Setfree
JF-Expert Member
- Dec 25, 2024
- 6,238
- 8,194
Shetani na mapepo ni viumbe wasioonekana kwa macho. Hao ndio wanaosababisha vitisho, hofu, nywele kusisimka, unasikia maneno au sauti bila kuona mtu anayeongea, kukandamizwa kifua, kunyolewa nywele, kujikuta umelala nje ya nyumba na kitanda chako nk nk.
Ukilala katika nyumba zenye uchawi au ushirikina na kushuhudia mambo kama hayo, dawa sio kukimbia au kuhamia nyumba nyingine. "Dawa" hii hapa: Kabla hujalala tamka maneno haya: "Kwa Jina la Yesu Kristo, nakuamuru shetani na mapepo yako, mtoke katika nyumba hii. Nakanyaga nguvu zote za giza. Wachawi hamuwezi kunidhuru, kwa Jina la Yesu Kristo, amen."
Fanya hivyo kisha omba Mungu akulinde, utalala shwari, shwari kabisa, siku zote.
Ila shetani anawajua wenye mamlaka ya kumkemea. Wenye mamlaka hayo ni wale tu waliookoka na wanaoishi maisha matakatifu. Kama hujaokoka, na unaishi dhambini, ukimkemea shetani au mchawi, haondoki. Sana sana atakurarua!
Huu hapa uthibitisho wa "dawa" ya kufukuza uchawi:
Luka 10:19
"Tazama nimewapa mamlaka ya kukanyaga nyoka na nge na juu ya nguvu zote za adui; wala hakuna kitu chochote kitakachowadhuru."