Nina boda boda mbili zinanipatia 20,000 per day. Mpaka sasa bado sijaonja mbichi ya hii bizne sijui huko mbeleni. Nimepanga hadi December nafunga mwaka na boda nane.
Kikubwa nilichobaini ni kuwajali hawa boda yaani usiwe siriaz sana siku aki dash we chukulia poa mwambie Ata adjust next day. Yaani ukiwa boss poa utaenda nao sawa tu.
Tupe mchanganuo chiefTunao ingiza wastani wa 5,000 kwa mtaji wa 6,000 - 14,000 tunatoa maoni wapi?
Laki na nusu mpaka laki na 80. Mie ninao ila hauna matairi. Ntakuuzia 130.Hiyo ya mikokoteni iko vizuri zaidi
Hivi mkokoteni mmoja unaweza kugharimu pesa kiasi gani mpaka kukamilika(matengenezo)@Fighter23,
Ndiyo mkuu. Kama utachukua kwaajili ya biashara kama nifanyavyo basi bei ya jumla itapungua boss. KaribuHapa inamaana utaniuzia hizo material?
Hapana mkuu, njia ninayotumia ni tofauti kidogo katika kuwafikia walengwa hivyo haiwezi athiri sana soko langu, tofauti na hilo sihudumii watu wa eneo moja, hii kitu naifanya ndani ya Tanzania nzima na Afrika mashariki kiujumla.Hivi hii biashara baada ya muda si itajifunga yenyewe? Namanisha Wanafunzi watakuwa wanatumiana hayo materials wao kwa wao.
Sent using Jamii Forums mobile app
Bado ni biashara mpaka sasa boss. Utofauti ni katika utafutaji masoko. Ukipata njia nzuri ya kupata wahitaji ni rahisi sana na ina matokeo makubwa sana.
Ni kucheza na saikolojia yao tu mkuu, wengi wanadhani wanadharauliwa kwakua wao ni bodaboda so ukiwakalipia wanadhani ni mmoja wao hapo watakuulia chombo chako makusudi kesho watakuletea mkweche wako nyumbani wakati washapata pikipiki nyingine. so kua boss poa inamfanya ajisikie chombo ni yetu wote na wanaitunza kwelikweli.Ila na sometimes kuwa poa sana nako kunaleta shida sana mkuu wakikuzoea
Sent using Jamii Forums mobile app
Wakuu kama kuna mtu anahitaji maelezo anaweza kunicheki kwa muda wake ila sema kweli, hii comment yangu imezua maswali mengi kwa baadhi ya wadau.
Nadhani weka hapa kwa faida ya wengi, hilo la kila mtu kukufata kwa muda wake sio poa.Wakuu kama kuna mtu anahitaji maelezo anaweza kunicheki kwa muda wake ila sema kweli, hii comment yangu imezua maswali mengi kwa baadhi ya wadau.
Ila niwahakikishie kuwa pesa ipo kama ukiamua kuisaka. Mimi nilikuwa mtu wa kulaumu sana na kuona aibu kufanya baadhi ya kazi kwan waliokuwa wanazifanya walionekana kama watu wa chini sana. Hata ukiangalia mavazi yao n ya ajabu ajabu kwa wengi wao. Ila nikajaribu kazi moja wapo. Kweli kabsa sijajuta make naona malengo zangu naanza kuzipatia njia. Nifanya kwa mtaji mdogo sana yani kuanzia 6000 mpaka 20000 tu napata faida ya mpaka 15000 kwa siku. Afu ni kwa masaa tyu. Kufikia saa 7 mchana unakuta nipo getto navuta pumzi tu. Saiv nimeanzisha na mradi wa kufuga kuku japo nimeanza kwa mtaji mdogo but baada ya muda nitaongeza.
Vijana wenzangu hasa wa maisha ya kawaida naomba tusichague kazi. Biasha haihitaji mtaji mkubwa sana but utayari wako na juhudi zako.
huwa siogopi kumshirikisha mtanzania mawazo yangu maaana najua wengi ni waskilizaji sio watendaji
so nafungukaga tu hata siogopi maana najua wanajua kuitikia wameelewa ila hawataki kuingia ktk utendaji
wengi ni waoga na wachagua fursa.
Mkuu mimi nilikua muoga zaidi yako
Jitoe tu, risk zipo kila sehemu
Nunua chombo utafute bodaboda mzoefu na anayeaminika kijuwe fulani mpe kazi akutafute dereva mzuri..usikurupuke
Sent using Jamii Forums mobile app
Hivi hii biashara baada ya muda si itajifunga yenyewe? Namanisha Wanafunzi watakuwa wanatumiana hayo materials wao kwa wao.
Sent using Jamii Forums mobile app
Habari wanajamvi, ninaendelea vyema na biashara ya maziwa ila kuna changamoto ya vifaa.ninauhitaji wa lactometer law ajili ya kupima ubora wa maziwa..thermometer ya kupima kiwango cha uchemkaji wa maziwa. Kitchen gloves hasa zile za colourless..nimeshindwa kuzunguka maduka mengi ya kariakoo kutokana na ufinyu wa muda..kwani nafungua saatatu asubuh nafunga sasita za usiku