nyingi wanakua waoga hata kujichanganya na kikundi cha watu pamoja kuogopa kabisa kufanya vitu vinavyo weza kupelekea hali yake ikajidhihilisha mbele za watu.
Naa kutokana na ( Anxiety and Depression Association of America),wanasema watu milion sita wanapatwa na tatizo hili kwa mwaka.

Kiuhalisia kuna nyingi, ila zote hizo tunaweza tukaziweka katika makundi manne kama ifuatavyo;

  • Psychotherapy (ushauri/kisaikolojia)
  • Medications (dawa)- Xanax, Valium, Klonopin, and Ativan
  • Complementary Treatments-Relaxation Techniques,Exercise,Nutritional Supplements, Dietary Changes
  • Lifestyle Changes(kubadili mfumo wa maisha)

Usitumie dawa(medications) bila maelekezo ya dactari. Pia ifahamike kwamba hii pia inasababishwa na upungufu wa madini ya magnesium pamoja na thiamine(vitamin B1), kwahiyo dietary changes ni kutumia vyakula vyenye madini hayo kwa wingi kama nafaka za bila kukobolewa, mboga za majani,na matunda.

Haishauriwi kutumia aina moja ya tiba, ni vema zaidi ukatumia zaidi ya moja.

WENZETU WANA TATIZO HILI, PIA KUNA WENGINE HAWAFAHAMU KAMA WANA HILI TATIZO, EM TUWASAIDIE WENZETU KWA KUJADILI TATIZO HILI KWA KUONGEZA DALILI ZINGINE,TIBA, PIA HATA CHANZO CHA TATIZO, ILI NAO WAYAFURAHIE MAISHA!
 
Naomba mtu analifahamu hili anipm kwa msaada pls.my god bless you>>....
 
Pia mimi ni mwathirika wa hyo kitu, huwa ninafikia hatua nashindwa kabisa kuongea mbele za watu kwa sababu ya hofu, kiukweli ni hali inayoninyima raha sana km kuna namna ya kunisaidia naomba mnipe mbinu za kuepuka hyo hali, mdau hapo juu mi natumia cmu kaka cjui naweza kuku pm kiaje sorry c unajua haya mambo ya mzungu yanazngua
 
Ah hata mim nina hlo tatitzo yan nikiwa mbele za watu natoa presentation huwa natokwa na jasho huku pumz ikikatika mda mwngne nakatsha hta cwezi endlea msaada wenu wakuu
 
Kwa sehemu kubwa hili hutokea kama ishara ya mwili kuanza kupungukiwa maji mwilini. Kama mtu ataongeza kiasi cha maji anachokunywa kila siku na kuacha vinywaji kama soda, juisi za viwandani na pombe tatizo hili litaisha bila shida yeyote. Kama hujuwi ni kiasi gani cha maji unapaswa kunywa kila siku tafadhali bofya hapa. Au unaweza kuni pm kwa maelezo zaidi.
 
Ah hata mim nina hlo tatitzo yan nikiwa mbele za watu natoa presentation huwa natokwa na jasho huku pumz ikikatika mda mwngne nakatsha hta cwezi endlea msaada wenu wakuu

Ndg ww nami hatupishani mi niko udom hakuna cku czpendi km za presentation hata mtiririko wa mawazo hunitoka kabisa ninapocmama mbele za watu, hofu nyng na trembling ya hali ya juu mm c muumini wa waganga wa kienyeji lkn kwa hl lnaweza kunipeleka kwa hao jamaa,coz naweza kufanikiwa kumaliza chuo ila kupata kazi ndo itakuwa shughuli pevu, cdhan km nitahimili maswali ya kwny interview, c kwamba mi nikilaza niko njema tu drsn issue ni kutojiamini, tafadhali wataalam nisaidieni, kupiga ctor niko vzuri issue inapokuja ni pale utakapotakiwa kwenda mbele ya wenzako kupresent au kuhubiri.
 
Wakuu msaada wenu maana confednc ni kila kitu katika maisha
 
Mbona mr mzizi mkavu huitolei ushauri hii thread? Tunahitaji msaada wako kiongozi!
 
