Kama unaamini uwepo wa Mungu, usiipite hii!

Brother kila kitu hapa Duniani unachokiona kimetengenezwa au kuundwa na muhusika Gari, pikipiki, nyumba, n.k hivyo hata Dunia, Jua , mwezi yupo aliyeviumba

Ata kama ndio umeviumba hivi vitu uje utunyanyase kwamba tusipo sifu na kuabudu utatuchoma moto. Ukiamua kumsaidia mtu msaidie bila masharti. Huko mbinguni yenyewe malaika wanasifu na kuabudu bila kuchoka na huku duniani anataka kusifiwa na usiposifu na kuabudu anakuwa mkali na mwenye wivu.
 

Hata kama hiyo qurani isinge kuwepo jua na mwezi vingekuwepo na angetokea mtu mwingine akaleta story za hivo ili kuwapa watu kazi za kufanya. Imagine dini zingekuwa hakuna unafikizir vatikani na Saudi Arabia wangekuwa matajiri wakubwa duniani. Unajua idadi ya watu watalii wanaoemda pale maka saudia kwa mwaka na mbuzi kondoo zinazo uzwa na kuchinjwa pale unajua maji ya zam zam yanauzwa pale shilingi ngapi mpaka kuyafikisha hapa Tanzania hapo bado italia kwa papa huu ni upigaji
 
Zikikaribia nyakati za mwisho, watu watakua wajuaji sana.

Hapana zama za zamani kulikuwa hakuna elimu na maarifa ila sasa hivi ni information age ukiwa mjinga umechagua mwenyewe elimu zote zinapatikana kwa lugha unayo ifahamu
 

Acha uoga mkuu sio kwasababu eti mimi sio mslam au mkristo basi hakuna nguvu inayo nilinda na kunitetea hapa duniani hiyo nguvu ipo lakini sio kama ya watu wa dini
 

Ayubu alifanya hayo unayosema ona kilicho mkuta. Mungu na shetani walipanga kumtesha ayubu wa watu hadi mke akamkimbia.
 
Acha uoga mkuu sio kwasababu eti mimi sio mslam au mkristo basi hakuna nguvu inayo nilinda na kunitetea hapa duniani hiyo nguvu ipo lakini sio kama ya watu wa dini
Kwa hivyo tunakubaliana kuna nguvu (Super Power)inayoweza kumlinda na kumtetea mtu duniani.
Wenzio hiyo nguvu wameiita Mungu.
Wewe unaiitaje?
 
Ukiona mtu anapinga uwepo WA mungu muweza WA yote ujue hajasoma au hajaelimika,

Kwa Sisi Wana AI tunajua elimu/ujuzi uliotumika kuumba ubongo ni WA Hali ya juu sana na sio accident, so lazima awepo muweza WA kufanya hilo na ndio maana tunamwita mungu Kwa maana anaweza kuliko yote,

Kwa wale madaktari watakwambia hivohivo, binaadamu Yuko perfect, na uumbaji huo usingewezekana bila kuwepo mwenye uwezo wa juu sana, na ndiyo yeye aitwaye mungu muweza wa vyote,

Ukisogea kwenye dunia, solar systems, viunbe wengine...... Ni the same

There must be the almighty to make everything perfect in the order you observe today. You don't need to see or touch the almighty, you just look around and you will see his creations
 
"Huwa nakasirika sana pale nipo kwenye mazungumzo ya maana halafu jitu linaingiza habari za Mungu, huwa natamani hata nilizabue makofi".
Mkuu, hiyo haitakuwa njia nzuri ya kumfundisha Ustaarabu kwamba kila jambo lina wakati wake.
 
Elezea kwa ushahidi kutoka kwenye Biblia tafadhari kama usemayo ni ya kweli.
 
Kwa hivyo tunakubaliana kuna nguvu (Super Power)inayoweza kumlinda na kumtetea mtu duniani.
Wenzio hiyo nguvu wameiita Mungu.
Wewe unaiitaje?

Hiyo super power sio mungu sisi tunaita energy na pia haitupi adhabu tukifa wala haituhukumu kwa chochote ikiwamo moto mkali wa jehanam
 
Aisee kama haujawai ona nguvu na miujiza ya Mungu bora ukae kimya kuliko kudhihaki.
Tena nakwambia siku ya hukumu watu watatoa hesabu kuhusu kila neno lisilofaa kwani kwa maneno yako utatangazwa kama mwadilifu au utahukumiwa.
 

Hivi wewe mkuu kungekuwa na mungu au kuna kwenda mbinguni unadhani wazungu wangegawa biblia bure au waarabu wangegawa hizo qurani bure au unadhani wanakupenda sana. Kwanini wasitafsiri vitabu vya kemia bailogia na jiographia wao wakakutafsiria biblia mpaka ya kabila lako? Hukiulizi ni mchezo huo wa kukutawala fikra zako. Wewe ndio umesoma alafu hukaelimika mzungu akupe kitu bure toka lini au mwarabu
 
Elezea kwa ushahidi kutoka kwenye Biblia tafadhari kama usemayo ni ya kweli.

Mkuu biblia nacho kitabu? Hivi unadhani mzungu anakupenda sana kukupa hiyo biblia au unadhani huku afrika kulikuwa hakuna mungu mpaka wakoloni walivyokuja na biblia ndio wakamleta mungu.

Kama huyo mungu wa biblia angekuwa mungu angekuja mwenyewe hapa afrika sio mpaka aletwe na wazungu wakoli waliokuja kuiba na kubaka wanawake wetu huku afrika.

Kama mbinguni ingekuwa kweli unadhani wazungu wangekupa biblia.? Dawa ngapi za kutibu magonjwa wanazo wanaficha ila biblia wakakupa bure. THINK
 
Shida ya kushiba hii. Hoja hazina mipangilio, unataka kuona watu wakicharuka then ujihisi mshindi kwa andiko lako. Anyway, amini unachokiamini.
 
Mkuu biblia nacho kitabu? Hivi unadhani mzungu anakupenda sana kukupa hiyo biblia au unadhani huku afrika kulikuwa hakuna mungu mpaka wakoloni walivyokuja na biblia ndio wakamleta mungu.
Kama huyo mungu wa biblia angekuwa mungu angekuja mwenyewe
Unahakika Biblia iliandikwa na hao wazungu unaowasema? na kwani hao wazungu sio binadamu kama sisi..!


Nb Haujajibu swali langu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…