Kama una stress pitia hapa, usiache kutupia na wewe maneno yako

Kama una stress pitia hapa, usiache kutupia na wewe maneno yako

Jiandalie makazi hukooo
IMG-20190314-WA0103.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna dada mmoja akiwa katika gari lake njiani alikutana mzee aliyekuwa anauza mayai "Dada alimuuliza,'unauza bei gani yai moja?'Mzee akamjibu Tsh 250 mwanangu..!'akamwambia nitachukua mayai 6 kwa 1000 badala ya 1500 kama haukubali naondoka,,!' " Mzee akamjibu:'njoo uchukue kwa bei yako mwanangu yamkini huu ni mwanzo mzuri sababu sijauza toka asubuhi" : "Akachukua mayai na kuondoka huku akijiona mshindi,akaingia kwenye gari lake akaelekea mgahawa wa jirani na marafiki zake,hapo wakala na kunywa na kuagiza kila walichokihitaji,wanakula kidogo na kubakisha kingi kwa vile walivoagiza,akaenda kulipa bill,akaambiwa anadaiwa 95000 akatoa laki moja na kumwambia mmiliki wa mgahawa keep change(sitaki chenji)" : "Tukio linaezaonekana kawaida sana kwa mmiliki wa mgahawa ila lisionekane kawaida kwa mzee muuza mayai" ~Pointi ni hii~"Kwanini tunapenda kujionesha kuwa wenye nguvu tunaponunua kitu kwa watu wa hali ya chini ambao ndio wenye uhitaji zaidi na tunajionesha kutokujali tunaponunua kwa wasio na uhitaji" : "Wakati mwingine upo tayari ukanunue kilo ya sukari super market kwa bei ya 3500 wakati mtaani kwako kuna kijana ana kibanda kilo ya sukari anauza 2700" ~Upendo ni kitu kimoja,utu ni kitu kingine,ubinadamu ni Upendo uliofungamana na utu.
 
Back
Top Bottom