Kama unaogopa hasara, baki na hela zako

Kama unaogopa hasara, baki na hela zako

Sikia....

Mzee Mengi alikuwa na gazeti linaitwa ALASIRI. Halikuleta faida. Gazeti la Dar Leo vile vile. Ushindani wa magazeti mengine ulikuwa mkali. Wasomaji wakabadilika. Internet zikaingia nk.
Akaachana nayo. Afu wewe eti unataka ufundishwe biashara ambayo hutaki kupoteza hela. Kaa na hela zako tu kwa kweli.

Hivi unadhani Novida imeenda wapi. Kama Coca Cola wanakosa soko la bidhaa yao wewe je? Lakini CocaCola wamefilisika? Mengi amefilisika? No.

Okay, tufanye hivi, ule ukumbi wa Sinema pale Mwenge ITV ulikufa kifo cha fasta. Competition. Century Cinemax ilileta upinzani. Wenye mradi wakajifunza.

Kuna matajiri wengi tu walipoteza sana pesa. Mabasi ya Scandinavia yapo tena? Kuna maduka mengi tu Kariakoo yamefungwa kipindi hiki.
Ni kawaida kwenye ulimwengu wa biashara. Si uliona Landmark Hotel Ubungo ilibadilishwa ikawa hostel. Umeona jinsi ambavyo tayari amerejea na kuwa hoteli ya kisasa zaidi. Alishajifunza. Sijui unaelewa?

Dar Village hapo Rose Garden Kijitonyama haijajengwa hadi leo. Mradi wa mabilioni uliingia mdudu miaka zaidi ya 8 sasa. Wewe unataka utakachoanza nacho kisife. Hela zako hutaki zipotee. Aisee you're not an entrepreneur. Kaa tu na hela zako. Bora ukazinywee soda tu au kula nyama choma kama unataka. Umekuwa mtu wa kutaka mafanikio yasiyo na changamoto yoyote. Ndo maana unasubiri ukiambiwa aisee biashara ya Matikiti inalipa hatari huyo umo. Ukiambiwa mayai ya kware yanalipa huyo. Hutaki kutulia kwanza ujifunze.

Hakuna biashara isiyolipa. Ila kuna akili zisizo za kibiashara ambazo lazima kuzibadili zijue biashara faida na hasara ni kawaida kabisa. Wanasema SOMETIMES YOU WIN AND SOMETIMES YOU LEARN.

Sasa wewe hutaki kulearn utafikaje kwenye mafanikio kibiashara?

Trump mwenyewe alifilisika kabisa. NIL. Zero. Rock bottom. Licha ya kuanza kwa mtaji mkubwa. Kama haupo tayari kukosekana pesa basi kazinunulie nguo mpya sikukuu zikifika uvae.

Na hiyo ndo maana kuna matajiri wachache. Wenye moyo wa UTHUBUTU katika jamii huwa ni wachache tu.

If you're afraid to lose money NEVER INVEST. Baki na hela zako.
Sounds good.. Tumepata somo aroo
 
Wengi wa waandishi wa hizi porojo za namna hii huwa hawafanyi biashara ya aina yoyote, huwezi ukaingia kwenye biashara huku ukija mindset ya kupoteza hela kisa ndo ujasiliamali, biashara unaweza ingia kwa kutiria maanani risk:reward ratio vinginevyo utakuwa unapoteza hela huku ukijipa matumaini feki. Na una uhakika gani kama mengi magazeti yalikuwa yanampa hasara.
 
seriously moderator aliebadilisha title ya huu uzi kakosea big time.

title mwanzo ilikua " kama unaogopa hasara basi usiwekeze"

mod mwenye akili nyingi akaona title haijakaa sawa kisha kai edit iwe
"kama unaogopa hasara baki na hela zako" ..seriously??

original title ilikua ina reflect content ya thread zaidi kuliko hii edited title ambayo imekaa kiudaku zaidi.

dah haya bhana nisje kupigwa ban bure, ngoja nikae kimya
 
Kuna mwandishi wa kitabu kiitwacho RICH DAD POOR DAD, aliwahi kuandika title ya kitabu kingine alicho ongelea CASHFLOW QUADRANTS. Ukisoma ndani inaonesha kuwa kila mtu huwa anachagua kukaa kwenye quadrant yake kutokana na kuchagua RISK au kukwepa RISK.

Quadrant ya kwanza anaongelea EMPLOYEES, yaani waajiriwa. Kundi hili la watu hawataki RISK kabisa. Ukikutana nao mshahara ni kila kitu kwao, hawashauriki kuhusu kufanya biashara, kumiliki biashara au kuwekeza. Nadhani uzi unawahusu zaidi. Lakini kwa dunia ya leo ukitegemea tu kuajiriwa hakika hauwezi kuwa tajiri na generation yako lazima ipambane.

Quadrant ya pili inaongelea SELF EMPLOYED, hawa ni watu wa kujiajiri, watu hawa huchagua kuangalia fursa kwenye jamii na kuzivalia njuga. Hawa ni kama mama lishe, wauza matunda, wauza maua n.k , Hawa huanzisha biashara zao na kuzisimamia wenyewe 24/7, Hawa wamechagua RISK ndogo. Na mapato yao huwa size ya kati. Mara nyingi hufanikiwa na kuwa na maisha ya kawaida sana.

Quadrant ya tatu ni BUSINESS OWNERS hawa ni watu wanao miliki biashara. Wao huangalia fursa kwenye jamii na kuzifanyia kazi kwa kuajiri rasilimali watu. Mfano wamiliki wa hotel, restaurant, guest house, bar, mabasi ya mikoa, dala dala. Hawa wanachukua risk kubwa na huwekeza pesa nyingi na hawaogopi kufilisika, japo hufanya risk management ili kujua ni biashara gani aimiliki na ni kwa wakati gani muafaka.

