Kama unaingiza faida ya Tsh. 30,000 na kuendelea kwa siku pita hapa

Kama unaingiza faida ya Tsh. 30,000 na kuendelea kwa siku pita hapa

Nauza iPad wakuu usijali kuhusu bei
0742537423
IMG_20200716_180659_0.jpeg
 
Thanks
Salooon local ya kunyoa watu,usiweke zile mbwembwe

sijui akimaliza kunyoa aoshwe then apakwe mafuta,hakikisha kazi yako ni kunyoa tu

mtu akishamaliza kunyoa Asepe zake akaoge kwao huko

Nyoa mtu mzima 1500, mtoto 1000

Wakija watu wazima wakikuomba uwanyoe kwa 1000 usikatae Wanyoe

Jioni unaondoka na zaidi ya 40k

ILA TU

saloon iwe yako na wewe kinyozi ndio uwe boss
 
Biashara ya kuuza earphones inalipa sana hasa maeneo yenye mikusanyiko ya watu kama stand n.k

Faida kwa pc moja ni kati ya sh500 mpaka sh 1500 au zaidi

Uhitaji ni mkubwa maana watu wengi wanashindwa kununua earphone original ambazo ni ghali sana

Kariakoo unanunua kwa bei ya jumla ambayo inaanzia sh 1000 kwa pc na kuendelea na mtaani unauza kuanzia sh1500 na kuendelea . Ukifanikiwa kuuza PC 20+ kwa siku tayari una 10k+ mfukoni. Tembelea maeneo ya stand uone watu wanavyopata hela kupitia hiyo biashara. Wengine wameongeza vitu kama chaja, protector ,cover n.k lakini kwa upande wa earphone naona ndio zinatoka sana.
 
Shida hamuweki Bei...sijui kwanini
Tunaanza 150, 000 kwa siku, kwa choo kimoja.
Kama ukichukua viwili yani kwa ajili ya wanawake na wanaume ni 130, 000 kwa kimoja.

Kama ni zaidi ya siku moja kwa choo kimoja ni 130, 000 kwa siku.

Kama ni viwili basi ni 120, 000

Long term, unakodi zaidi ya mwezi bei ni 100, 000

All figures in Tanzanian shilings
 
Miezi miwili iliyopita nilikua najihusisha na biashara ya vipodozi vya usoni vya wanawake..nilikua natumia mtaji wa tsh 30000 kwa siku nilikua naweza kupata wateja si chini ya 5 hadi 6 na kila bidhaa nilikua nauza 30000.. kwahiyo nilikua napata hadi laki na nusu faida..ila tatizo ilikua inachosha Sana na nilivyopumzika ndiyo nikapumzika mazima.
Ulikua unauza kwa kutumia strategy gani?


Na je naweza kuviuza kwa wazi wazi kama kariakoo pale?
 
Biashara nyngne inayolipa ni sales, nunua pikipiki yako then chukua Bidhaa kutoka kwenye maduka ya jumla zungusha mtaani, 30k faster tu, kama mtaji unaruhusu nunua kirikuu minimum profit apo 50k, ushawahi kujiuliza why hiz selling companies inakikirikuu tu na mtaji usiozidi 10m lakn wanamlipa salesperson 400k, wana HR, accountants,managers, madepartments kibao na wanawalipa handsomely, they pay bills kama rent kwa mamilion ya hela kwa hicho hicho kikirikuu?
Elezea hapa
 
- So far narecommend tumia pepperstone broker

- Deposit kwa credit card (ABC Bank au Equity) direct inakata, within 2 minutes

- Withdraw direct to credit card (ABC Bank) , inachukua siku 2 - 3

- Mpesa option ishakua kimeo mpk hapo watakapo resolve na BoT. Lini hatujui
Habari mkuu. nilikuwa nahitaji msaada wako. Nimeku PM naona umefunga
 
Mimi nauza matunda kwa siku mauzo hadi 70elfu nikitoa faida hadi 33elfu napata kwa siku. Nacheza mchezo(kibati) watu mia na ishirini, jina moja ni tsh 2000 ivyo nacheza majina matano kila daily ten. Kwenye faida yangu ya 30elfu natowa ten ya mchezo nabakiwa na 20 hivyo kwa mwezi kikosi M na laki sita ..bila makato yeyote maisha yanasonga.
Achilia mbali na trade forex na kuuza mchele.

Baada ya hapo nakuja kuilaumu serikali.
 
Back
Top Bottom