Imekua ni kawaida kusikia mtu akisema ninapanic sana. Je; ni kweli kinachowatokea ni tatizo linalojulikana kama panic attack au ugonjwa wa panic? Dalili za tatizo hili la panic ni kama hizi zifuatazo
Kwanza kabisa;

Dalili hizi hutokea ghafla na hufikia kilele au ukali wake ndani ya dakika 10-15. Kwa watu walio wengi; dalili hizi huisha baada ya dakika 20-30 na ni mara chache sana dalili hizi zitadumu kwa zaidi ya lisaa limoja.

PANIC ATTACK HUHUSISHA MJUMUIKO WA DALILI NA HISIA ZIFUATAZO
• Kushindwa kuhema au kukosa hewa
• Mapigo ya moyo kwenda kasi. Heart palpitations or a racing heart
• Maumivu ya kifua (Chest pain or discomfort)
• Kutetemeka (Trembling or shaking)
• Kutokwa jasho (Sweating)
• Kichefuchefu au tumbo kuvuruga (Nausea or upset stomach)
• Kizunguzungu au hata kuzimia (Feeling dizzy, light-headed, or faint)
• Kufa ganzi (Numbness or tingling sensations)
• Hot or cold flashes
• Hofu ya kufa au kuchanganyikiwa (Fear of dying, losing control, or going crazy)
• Choking feeling
• Feeling unreal or detached from your surroundings

IKIWA TATIZO HILI LA PANIC LINAKUPATA NA KUJIRUDIA MARA KADHAA KWENYE MAISHA YAKO NA KUKUNYIMA RAHA AU KUKUFANYA USHINDWE KUFANYA SHUGHULI ZAKO; HUITWA PANIC DISORDER AU UGONJWA WA PANIC. UGONJWA HUU HUTIBIWA NA WATAALAM WA AFYA NA MAGONJWA YA AKILI NA UNAPONA KABISA
 
Mimi ulinipata baada ya kufiwa na mke wangu,,, tena ulikuja aghafla sana , nilijua huu ndo mwisho nililia sana hasa nikiwaona wanangu,,, tofauti na magonjwa mengine huu unakufanya eti uone kama malaika wa mauti anakusubiri akutoe roho.. sikua naumwa chochote kabisa ulinikuta naangalia TV tena katuni aghafla nikapata woga wa ajabu,, niliwaogopa bata wa katuni.. nikakimbilia msalani sikupata kitu.. nikachukua udhu nikasali nikiamini ni sala yangu ya mwisho... familia ika panic pia... wa mamombi walifanya, wengine wakidhani nimepigwa jini, ugonjwa huu waweza kukuingiza kwenye ushirikina fasta ni hatari sana.. hospital nilikwenda na huko nikapewa dawa za kulala kwa muda mrefu na zingine hata sizifahamu .... baada ya muda mrefu nikapona..... namuomba sana Mola wangu nisije ugua tena ugonjwa huu,, nakuwaombea wengine pia... Ameen
 
Tofauti na tezi dume, kikwete anasumbuliwa na ugonjwa huu wa panic attack.
 
Mimi ulinipata baada ya kufiwa na mke wangu,,, tena ulikuja aghafla sana , nilijua huu ndo mwisho nililia sana hasa nikiwaona wanangu,,, tofauti na magonjwa mengine huu unakufanya eti uone kama malaika wa mauti anakusubiri akutoe roho.. sikua naumwa chochote kabisa ulinikuta naangalia TV tena katuni aghafla nikapata woga wa ajabu,, niliwaogopa bata wa katuni.. nikakimbilia msalani sikupata kitu.. nikachukua udhu nikasali nikiamini ni sala yangu ya mwisho... familia ika panic pia... wa mamombi walifanya, wengine wakidhani nimepigwa jini, ugonjwa huu waweza kukuingiza kwenye ushirikina fasta ni hatari sana.. hospital nilikwenda na huko nikapewa dawa za kulala kwa muda mrefu na zingine hata sizifahamu .... baada ya muda mrefu nikapona..... namuomba sana Mola wangu nisije ugua tena ugonjwa huu,, nakuwaombea wengine pia... Ameen
asante kwa kuelimisha wengine. natumaini maelezo yako yatawasaidi kujua kua tatizo hili halisababishwi na ushirikina na kua linatibiwa hospitalin
 
Back
Top Bottom