Quadrant ya nne ni INVESTORS, hawa ni wawekezaji kama ulikuwa unawasikia, hununua shares kwenye makampuni makubwa. Hununua majengo na kuuza, Huwekeza kwenye mabenki, huingia ubia na serikali au taasisi n.k Mara nyingi hawa hutokea Quadrant ya pili au ya tatu. Ki ufupi wanajua nini maana ya biashara na mara nyingi ni professionals wa biashara au wameajiri watu ambao ni professionals. Hawaogopi risk hata kidogo.

Kwa hiyo nakubaliana na moderator. Ila arudishe heading ya kwanza kama unaogopa risk usi wekeze. Kimbilia kwenye Quadrant ya kwanza.
 
Hiii ya lendrmak hotel kuwa hostel ndo imeniacha hoi kabsa
Mkuu kama una mentality ya kijasirimali huwezi kushangaa landmark kuwa hostel. Mi kwanza kabisa nikipata nafasi ya kumuona huyo mmiliki ya hiyo hotel nampongeza. Kama huna wateja wa kutosha kwa nini ung'ang'anie hotel wakati kila mwezi unaishia kula hasara ya kutosha! Kumbuka hotel ina gharama kubwa za uendeshaji kuwalipa wahudumu na gharama nyingine nyingi!.

Lakini pia tukumbuke kuwa ile bado ni hotel kwa maana ya jengo na investment nyingine kwenye hilo jengo! Siku biashara ikirudi kwenye mstari wake kama kawaida anaendelea kama kawaida! Issue hapa hiyo hostel kawapangisha akina nani na wanamlipa kiasi gani kwa siku/mwezi.

HUYO NI MFANYABIASHARA WA SIKU NYINGI ANAJUA ANACHOKIFANYA!
 
Mbona umepost kwa hasira mkuu .... Umeliwa? any way investment is not Gambling. Tujifunze kupitia kufeli na kwa walio faulu ili tusonge!!
 
We fanya biashara zako kimya kimya kama umefilisika huko usije kutoa ovu hapa.
Unachotaka wewe ni wenzio mafilisike kama wewe ulivyofilisika ndipo upate faraja ya moyo sasa huo upuuzi peleka kwenu acha watu wawekeze... ndugu unavyotaka wewe sio lazima kuna watu wamefanya biashara hata kama waliyumba lakini hawakufikisika.
Principle yako sio universal so usiforce ufananae na waliofaulu kibiashara.
Mind your business umeandika kwa ukali mno kama una shari bwana.

Hiki kitu ndicho nilichokisemea jana kwamba baadhi ya watanzania ni nuksi kwani wana wivu sana wa kimaendeleo... can't imagine unataka mwenzio afilisike ili iweje sasa kwanini usimuombee atajirike ili aje kukunyanyua mkono?

Shame upon you ndugu we ni ya sample ya kwanza ambayo nimeipata humu toka nitoe bandiko langu jana
 
Mbona umepost kwa hasira mkuu .... Umeliwa? any way investment is not Gambling. Tujifunze kupitia kufeli na kwa walio faulu ili tusonge!!
Ni kitu hata mimi nilichoki observe mkuu huyu mtu kaliwa sio bure...
 
Sikia.... BAKI NA HELA ZAKO

Mzee Mengi alikuwa na gazeti linaitwa ALASIRI. Halikuleta faida. Lete Raha vile vile. Ushindani wa magazeti mengine ulikuwa mkali. Wasomaji wakabadilika. Internet zikaingia nk.

Akaachana nayo. Afu wewe eti unataka ufundishwe biashara ambayo hutaki kupoteza hela. Kaa na hela zako tu kwa kweli.

Hivi unadhani Novida imeenda wapi. Kama Coca Cola wanakosa soko la bidhaa yao wewe je?

Okay, tufanye hivi, ule ukumbi wa Sinema Mwenge ITV ulikufa kifo cha fasta. Competition.

Kuna matajiri wengi tu walipoteza sana pesa. Mabasi ya Scandinavia yapo tena? Juzi tu Landmark Hotel ikawa Hostel.

Dar Village hapo Rose Garden Kijitonyama haijajengwa hadi leo. Mradi wa mabilioni uliingia mdudu miaka zaidi ya 8 sasa. Wewe unataka utakachoanza nacho kisife. Hela zako hutaki zipotee. Aisee you're not an entrepreneur. Kaa tu na hela zako. Ndo maana unasubiri ukiambiwa aisee biashara ya Matikiti inalipa hatari huyo umo.

Hakuna biashara isiyolipa. Ila kuna akili zisizo za kibiashara ambazo lazima kuzibadili zijue biashara faida na hasara ni kawaida kabisa. Wanasema SOMETIMES YOU WIN AND SOMETIMES YOU LEARN.

Sasa wewe hutaki kulearn utafikaje kwenye mafanikio kibiashara?

Trump mwenyewe alifilisika kabisa. NIL. Zero. Rock bottom. Licha ya kuanza kwa mtaji mkubwa.

If you're afraid to lose money NEVER INVEST. Baki na hela zako.
Mbina hujaandika watu au makampuni ambayo hayajawahi filisika sokoni?
Peleka uchafu wako huko kila.za ww
 
Mod naombeni mtoe huu uzi sticky kwani unapotosha au ufutwe unasambaza chuki za kibiashara.
 
Labda uwe na mahela Mengi aisee...hivi hivi siwezi ku gamble na hiki kidogo nilicho nacho...it’s too risky
 
Back
Top Bottom