Kama una stress pitia hapa, usiache kutupia na wewe maneno yako

_*Kichaa baada ya kukuta folen kubwa ya maji,akawadanganya wa mama,yaani nyie mmekalia foleni ya maji wenzenu wanagawana nyama kuna gali limegonga ng'ombe kumi[emoji23][emoji23][emoji23]wamama wote mbio[emoji1322][emoji1322][emoji1322][emoji1322][emoji1322][emoji1322][emoji1322][emoji1322]kwenda kwenye nyama,walipotoka akachota ndoo moja,nae akatoka mbio kwenda kwenye nyama akisema inawezekana ni kweli[emoji1322][emoji1322]
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Dada mmoja alikwenda kwenye duka la wanyama kununua kasuku.
mambo yakawa hivi:
DADA: Nimekuja kununua kasuku.
MMILIKI: Nina aina mbili ya kasuku aina ya kwanza anarudia kila kitu unachozungumza na aina ya pili anafikiria mwenyewe kisha anazungumza"
Je ww unamtaka yupi?
DADA: Nadhani namtaka anayefikiria mwenyewe.
(MMILIKI akamletea dada kasuku kulingana na alivochagua kisha akaambiwa amfanyie majaribio.)
DADA: Naonekanaje?
KASUKU: Unaonekana kama kahaba.
DADA: "...kwa hasira..." "Siwezi kununua kasuku kama huyu! Hana adabu!"
MMILIKI: Samahani dada naomba unisubili kidogo.....(akampeleka kasuku nyuma ya duka na kumzamisha kwenye ndoo ya maji kisha akamuonya, "kama ukirudia tena kumkosea adabu yule dada ntakuja nikuloweke kwenye maji siku nzima.
". MMILIKI aliporudi kaunta akamuomba dada amjaribishe kasuku kwa mara nyingine na akamsihi akisema ".kwa sasa unaweza kumuuliza chochote naamini atakujibu vizuri bila matatizo yoyote"
MAJIBIZANO YAKAWA KAMA HIVI:
DADA: Kama nikirudi nyumbani usiku wa manane na nikaja na mwanaume huyo mwanaume atakuwa ni nani?
KASUKU: Mume wako!
DADA: Vizuri! vipi kama nikija na wanaume wawili?
KASUKU: Mume wako & shemeji yako.
DADA: Vzuri! Vizuri sana" kama nikija na wanaume watatu je?
KASUKU: Atakuwa ni mume wako,shemeji yako na kaka yako!
DADA: Waooooooo!!! Vipi kama nikija nyumbani na wanaume wanne?
KASUKU: (Akageuka nyuma akamwangalia miliki wake ) . . . . kisha akasema "Tafadhali kaniloweke kwenye maji, nilishasema mapema kwamba huyu mwanamke ni kahaba!!!
[emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji124] [emoji125] [emoji125] [emoji377] [emoji377] [emoji377]
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] inawezekana ni kweli [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] Nadhani kasuku alichoka kudanganya
 
[emoji23] [emoji23] [emoji119]
 
Hii [emoji116] ikikupata utafanyaje?

*Unatembea kilometa 10 na begi mgongoni kwenda kazini. Unafika pale kazini kwako unagundua kwamba funguo za ofisi umezisahau nyumbani. Unarudi nyumbani ukiwa na hasira na unaamua kuacha begi mlangoni pa ofisi. Unapofika Nyumbani unagundua huna funguo za mlango wa Nyumba yako na unakumbuka zipo ndani ya begi uliloacha kwa mlango wa ofisi. Unaporudi ofisini kuchukua funguo, unaamua kubeba begi lenye funguo unarudi nalo nyumbani. Ulipotoa funguo za mlango wa nyumba ktk begi ndipo unagundua kwamba funguo za ofisi pia zipo ktk begi* [emoji38][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
 
*TANGAZO.*
*Jamani wanagroup tungefanya mpango ili mtu akiumwa tuwe tunaenda kumtembelea na kilo 3za mchele kila mmoja.nyama kilo 1,mafuta lita 3 ,viungo vya pilau na pesa kidogo hata elfu 50.na kama tumeelewana tuanze leo maana mwenyewe sijisikii vizuri nahis naumwa*
[emoji39][emoji39][emoji39][emoji39][emoji39][emoji39]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…