Kama una stress pitia hapa, usiache kutupia na wewe maneno yako

Utoto bado sijaacha..!!

*Nimefika Ubungo stendi ya mabasi wapiga debe wakawa wanasumbua sana wananiuliza naenda wapi, nikajibu ZANZIBAR.*
*Nimewaacha nawasikia wanataja sehemu za siri za binadamu itakuwa wanakumbushana biology*

"Ideas are easy but Implementation is hard."
 
"Count your money before you leave the counter "sasa nipo hapa penye ATM nimemaliza kutoa pesa na kuikumbuka kauli hiyo hapo juu na pana foleni ndefu kiasi hapa nazozana na jamaa wananiambia nikae pembeni sasa kosa langu ni lipi jamani?
 
Mwanafunzi :baba nimeambiwa twende wote na mwalimu
Baba :tayari umeisha korofisha mambo huko?
Mwalimu :mzee nimemuuliza mwanafunzi kampala iko wapi?
Baba :weye mara ngapi nimekwambia uache kuchezea vitu vya watu haya sasa kampala ya mwalimu iko wapi? dogo akaanza kuchezea fimbo mpaka mwalimu ikabidi atoke nje na kuja na mwanafunzi mwingine huku akimwambia basi mzee tumeipata kampala.
 
Masai alienda kwenye Nyumba ya Ibada wakati wa kuinama ikatokea jamaa akawa amemgusa makalio kwa bahati mbaya. Masai akadhani labda ni utaratibu wa hiyo Nyumba ya Ibada na yeye akamgusa wa mbele yake makalio.

Jamaa wa mbele: Wewe Masai vipi? (Kwa sauti ya kunong'ona)

Masai akajibu: Imeansa huku nyuma endelesa huko mbele.

[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] Kweli Masai hawapendagi ujinga.
 
Ikiwa yapata nusu saa tokea kupaa kwake ndege moja iliyobeba abiria zaidi ya 200


..ikasikika sauti tokea kwa rubani ikisema "injini moja haifanyi kazi na iliyobaki haina nguvu kabisa ni wakati wa kufanya maombi kwani muda sio mrefu ndege hii inaanguka,tumieni nafasi hii kuombana msamaha ili mfike mbinguni salama."


Abiria wakaogopa sana na ukimya na hofu vikatawala.


David na Grace walikuwa miongoni mwa abiria wa ndege ile..


Grace: mume wangu nisamehe Aidan sio mwanao ni mtoto wa yule mlinzi,na hata kipindi umetekwa wakati umefuata pesa benki ilikuwa ni mpango wangu ili nipate pesa ya ada ya boyfriend wangu chuo kikuu.


David:wala usijali mamy,unisamehe pia kwa kuwa nishatembea na wadogo zako karibia wote kibaya zaidi yule mtoto wa mwisho wa mdogo wako Angel ni wangu japo mume wa Angel huwa anadhani anafanana na mwanenu Anita kwa sababu ni watoto wa Mama mkubwa na mdogo.

Basi watu wakawa bize kwelikweli kuombana msamaha na kusali. Ghafla ikasikika sauti ikisema
"Asante kwa maombi yenu hali ya ndege imetengamaa na tutafika salama"[emoji2][emoji2]


Watu wote "aaaaahhhh we rubani mjinga nini usitutanie sisi, we si umesema hii ndege inaanguka sasa iweje unageuza kauli ghafla?? tunasema ndege lazima ianguke hiii haiwezekani,kama imekushinda tunaiangusha wenyeweee[emoji35][emoji35][emoji35]

"Ideas are easy but Implementation is hard."
 
sijui kwanini naona haifurahishi
 
Pombe kweli mbaya, kuna mlevi Jana aliulizwa mwezi umepatwa umeuwona, akajibu "sijauwona mimi nafata saudia"
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]

[emoji252]You get what you work for not What you wish for [emoji252]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…