Kama unaingiza faida ya Tsh. 30,000 na kuendelea kwa siku pita hapa

[emoji240][emoji240][emoji240]
 
Heshima yako mkuu, barikiwa sana.
Naaaam nipo hapa
[/
Mkuu nakubaliana na wewe kabisa. Kuna ofis moja niliiona imekaa local Sana na hapo hata TRA wakipita hata hawawezi kujisumbua kuingia,ila jamaa Yuko busy muda wote na mtonyo wa kutosha,hata ukitaka 2M pale unapata. Cha ajabu sasa hata mtu akifika anataka kuweka/kutoa buku jamaa haachi tofauti na hawa wanaopamba ofis zao! Kikubwa ni kuwaaminisha watu kuwa kwako watapata wanachokihitaji,watu watakuja Tu.
 
Nenda ukawe free lancer, achana na hizi kazi za motor & pestle, angalia una ujuzi gani jiunge na site husika za freelancing anza kutoa huduma kwa kutumia computer tu ukiwa umelala geto. Nb inachukua muda kufanikiwa kuwa mvumilivu.
 
Nenda ukawe free lancer, achana na hizi kazi za motor & pestle, angalia una ujuzi gani jiunge na site husika za freelancing anza kutoa huduma kwa kutumia computer tu ukiwa umelala geto. Nb inachukua muda kufanikiwa kuwa mvumilivu.
hii ni kitu gani? ebu ifafanue niielewe tafadhali

kama hautojali (nisamehe kwa kupoteza muda wako)
 


Kongole zaidi kwa wife!maana majority hawapend ishu hizo!karibu mkuu sana!
 
Duh mimi sijui nakwama wapi. Banda langu likiwa linaniingizia hivyo wallah ndani yamwaka nakuwa najengo
mkuu inawezekana, amini usiamini, mimi ninayo mabanda matatu now , halafu yote yapo karibu karibu tu, kila moja halishuki jumla ya kamisheni m 1 kwa mwez, hilo nililokuonesha picha huwa linafika total 1.5m

N.B
Location matters, hapa nilipo kuna mzunguko sana wa watu wengi
 
Tunaweka nyimbo,movie,season kwenye flash (zilizotafsiriwa na madj) hatuuzi bongo movie mana msako anytime...ofisi yaingiza 20000-25000 per day hapo sijatoa matumizi 8000 kwa siku pamoja na kipande cha mfanya kazi (siwalipagi kwa mwezi ni per day kila mtu afe na chake).

Alhamdu lillah now ziko ofisi 3 hii ya 3 bado mpya so haijafikia level ya 20-25 ipo kwenye 10000-15000.Kwa hizi ofisi tatu sikosi 40000 kwa siku.Huezi amini bado sijawa tajiri.Gharama ya kila ofisi ni 5-6 Ml....Kazi yangu sifanyii kwenye vibaraza nakodi frem so kodi kama kawa.

Changamoto ni kukosa wateja hasa walio kwenye matumizi ya CD so had mtu aje kwenye flash huchukua muda mana kila ninapofungua nakuwa kama ndio nawaamisha kwenye technolojia ya flash mana washazoea kukodi cd.
Changamoto ingine ni kukatika kwa umeme yan umeme ukikata na ofisi nafunga ( ila kwa sasa nimeweka vifaa vya electronics mf chaja earphones nk.
Changamoto ingine ni kupata kijana mzoefu wa kazi mana anakuja mteja anataka nyimbo ambayo yeye haijui labda anajua kuiimba kipande nk,Kutafuta mafile na upangaji yan ushapu na uzoe wengi huitaji muda kuwa katika lavel hii ila kwenye nyimbo huwa majanga hasa za zamani.
Changamoto ingine Kukesha usiku kupakua movie almost 21gb per day lazima itumike 20 usiku kwaajili ya movie 1gb mchana kwaajili ya nyimbo mpya (asante ttcl)
Changamoto ingine ni madhara ki afya ( long run) kwa kule kukaa muda mrefu kwenye kiti na kutumbulia macho kioo.
Changamoto ingine ni uwepo wa flash na memory card feki hii inatukosesha wateja mana mtu anakuja na flash umuwekee movie za 2000 ukitaka kuweka unagundua ni feki basi huwa hatuna haja ya pesa yake zaidi ya kumwambia flash yako ni feki hazitocheza tukikuwekea.


UPDATE 11 July 2024
Biashara ya library ishakuwa kimeo now studio kila kona.Movie zinauzwa bei ya mafungu tena yakutupa.
Nilishazifunga izo mbili nimebakiwa na moja noyo mauzo yameshuka imechezea kwenye 10k-15k kwa siku.

Hesabu iyo inakuwa kwa kuboresha kuwauzia na Zisizotafsiriwa HD so tunatumia router kupakua icho ndio kinachotuweka mjini kwani studio nyingi hawana au hawajui hata huko kudownload toka pirates sites.
 
Umewekeza uswazi au jamii ya kati? Samahani kama unaweza taja maeneo nije nijifunze kutoka kwako
 
Hahahaa umenikumbusha mbali sana, basi bhana kuna siku tunavuka boda kwenye zile harakati zetu zileee (najua usha nielewa). Kuna jamaa alikuwa kabeba viroba viwili za hizo mambo jamaa alikuwa anatetemeka njia nzima itakuwa ndio alikuwa anaanza. Ila ata kwa kule nako enda hiyo ishu iko poa tu alafu asikari wa kule wako peace sana ni kitendo cha kuelewana nao tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…