Yaani stationery napiga picha nne sh 1,000 siku naweza piga hata 30...copy sh 100. Kuprint 500, kuchapa barua, hati, mkataba, au chochote kile...page moja sh 1,000 (pamoja na kuprint)
Kusafisha picha za kwenye simu, memory card...sh 400/pc au kama nyingi tutaelewana.
Mfano juzi kati hapa walikuja CCM wanataka niwaandalie karatasi za kupiga kura serikali za mitaa. Ile siku nilimaliza ream 7....kazi nikaelewana nao tu wakanipa sh 50x500x7 nikapiga plus vitu vingine vingine wakaniachia kama laki 2 hivi kwa kazi ya masaa 5....
Siku hizi kuna watu wanaandaa katiba za vikundi, yaani kazi ni nyingi mno watu wanataka kuandikiwa (typing). Form 6 kibao wanataka kwenda chuo wakija kuprint maform yao ya chuo....unakula kichwa, lamination....n.k
Siku hizi watu wengi wanajaza form za NIDA, so wanapiga picha passport size waende nazo serikali za mitaa. Nimechukua ile form A1 ya NIDA nimeitoa copy....unachangia 200 ya copy nakupa form....au ukipiga picha ya passport size....form bure. N
Mimi stationery yangu siuzi makoro koro mengi kama maua....yaani pale ni print works tu. Pale nauza peni tu na counter books, chalks,shelfu langu ni nusu ukuta wakati kuna kuta 3...print works tu ndio zinanilipa. Technically unahitaji mtu anayejua kucheza na publisher, word, excel kidogo, adobe....utapiga hela sana. Ninawasichana 2 wa kunisaidia kazi na still kunakuwa na foleni kiaina.
NB: Ofisi ipo sehemu ya uswazi ambako layman ni wengi wasiojua hata basics za computer. Huwezi kufungua biashara hii maeneo ya Survey ukapiga hela.