Kama unaogopa hasara, baki na hela zako

Sikia....

Mzee Mengi alikuwa na gazeti linaitwa ALASIRI. Halikuleta faida. Gazeti la Dar Leo vile vile. Ushindani wa magazeti mengine ulikuwa mkali. Wasomaji wakabadilika. Internet zikaingia nk.
Akaachana nayo. Afu wewe eti unataka ufundishwe biashara ambayo hutaki kupoteza hela. Kaa na hela zako tu kwa kweli.

Hivi unadhani Novida imeenda wapi. Kama Coca Cola wanakosa soko la bidhaa yao wewe je? Lakini CocaCola wamefilisika? Mengi amefilisika? No.

Okay, tufanye hivi, ule ukumbi wa Sinema pale Mwenge ITV ulikufa kifo cha fasta. Competition. Century Cinemax ilileta upinzani. Wenye mradi wakajifunza.

Kuna matajiri wengi tu walipoteza sana pesa. Mabasi ya Scandinavia yapo tena? Kuna maduka mengi tu Kariakoo yamefungwa kipindi hiki.
Ni kawaida kwenye ulimwengu wa biashara. Si uliona Landmark Hotel Ubungo ilibadilishwa ikawa hostel. Umeona jinsi ambavyo tayari amerejea na kuwa hoteli ya kisasa zaidi. Alishajifunza. Sijui unaelewa?

Dar Village hapo Rose Garden Kijitonyama haijajengwa hadi leo. Mradi wa mabilioni uliingia mdudu miaka zaidi ya 8 sasa. Wewe unataka utakachoanza nacho kisife. Hela zako hutaki zipotee. Aisee you're not an entrepreneur. Kaa tu na hela zako. Bora ukazinywee soda tu au kula nyama choma kama unataka. Umekuwa mtu wa kutaka mafanikio yasiyo na changamoto yoyote. Ndo maana unasubiri ukiambiwa aisee biashara ya Matikiti inalipa hatari huyo umo. Ukiambiwa mayai ya kware yanalipa huyo. Hutaki kutulia kwanza ujifunze.

Hakuna biashara isiyolipa. Ila kuna akili zisizo za kibiashara ambazo lazima kuzibadili zijue biashara faida na hasara ni kawaida kabisa. Wanasema SOMETIMES YOU WIN AND SOMETIMES YOU LEARN.

Sasa wewe hutaki kulearn utafikaje kwenye mafanikio kibiashara?

Trump mwenyewe alifilisika kabisa. NIL. Zero. Rock bottom. Licha ya kuanza kwa mtaji mkubwa. Kama haupo tayari kukosekana pesa basi kazinunulie nguo mpya sikukuu zikifika uvae.

Na hiyo ndo maana kuna matajiri wachache. Wenye moyo wa UTHUBUTU katika jamii huwa ni wachache tu.

If you're afraid to lose money NEVER INVEST. Baki na hela zako.
 
dahh makini sana!! mwenyew napitia changamoto mno kibiashra but,, umeniongeza nguvu mkuu. nashukuru
 
somo zuri,linatufu disha kuhusu survivorship bias,ila hapo kwa trump kuna ukakasi kidogo,kufile for bankruptsy haimanishi kuwa huna kitu kabisa,hata homeshoping center wali file fo bankruptsy wakaja kuibuka kama GSM.ile ni tekniki tu ya wafanyabiashara
 
Not taking risk at all is the biggest risk.

Na mara nyingi wanao ogopa hasara ni wasomi. Theory nyingi kichwani lakini kwenye kuifanyia kazi ni utata.

Wanataka kabla ya kuanza kufanya kitu wasione upenyo wowote wa hasara. Na kutanguliza neno kama isiponilipa je?

Tujifunze kujitoa muhanga
 
Kuna njia moja tu za kuepuka hasara,
Uache kbsa kufanya unachohc kitakupa hasara, kinyume na hapo ni kua makini ku minimise hasara. Kupitia hasara ndo weng hujifunza cha kuepuka hapa n ile kujifunza kwa gharama/hasara kubwa
 
Kupata hasara kunauma lakini ndo kujifunza kwenyewe
 
Umeandika ukweli mtupu na naongezea invest Money you can afford to lose. Ingawa kikubwa ni jifunze ku invest bila kuogopa hasara.
 
no lazima ujue risk ya kila kitu ndipo ufanye uwezi ingia kichwa kichwa tu ufanye kitu oooh weee pesa yoyote inahuma hata hao uliowataja waliweka pesa coz walijua ni opportunity before xo me nadhan umakini unatakiwa ila kufeli iwe bahati mbaya
 
Kila biashara inalipa, na kila biashara ina hasara, kinachotakiwa ni kujifunza pale unapopata hasara, maana ni lazima kuna mahali umekosea, na sio kuachana na hiyo biashara.....unatakiwa kujiuliza kwanini wewe umepata hasara lakini kuna mwenzako anafanya biashara kama yako na anapiga faida ya kutosha?

Kukata tamaa ni mwiko kwa mjasiriamali. Kama unaogopa hasara wewe huna sifa za ujasiriamali. Baki na hela zako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…