Kama una stress pitia hapa, usiache kutupia na wewe maneno yako

Kama una stress pitia hapa, usiache kutupia na wewe maneno yako

TBT kule primary:
Andika insha ukianzia na........
*Nilipofika nyumbani, nilipata mama
amepigwa na butwaa...... (endelea)*
....nikakimbia mpaka kwa akina
butwaa.Nikamuuliza "Butwaa,mbona umepiga mamangu?" Nikampiga butwaa
mpaka akatokwa na damu.Hapo ndipo
niligundua damu ni mzito kuliko maji!!! [Emoji23][emoji23][emoji23]wat was wrong with us
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Cheka kidogo
Mke:Hili jiji letu siku hizi lina wasichana wazuri na warembo kweli sijui wametoka wapi ?
Mume:Sa wabaya watoke Wapi wakati wote wameshaolewa?
Namuona mke hapa keshabeba furushi la nguo I think anaenda kuzifua
 
Nimeenda hosipitalini kupimwa ugonjwa, matokeo yanakuja docta ananiambia eti choo changu ni mbaya... saizi nipo najenga nyingine, sipendangi ujinga mimi
Nadhani ulikuwa na cha shimo, sasa hivi jenga cha sink
 
TANGAZO Kama unajijua uliwahi kutembea na mimi nakushauri ukapime na ukiona hujapata majibu sahihi mchukue na mwenzio mkarudie kupima , tena nasisitiza mkapime ,maana nakumbuka mara ya mwisho tulitembea kutoka kimara hadi chalinze so sina uhakika na umbali huo
We Endelea tu kuwaza Ujinga ujinga
 
Jamaa mmoja alienda Benki na kuomba mkopo wa shilingi 200,000 ili asafiri kwenda Dar. Ofisa mikopo akamwambia lazima ajaze fomu fulani na awe na kitu cha kuweka dhamana. Mdau akajaza fomu kisha akakabidhi funguo za benzi yake aliyokuja nayo pamoja na nyaraka za umiliki wake kwa meneja. Ofisa mikopo akaiingiza gari kwenye yadi ya benki na kumpa mhaya laki mbili yake. Kilichomshangaza meneja wa benki ni kuwa benzi ile ina thamani ya Milioni 255,000,000 na kuwa iweje mwenye gari kama hii amekosa.
 
3586fd034994876a617d661dffa42db5.jpg


Wanakwaya wa AIC Makongorosi
 
Wadau Leo Nilikuwa najisikia kuumwa Nikaamua kwenda hospital kupimwa, baada ya vipimo daktari akasema vipimo vinaonesha Nina upungufu wa Madini Kwahiyo Naombeni mchango wenu ili Niweze kufika buzwagi au nyamongo ambako Madini huchimbwa ili niongeze mwilini ukijisikia unaweza kunipa hata mchango wa makinikia
 
Mwalimu mmoja alikuwa anafundisha darasani, wakati anafundisha kwa bahati mbaya akajamba! Basi wanafunzi wote wakaziba pua na kuanza kucheka, ndo mwalimu akaona ni aibu bora aombe likizo ya mwezi mzima ili wanafunzi wawe wamesahau. Mwezi ulipoisha akarudi na kuingia darasani,akawauliza wanafunzi,"Tuliishia wapi?" Wanafunzi:"Tuliishia pale ulipo jamba". Basi mwalimu akapigwa na butwaa na akaamua kuacha kazi jumla.
 
Back
Top Bottom