Kama unatafuta Ajira kwa kusambaza CV Ofisi za Umma na hujui nafasi ya Mlinzi hupati kazi ndugu yangu

Kama unatafuta Ajira kwa kusambaza CV Ofisi za Umma na hujui nafasi ya Mlinzi hupati kazi ndugu yangu

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
Habari!

Katika kuhudumia watu (wateja) kama mlinzi ndani ya miaka 6 napenda kuteta na vijana mnaosaka ajira. Ratio ya ajira na wasomi sasa imekuwa tofauti sana.

Sasa kinachomata ni connection na akili. Kuna ofisi watu wana hela mpaka huna wa kumuhonga. Imagine mpaka Mimi mlinzi unanikuta nimetupia suti na pembeni kuna Suzuki yangu.

Hapa ukifika huna connection au huna akili bali una vyeti tu hupati kazi. Kijana anafika getini na bahasha yake anaomba kuonana na boss direct hataki kusikia maelezo.

Ukimuuliza unataka kuongea naye nini hebu niambie anaona unambania ridhiki. Kwa hekima ya kawaida tu namruhusu aende kwa PS. PS anamwambia shortly kuwa hakuna kazi anarudi mnyonge.

Walinzi tunajua sera za ofisi yote, tunamjua kila boss na tabia zake. Ofisi inabadilishwa maofisa kila mwaka ila sisi tupo.

Nimeleta Uzi baada ya brother mmoja leo kutorodhika na maelezo yangu na kuomba aonane na boss. Kajibiwa tu hakuna nafasi ya ajira iliyo wazi. Akarudi kwangu kuomba msaada maana alikumbuka maneno ya awali nikamwambia sina msaada Mimi ni mlinzi tu ondoka.
 
Wanajua wote ni lasaba B au form 4 ya kuunga vyeti vitatu
ilishatokea Coca cola hp mikocheni Yani kipande Cha karatasi ( Degree ) Cha mtu mmoja ( Gang leader )kiliponza watu wa nne wakakosa nafasi .... Kujishusha tu ambako hakumpunguzii mtu kitu vijana wakaleta jeuri wakidhani ma GPA yao yangewatisha watu.
Kumbe Kampuni inaanzia getini pale 😁......
 
Ilikuwaje huko?
 
Ilikuwaje huko?
Kaka dharau Yani mtu kupigiwa simu na HR kawaona walinzi km choo anawaambia na wenzie niskilize mm hawa walinzi tu kumbe walishapiga simu kumtaarifu na jamaa akawa anaskia sehemu ya mzozo.
 
Japo Mkuu, mimi naona hii inabidi pande zote muifanyie kazi.

Walinzi na wadada wa mapokezi ni aina ya binadamu wenye majibu ya hovyo kuliko hata mabosi wenyewe. Ndio maana wengine huona ni bora akafokewe na bosi kuliko na mlinzi.

Wakati niko mwaka wa mwisho Chuo nilianza kuzunguka maofisi kutafuta ajira, nilijifunza vingi sana. Mpaka nikahisi watu wenye nafasi za chini kwa sababu ya kuchukuliwa poa na wenye vyeo vikubwa kazini na wao wameamua wawafanye watafuta ajira ndio sehemu ya kumalizia hasira.

NB: Walinzi na wahudumu wa mapokezi wanaojitambua wapo, ila ni wachache sana.
 
nakubaliana na mleta mada nakumbuka mwaka fulani nilikuabkwenye harakati za kusambaza ma cv nikakutana na bean mmoja mlinzi yule alinifunua sana macho kwakua nilikuabmstaarabu sana kwake kwani nilipofika alinikalisha sana getini na baadae akanipiga kizinga sikua na hiyana nikampa akaenda nunua maji aliporudi akaniambia skia mdogo wngu makupa somo.
akatiririkaaa nikamuelewa vizur akaniruhisu niingie na mida huo boss alisharudi bas kulingana na maelezo yake nioifanikowa kuonana na wakuu w apale mambo yakaenda safi japobsikukaa sana nikaja kubahatika sehemu nyingine ila nilitumia mbinu zile zile. kila mtu ana nafasi yake
 
Ni matumaini yangu wote wazima. Mimi ni kijana wa kiume nimesoma diploma ya procurement and logistics management na bachelor degree ya business management, natafuta ajira nipo tayari kufanya kazi mkoa wowote
 
nakubaliana na mleta mada nakumbuka mwaka fulani nilikuabkwenye harakati za kusambaza ma cv nikakutana na bean mmoja mlinzi yule alinifunua sana macho kwakua nilikuabmstaarabu sana kwake kwani nilipofika alinikalisha sana getini na baadae akanipiga kizinga sikua na hiyana nikampa akaenda nunua maji aliporudi akaniambia skia mdogo wngu makupa somo.
akatiririkaaa nikamuelewa vizur akaniruhisu niingie na mida huo boss alisharudi bas kulingana na maelezo yake nioifanikowa kuonana na wakuu w apale mambo yakaenda safi japobsikukaa sana nikaja kubahatika sehemu nyingine ila nilitumia mbinu zile zile. kila mtu ana nafasi yake
Kumbe tusiichukulie poa
 
Back
Top Bottom