HAHAHAHAHAAAAAA DUH [emoji16][emoji16]
Ndege ilipata hitilafu angani Ndipo rubani akatoa taarifa kwamba ndege imepata hitilafu na itadondoka baada ya dakika 10. Ndani ya ndege kulikuwa na watu watano Lakini maparashuti yalikuwa manne tu.
Watu hao ni mchungaji, waziri, mwanajeshi, Msukuma na mwanafunzi wa chekechea, Mchungaji akasema yeye anategemewa na kanisa hivyo hapaswi kufa. Akachukua parachute akaruka. Waziri akasema wananchi wanamtegemea alete maendeleo, Akachukua parachute akaruka. Msukuma akasema familia inamtegamea akachukua parachute akaruka faster.
Wakabaki mwanajeshi na mwanafunzi wa chekechea. Yule mjeshi akamtazama mwanafunzi akamuonea huruma kisha akasema. Mimi najitolea kufa kwa ajili yako, we chukua hilo parachute lililobaki ujiokoe halafu mi ntakufa na hii ndege.
Yule mwanafunzi akajibu "usijali yamebaki maparashuti mawili" yule mjeshi akashangaa[emoji32][emoji32] akauliza mawili kivipi.? Mwanafunzi akasema YULE MSUKUMA KACHUKUA BEGI LANGU LA SHULE ALIDHANI NI PARASHUTI.
[emoji3][emoji3][emoji3]