Kama una stress pitia hapa, usiache kutupia na wewe maneno yako

dunia isingetoboka kusingekuwa na jua wala mvua, wazee wa zamani walikuwa na akili ya kuzaliwa ni kweli kabisa dunia ni tambara limetoboka

[HASHTAG]#WapostPumba[/HASHTAG]​
 
Wakati huu wa baridi, mademu wembamba mapaja yao ni ya baridi kama panga lililolala nje.. 🙂 🙂
Wewe umeacha nikacheka kwa sauti [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] jamani jamani haya sawa
 
We unaumwa ile pale yanga c
 
[emoji3]hii imenigusa saana mkuu[emoji3]majuzi kati na mimi yalinikuta,nlichkua dem mwenye miguu kama ya mange kimambi[emoji3]alfajir kumgusa paja nlihisi kama natoa soda ilioganda kwenye friji[emoji3]
[emoji23] [emoji23]
 
watu kwa uchokozi.! hivi ukipigwa utalia kweli?
 
Nowadays before dating anyone ask them to bring a letter of recommendation from their EX. You deserve to know who you are dealing with....[emoji23][emoji23]
[emoji122][emoji122][emoji122][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] hahahha
 
Kweli ukipita hapa usipopata kitakachokuchekesha basi ww utakuwa cyo wa kawaida !! [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Mchaga baada ya kufa akaulizwa na malaika anayetoa roho: Mangi hapa ni njiapanda kulia ni Mbinguni na kushoto ni Jehanamu, Je unachagua kwenda wapi?

MANGI: Bwashee, mi nabaki hapa hapa njiapanda aisee.
MALAIKA: Kwa nini?
MANGI: Aisee, nikifungua duka hapa si nitapata wateja wa Mbinguni na Jehanam. Yani patakuwa senta ya hatari, supu na nyama choma muda wote. Hata we utafaidi, unavyoenda kuchukua roho unaniletea stock nakupa hela yako cash mkononi. Na kila ukipita hapa unapiga mchemsho wako wa ulimi na bia mbili chap kabla ya kuingia mbinguni.
Kwanza nashangaa Shirima alipitaje hapa bila kushika ploti, au alikufa amelewa sana?
 
Jana niligombana na mke wng, Akaniambia nibebe kila kitu changu niondoke, Bas kiustaarabu tu nikachukua nguo zangu,mwishoni nikambeba na yeye nikamuweka begani nikaanza kuondoka nae

hua sipendagi ujinga, amesahau na yeye pia ni wangu
 
[emoji23][emoji116][emoji818]

Wakati unafikiria dingi yako afe ili urithi nyumba, dingi nae anafikiria uanze kufa ili apangishe chumba unacholala.. hiyo inaitwa kufa kufaana.. [emoji23][emoji23][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] [HASHTAG]#Hatutaki[/HASHTAG] ujinga
 
Ladha ya bia ya 1 hadi ya 6..
Kwa wanywaji wazuri wa bia,

chupa ya kwanza [emoji481] huwa haileti hisia yoyote. Mnywaji humaliza chupa hiyo bila kuona matokeo yoyote zaidi ya kupoza koo… Na mara nyingi huwa mkimya, pengine huwa anasoma gazeti lake au kwa siku hizi anawasiliana na ndugu na jamaa kupitia simu yake.

chupa ya pili [emoji481][emoji481] kimsingi ndipo mazungumzo ya awali na wanywaji jirani huanza na haya huwa mazungumzo ya busara, yakihusu muelekeo wa ligi mbalimbali, siasa, idadi za ajali na kadhalika na wakati huu hata takwimu hutolewa zilizo sahihi….

Mtu anaweza kukutajia wachezaji wote wa ligi daraja la tatu la huko Ujerumani bila kukosea, hata idadi ya wachezaji wa Yanga bila kukosea.. Ila wakati huu kama unaanzisha mashindano ya kucheua ni wakati mzuri kwani bia ya pili huongeza hisia za kucheua.

Bia ya tatu [emoji481][emoji481][emoji481] huanza kumfanya mnywaji aanze kusikia furaha na pia huu huwa wakati ambapo karanga na korosho huliwa sana…. Pamoja na mazungumzo kuhusu mpira na siasa, ghafla mazungumzo kuhusu michepuko huanza kujitokeza…..

Bia ya nne [emoji481][emoji481][emoji481][emoji481] huanza kusababisha masikio yaanze kupoteza nguvu za kusikia kwani utaona mnywaji ghafla amepandisha sauti, na ukijumlisha na kuwa baa zetu huwa na muziki una kelele utadhani waliopo wote wana matatizo ya kusikia….. bia hii humsaidia kuongea kwa nguvu kushindana na kelele za muziki.

Bia ya tano [emoji481][emoji481][emoji481][emoji481][emoji481] ni hatari kidogo kwani ukiinuka kwenda chooni mara nyingi unarudi hujafunga zipu……na kipindi hiki ni kibaya kwa wanywaji wa kike maana unaweza kumkuta akienda chooni akijiangalia kwenye kioo anaanza kulia peke yake na kulalamika; ‘Mi sipendwi mpaka leo sijaolewa’ au ‘ Mume wangu sijui yukoje hanijali’

Japokuwa lazima isemwe ukweli ukifikisha bia hii, maisha ni raha sana unaweza ukaanzisha shoo ya kukata mauno katikati ya baa na kudai wewe ni mkali kuliko Shilole.

Kuanzia bia ya sita [emoji481][emoji481][emoji481][emoji481][emoji481][emoji481] na kuendelea, chochote utakachosema au kufanya ni wazi kesho yake asubuhi utajilaumu sana. ……. …Kuna watu husema ukilewa ndipo unakuwa mkweli, hivyo basi wakati huu hata bosi wako akitokeza unamueleza ukweli jinsi alivyo fala na hajui kuendesha kampuni.

Au unasema ukweli jinsi unavyompenda mke wa jirani yako ambaye mmekaa mnakunywa naye. Kimsingi uwezekano wa kutapika pia upo karibu na kama umekaa na mchumba wako huu ni muda ambao pia uchumba unaweza kuvunjika
 
Kimchepuko chako kinakuandikia meseji kama hii…

…Samahani baby kama unavyojua nimeokoka ,nimetubu kanisani lakini nabii kaniambia niwaombe msamaha wote niliowakosea.

Nimemkosea sana mkeo kwa kumwibia mumewe na nimepanga kuja kumwomba msamaha kesho ntakuja na nabii na Mchumba wangu mpya nilie mpata kanisani.

Samahani kwa usumbufu uliojitokeza lakini hilo ni kwa ajili ya utukufu wa bwana!!!

Wako Manka wa Magorofani[emoji28][emoji28]
 
Fikiria mko kwenye ndege angani mkisafiri,mko umbali wa kama futi 40 elf juu ya ardhi.Ghafla rubani anatoka kwenye chumba chake na kuja kwa abiria akiwa kifua wazi huku jasho likimtoka...anawatazama abiria kwa muda bila kusema kitu.Kisha anatoa kauli moja tu.."sijui itakuwaje!...wacha tuone!"...kisha anarudi kwenye chumba chake na kujifungia!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…