zerominus10
JF-Expert Member
- Aug 25, 2022
- 8,142
- 13,721
Amina, Mama Mtumishi barikiwa kwa maombi hakikaHuu ni mfano(mwongozo tu) wa jinsi unavyoweza kuomba asubuhi, mchana au usiku:
"Baba wa Mbinguni, kwanza nakushukuru kwa kuniokoa na kuniahidi kuwa nikiomba lolote utanipa. Nakuja mbele zako sasa kwa unyenyekevu nikiwa na hitaji langu hili(taja hitaji lako). Ninaamini kuwa Wewe Mungu una uwezo wa kunisaidia au kuniongoza katika njia sahihi. Naamini utanipa kama ulivyoahidi. Napokea kwa imani majibu ya hitaji hili.
Katika jina la Yesu Kristo, Amina."
Asante kwa ushuhuda mzuri. Ubarikiwe sanaKabla ya maisha yangu kufichwa ndani ya Kristo katika Mungu nalikuwa mtu wa namna zaidi ya hiyo hasira,chuki,kukataa maonyo,kutokukubali kukosolewa na Mambo mengi ya namna hiyo.
Lakini kwa sasa ni historia uniseme,unitukane,unidhihaki,unisingizie uongo,unionye hainiumi na hainisumbui Kama zamani kwasababu mimi siyo tena mtu wa ulimwengu huu,na Kama siyo mtu wa ulimwengu huu kwanini niingie kwenye migogoro na watu wa huu ulimwengu?
Ni kweli kila binadamu anaweza kukasirika, na hasira mara nyingi huja bila ruhusa. Hata hivyo, Biblia haituhimizi kukasirika, bali inatufundisha kuitawala ili tusitende dhambi.Hakuna binadamu asiye kasirika ,mm nadhani mada yako ingekuwa na mantiki iwapo ungesema mtu asiye weza kudhibiti hasira zake ni mpumbavu.
Hasira haitaji ruhusa yako kuingia ndani ya kifua chako huwa inakuja automatically baada ya kufanyiwa kitu usicho kipenda au cha kuudhi ila kitendo utakacho fanya baada ya hiyo hasira ndo kitakuhukumu iwapo ni mpumbavu au ni mwenye busara.
Huwezi kuniambia eti mwizi aniibie alafu nisiwe na hasira naye, au mke wangu nimfumanie anafanya uzinzi eti nisikasirike ww utakuwa sio binadamu bali utakuwa ni robot.
Wanaotafuta kujua siri ya kushinda hasira, Siasa mbaya sana amefichua siri hiyoKabla ya maisha yangu kufichwa ndani ya Kristo katika Mungu nalikuwa mtu wa namna zaidi ya hiyo hasira,chuki,kukataa maonyo,kutokukubali kukosolewa na Mambo mengi ya namna hiyo.
Lakini kwa sasa ni historia uniseme,unitukane,unidhihaki,unisingizie uongo,unionye hainiumi na hainisumbui Kama zamani kwasababu mimi siyo tena mtu wa ulimwengu huu,na Kama siyo mtu wa ulimwengu huu kwanini niingie kwenye migogoro na watu wa huu ulimwengu?