Kama una stress pitia hapa, usiache kutupia na wewe maneno yako

Kama una stress pitia hapa, usiache kutupia na wewe maneno yako

LEO HADI KIELEWEKE[emoji1321]

e9de6b36e5923e64e178a6df203b51fc.jpg

[emoji16][emoji16][emoji16]humu kuna wala Msuba
Wala Majani au wala Stick?[emoji16][emoji28][emoji28][emoji2]
 
*Manzi anakupenda balaa.. Anasubiri wewe tu umwambie ili muanze maisha matamu. Tatizo moja linajitokeza, we ni domo zege* [emoji134]♂[emoji134]♂[emoji134]♂
[emoji134]♂
*Unajikakamua usiku huo, unamtumia meseji kuwa unakitu kitamu sana cha kumwambia. Demu anakujibu kwa bashasha, niambie. Unakaa kimya dakika 10. Anatuma txt ingine kuomba umwambie.*
*Unaamua kughairi kumwambia kwa madai ni jambo la kipuuzi sana hasa kwa umri wenu. Ila demu anakusisitizia umwambie. Anakopa hadi salio na kukupigia akiomba umwambie hivyohivyo. Unaamua kumwambia kuwa utamwambia kesho Manzi hana jinsi, anaamua kutry to sleep with broken heart.*
*Kesho yake mtoto anajipara balaa. Tena anachagua saa 2 usiku ambapo tayari wazee wake wamelala. Mnakutana maeneo fulani ambapo watu si rahisi kuwaona. Unaanza porojo zako. Mara leo tumekula nyanya chungu, mara ukila dengu ukijamba ushuzi unanuka balaa. Hujakaa vizuri unaanza kuhadithia mkesha wa mwaka mpya. Mwishowe manzi anakuuliza jana ulitaka kuniambia nini? Tena huku kalegeza macho nadhani hata ubongo pia utakuwa umelegea. Chance pekee ambayo kamanda kama mimi nadokoa tu! Nafunga goli la kunyanyulia kombe*
*Unakaa kimya dakika kadhaa. Manzi pumzi zinapishana huku akili yake inawaza maneno matamu utakayoyamwaga. Na kweli, kimya kingi kina mshindo. Domo zege unaamua kufunguka uliyotaka kumwambia.*
*Unaanza kwa kumtaja. Naye anaitika kwa heshima. Unamwambia hili jambo ni la kipuuzi sababu ya umri wenu kutoruhusiwa na wazazi wenu na hata dini. Demu anakurekebisha, anakwambia hamna kitu cha kipuuzi kama tutaridhiana. Unafurahi kwa kukupa ahueni ya kuzidi kutiririka. Basi unaendelea kwa kumuita tena jina lake.*
*Unamwambia jambo nililotaka kukwambia.*
*Hapo unatulia kwa sekunde kadhaa kama vile MaMC wanavotaka kumtangaza Miss World. Binti Kimoyo kinaenda paa paa paa mpaka kitisheti kinafunuka*
*Unamalizia kwa kusema, naomba uniibie peni kwenye duka lenu*
*Kiukweli usipopigwa kofi na Malaika, utapigwa konzi na Shetani*
[emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13]
 
Mwalimu: Andikeni insha ukiwa kama mwanajeshi wa JKT vitani Somalia unapambana na Al Shabab, elezea mapambano hayo

Kayumba: (full mausingizi) [emoji42][emoji42][emoji42] fo fo fo

Mwalimu: Kayumba kwa nini Umelala wakati wenzako wanaendelea na kazi?[emoji34]

Kayumba: Yaani ile tunaanza tu vita nikafa[emoji25]

Mwalimu:[emoji35]
 
Pana jamaa alifariki katika mji mmoja sasa kutoka kwao mpaka mji alifariki pana umbali ikabidi watu waandae jeneza vizuri na wafiwa wakajitia penye pick up mpaka kijijini kwao baada ya mazishi lile jeneza wakawa bado zile shuka wameziacha vile vile kana kwamba pana mtu ndani.
Wafiwa wote walibaki msibani gari ikaondoka na tingo na dereva wake kufika mbele kuna jamaa akaomba lift wakamchukua ila wakamwambia asikhofu kuhusu jeneza wametoka kuzika so halina mtu ndani yake baada ya mwendo kidogo
mvua kubwa ikaanza kunyesha bwana yule akaona isiwe tabu akaingia penye jeneza na kutulia baadae kidogo mbele huko jamaa watatu wakaomba lift basi wakapanda vizuri na mvua ikaendelea kunyesha mpaka ikakatika sasa yule bwana ndani ya jeneza baada ya kuhisi kama mvua imekatika akapekenyua zile shuka huku akisema "ahh kumbe mvua imekatika "duh wale jamaa watatu walichupa toka ndani ya gari kama mkizi vile wakijua marehemu kafufuka.
 
Back
Top Bottom