Kama una stress pitia hapa, usiache kutupia na wewe maneno yako

Mambo mengine muwe mnauliza abiria.

Saivi safari imeshindikana kisa mmasai kang'oa gia ya basi.

imekuwa hivi..Mmasai huyo na shuka lake kakaa karibu na dreva mbele na akawa makini sana na dreva. sasa tumefika Singida tukaenda kula wote yeye kabakia ndani ya gari.

alivyoona dreva anazungusha gia akafikiri anataka kung'oa ila imemshinda.

Tumetoka kula anamkabidhi dreva gia na kusema "yelow tayari nishakusaidia kung'oa ile chuma."
Hata hatujuw la kufanya.
 
Nilisikia konda wa basi akitoa matangazo kwa abiria wake kuwa wale wasiokuwa na ticketi waingie ndani ya basi wakatiwe, na Kila abiria achimbe dawa kabla basi halijaondoka as dereva akishaondoa gari hasimamishi.
Kweli luga gongana..
 
Nimecheka sana kwa kweli..[emoji23][emoji23]
 
Du
 
Kuna demu nilikuwa na date naye hapa mtaani,juzi tulitofautiana kidogo,akatupa line yake ya simu chooni,akaniambia hataki mawasiliano na mimi,akaniambia kati ya wale wanaume mbwa aliowahi kukutana nao mimi ni mmoja wapo,basi jana nikamuona amevaa vizuri katoka na boda boda,hakurudi tenaa,huwezi amini nilijistukia kweli mimi mbwa baada ya kujikuta nimekaa nje ya geti lao mpaka saa nane usiku nikimsubiri arudi na hajarudi,hii ni story ya kweli lakini
 
*Wote MKEO na MCHEPUKO wanapata mimba kwa wakati mmoja, wanajifungua na baada ya kupima DNA hakuna mtoto hata mmoja ambae ni wakwako*

*Hii ndo tunaita "KUPOTEZA NYUMBANI NA UGENINI"*
πŸ˜ƒπŸ˜œπŸ€”πŸ˜ƒπŸ˜œπŸ€”πŸ’ͺ🏾πŸ’ͺ🏾
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…