Kama unaingiza faida ya Tsh. 30,000 na kuendelea kwa siku pita hapa

Kama unaingiza faida ya Tsh. 30,000 na kuendelea kwa siku pita hapa

Kama kitu ni halali kimenyooka hakina shida na wala si haramu kwa serikali, unakaaje uchi kwa mfano? mbona kuna mwamba mmoja huko juu kameza rula na kanyoosha maelezo yeye anauza bangi na imemtoa?

... huku tunachotafuta ni akili za kuambiwa alafu mtu anachanganya na za kwako, anatoka na idea yako wewe mwenyewe... akiamua kukopy idea ya mwingine sio dhambi, maana kila mtu anauwezo wake binafsi wa kuendesha biashara yake.... mfano inawezekana wote tumejipanga tunauza spare ila wateja wakaja duka langu kwa wingi sababu labda nahuduma nzuri, kila spare nayouza namwelekeza mtaja ubora na ubaya wake, kulingana na kipato chake, au nkampa Fundi for free akienda mfungia nakadhalika...

Sasa wewe ndugu yangu unaona huo mtaji wa 60M ndio kama roho ukitoa siri ya kupata 300,000 kwa siku utakufa... hutakufa, wala hakuna atakaeshindana na wewe baba, maana huwez jua mtu yuko wapi au nchi gani na anafanya nini...ila unaskitisha na kukuonea huruma kwa spirit ulionayo, hata nikipima majibu yako naona bado niyakitoto sana bado hujakomaa pia sio kosa lako "WABONGO" ndio tabia yenu
Hatar sana , only in bongo land! A bongo man can dearly give you gossip news of the town or a cret of beer, not a million shilling deal !
 
Mtaji wa buku kwa siku 3 (bando)
Smart fon fulu chaji..
Naanza udalali mtandaoni..
Sikosi elfu 10 sometime hata laki

Anyway nauza (kama dalali) viwanja mashamba gari used pikipiki used hapa hapa Dar.
Call 0744033555
 
Wewe ndie mbongo mtanzania halisi... wanasema "Kuliko mbongo akupe ushirikiano, mbinu, fursa au njia ili na wewe ufanikiwe ufike malengo yako ndio kwanza anakukatisha tamaa" ukitoa idea kumsaidia mwingine haimaanishi atakupita kwa mafanikio ulionayo au utafilisika wala...

Dunia ni kubwa sana ndugu yangu na kuna fursa matrilion na matrilion wala hatuwezi kuyamaliza mpaka mtu unarudi kaburini... kuunga unga mjini ndio biashara gani sasa... kama sio majibu ya kihuni na ya kitapeli...

Kuna watu wanafanya biashara kubwa sana kwa mitaji ya mara tano ulionao na wala sio wachoyo wa kukuonyesha njia na wewe ufanikiwe... kwa style hii bongo tupeane Umbeya tu ila deal za maana tuwaachie ngozi nyeupe waje kuzifanya huku huku kwetu sisi tubaki na umbea, majungu, fitina, ushirikina na yanayofanana na hayo...
Nimecheka saaana mkuu, bongo ni laaana boss asikwambie mtu , watu wana roho mbaya kinyama , mbongo kukupa connection ni ngumu Kama nyama ya pumba
 
Salooon local ya kunyoa watu,usiweke zile mbwembwe

sijui akimaliza kunyoa aoshwe then apakwe mafuta,hakikisha kazi yako ni kunyoa tu

mtu akishamaliza kunyoa Asepe zake akaoge kwao huko

Nyoa mtu mzima 1500, mtoto 1000

Wakija watu wazima wakikuomba uwanyoe kwa 1000 usikatae Wanyoe

Jioni unaondoka na zaidi ya 40k

ILA TU

saloon iwe yako na wewe kinyozi ndio uwe boss
Hizi ndizo points zenye mashiko
 
Nauza mkorogo 😂😂 vifaa vinanigarimu 50000 natoa kopo 10, kila kopo nauza 25000. Kwa siku naweza kuuza kopo mbili mpk nne. Wateja Facebook na Instagram. Na business nyingine ila hii ndio inanipa faida kubwa.
Naomba unifundishe jinsi ya kuutengeneza ili nami jijue niweze kufanya hiyo biashara tafdhali
 
salaniatz, Additional nje studio yan mimi binafsi mana studio wapo vijana so muda mchana sikwamba napiga soga au kuranda mitaa. Niko huku
1.AdSense App
2.Whatsap Group
Hizi nikwa wale wadau wa movie walioko mbali
Hapo 22 members unatoa 3 mimi na washikaji zangu wa2 ndio sio wateja wengine 19 kila mmoja 5000 kwa mwezi 19 X 5000=95000 kwa mwezi makadirio ni kuongezeka sio kupungua.

