Kama una tabia hizi 10, huwezi kamwe kufanikiwa kwenye maisha

Mafanikio makubwa hapa duniani ni kwa mtu kuupata UFALME WA MUNGU. Hakuna mafanikio yoyote zaidi ya hayo. Hata kama utakuwa na pesa na mali kuwazidi akina Ellon Mursk, Bill Gates, Mark Zuckerberg n.k. kama hujaupata UFALME WA MUNGU wewe bado hujafanikiwa na unaishi maisha ya hasara.
Hata kama utakuwa na elimu ya juu na maPHd na madegree ya kila namna, kama jina lako halipo kwenye UFALME WA MUNGU, wewe bado hujafanikiwa.
Amini nakwambia ukiupata UFALME WA MBINGUNI basi wewe umefanikiwa tayari maana vyote vinaharibika na kupita, mali na pesa na elimu ya dunia utakufa na kuviacha. Lakini UFALME WA MUNGU ni wa milele.
Jambo la muhimu kufahamu ni kwamba tupo hapa duniani ili tujifunze kwa bidii sana namna ya kuupata UFALME WA MUNGU, na tuutafute UFALME huo kwa bidii sana kuliko kitu chochote kile. Maisha ya duniani ni kama "chuo" au "shule" ya kujifunza namna ya kuupata na kuishi katika UFALME WA MUNGU. Hayo mambo mengine ya utajiri, mali na mapesa ni kikwazo tu ili Wanadamu wasahau lengo la wao kuwepo hapa duniani.
Sisemi watu wasifanye kazi, hapana, tufanye kazi lakini cha muhimu kuliko vyote kwanza ni kuutafuta UFALME WA MUNGU kisha hayo mengine yatafuatia baadaye.
Wachache sana wataelewa nimeandika nini.
 
Definitely [emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji1666][emoji119][emoji119][emoji119][emoji119][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji2957][emoji2957][emoji2957][emoji2957][emoji2957][emoji2957][emoji91][emoji91]
 
Umeelewa sema umeamua kucomplicate " much know"
 
utaskia mimi nilianza na kijiko sasa hivi namiliki Hotel
Mtakuja kuua vijana
 
Kwani amevunja Sheria ya nchi
 
Well said
 
Kuna Mpuuzi Mmoja ananicheleweshea Mafanikio yangu hivyo ngoja niitumie hiyo #7 ( kwa Kumtoa Kafara ) ili Utajiri unikimbilie kama wa Aliko Dangote, Patrice Motsepe, Moise Katumbi Chapwe na Mohammed Dewji.
 
Mahali pa kupata kwa ufupi nilikotoka na ninakokwenda kwa wale walioleta upinzani kwenye uzi huu kwamba nilivyoshirikisha hapa haviwezekani au havina maana. Nimekuwa naviishi na matokeo yake nimekuwa nayaona.
 
Tunawafahamu !! Mnaandika mbinu za kupata pesa ili watu watajirike, ja ajabu mnaanza kuzunguka kwa wenye fedha wawafadhili ili mchapishe mbinu zenu ziwe vitabu. Si mtumie hizo mbinu kupata fedha za kuchapia vitabu vyenu ????!
 
Tunawafahamu !! Mnaandika mbinu za kupata pesa ili watu watajirike, ja ajabu mnaanza kuzunguka kwa wenye fedha wawafadhili ili mchapishe mbinu zenu ziwe vitabu. Si mtumie hizo mbinu kupata fedha za kuchapia vitabu vyenu ????!
Sasa hiyo si ndiyo mbinu mkuu?
Au ulitaka kila mtu atumie mbinu unayokubaliana nayo wewe ndiyo awe sahihi?
Kuuza mbinu nayo ni mbinu pia.
Karibu mkuu ujifunze, ili uweze kuuza vizuri kile kilicho ndani yako.
Pitia comments za nyuma nimeweka kitabu cha Psychology Of Selling, kisome kitakusaidia sana.
 
"Utajiri" neno hili lina tafsiri nyingine ambayo hutumika mara chache sana,ambayo ni kukinai yaani kutosheka na kile ukipatacho kupitia jitihada za utafutaji huku ukichunga mipaka ya sheria za Muumba! Zingatia kukinai sio uvivu! Mambo manne yafuatayo yanafungua mlango wa utajiri; 1. Epuka kulala asubuhi baada ya kuamka....fanya kitu kv mazoezi,kusoma,ibada,tembelea wagonjwa. Unaweza kulala kama ni hapana budi baada ya jua kuchomoza. Bila ya dharura utalala time nyingine. 2. Usimfanyie khiyana kiumbe yoyote ukamkosesha kitu au kumchonganisha au kumzibia njia ya mafanikio. 3 Usiruhusu uvivu ktk kazi,kusoma,kusikiliza,kutafiti nk 4. Fanya ibada na maombi kwa wingi hasa kumuomba msamaha Muumba na uliowakosea. Zingatia ibada iwe SAHIHI. .......waambie nipo karibu naitikia maombi ya mwenye kuniomba.
 
Hawa ndo wale wanaopita na vitabu mitaani vyenye kanuni za jinsi ya kuwa tajiri πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
How to become rich. Alafu unakuta mwandishi wa kitabu alikopa pesa kupublish kazi yake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…