Gharama za AdSense na WhatsApp
Nalipia 13000 app kila mwezi 66$ mwaka
Nalipia link za movie 12000 kila mwezi ( mimi sio dj so nauziwa)
Nalipia 22000 kila mwezi Google drive>2Tb
Nalipia 30000 kila mwezi bluehost>hosting
Jumla kwa kila mwezi 77000 maximize 80000 kila mwezi.

Sasa chukua
WhatsApp 95000 kwa mwezi
AdSense 800000+ kwa mwezi hupanda kila mwezi
Ofisi 3 kwa mwezi 1200000 ( studio/library) 40000/day
Jumla 2095000 maximize to 210000/month
Toa kod za frem zote 3 (50+70+80) 200000
1900000 remain take home iyooooo.....

Hapo sijaongelea kabisa ivyo vifaa vya simu chaja nk coz ndio nimeianza so cna makadirio yake exactly.

Kuna kipindi niliwahi kushare mauzo ya izo ofisi ikioshesha mauzo katika $ ila ni tsh sema program cjajua namna yakuibadili kuwa tsh but ninachokiangaliaga ni namba za pesa digits yan unakuta kwa siku nimejaza jumla ya mauzo $20000 lakini hii ni tsh sio $.

HIVI NI HATARI KUSHARE TAARIFA ZANGU KAMA HIVI....BAHATI MBAYA SINAGA UCHOYO KUSHARE KILE NINACHOONA NINAFANYA KATIKA HAZIRA YA WATU NAAMINI KILA MTU NA BAHATI YAKE...NIMEEHUDIA WATU WENGI WAKINISHANGAA KWA NINI NINAMOYO HUU KUTOA NONDO HIZI NA NAMNA NINAVYO FANYA BUREEEE BILA KUFICHA.KUNA MMOJA HADI AKAWA ANADUWAA ANASEMA WATU KAMA NI NINYI NIWACHACHE SANA.....

LABDA NA WEWE WAWEZA KUWA SHUHUDA WANGU KWA UCHACHE HUU INGEFAA NIFUNGUE UZI WANGU ONE DAY YES...ILA KWA MLIOKO MOROGORO KARIBUNI SANA 0713055107
Usinipigie simu kuniuliza juu ya haya ila nitafute ukiwa Morogoro tupeane ideas hasa za biashara iyo AdSense usiitamani.


View attachment 1278568View attachment 1278573View attachment 1278575

UPDATES
BAADA YA ADMOB KUNIWEKA ROHO JUU KILA SIKU YAN KILA MWEZI NAPATA ADS RESTRICTED,,,,ADS SAVING LIMIT SO NAKUTA MWEZI MZIMA NINA DOLA 15.....NOW NAUZA KWA SUBSCRIPTION TU.NIKO NA SUBSCRIBER ZAIDI YA 130 HII INAMAANA 5000X130+=650000+ KWA MWEZI.......
GHARAMA ZA UENDESHAJI
NALIPA MADJ KUPATIWA MOVIE KILA MWEZI JUMLA 40000 (KILA DJ NA BEI YAKE WENGI NI 2000 KWA WIKI SAWA NA 8000 KWA MWEZI)
NALIPA WEBSITE HOST 35000 KILA MWEZI
NALIPA GOOGLE DRIVE 112000 KILA MWEZI (10TB)
INTERNET KILA SIKU 1000=30000 KILA MWEZI
KUNA APP NNAYOLIPIA KWA MWAKA AMBAYO NI SAWA NA 13000 KWA MWEZI
JUMLA COST KWA MWEZI 40000+35000+112000+30000+13000=230000.

KUMBUKA WATEJA WANAONGEZEKA BAADA YA KUFUNGA LINK NA KUZIFUNGUA KWA SUBSRIBER TU HIVYO KUNA RATE YA 1 SUBCRIBER PER DAY NIKIMAANISHA WANAONGEZEKA 30 KILA MWEZI HIVYO HUENDA KUFIKIA MWEZI WA 3 MWISHONI WAKAWA 200+.
INAGHARIMU MWAKA KUIJAZA 2TB SABABU KWA WIKI NAKUSANYA GB 60-80.
KUMBUKA INANIGHARIMU MASAA 6-8 KWENYE KITI NIKITUMBULIA MACHO COMPUTER.
KUMBUKA TOA PESA UPATE PESA NDIO MFUMO HAI KWANGU
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2021-01-20 at 13.13.09 (1).jpeg
    WhatsApp Image 2021-01-20 at 13.13.09 (1).jpeg
    35.1 KB · Views: 57
  • WhatsApp Image 2021-01-20 at 13.13.09.jpeg
    WhatsApp Image 2021-01-20 at 13.13.09.jpeg
    15 KB · Views: 55
Back
Top Bottom