Kama unataka kufanikiwa kweye maisha, acha kufanya kazi za kimasikini zenye asili ya kimasikini.

Uvuvi unategemea ndugu kama unazo boti uvuvi ni deal sana
 
Mtu anaweza akawa polisi akajibana akapata mtaji akafanya biashara akapiga hela...traffic police wanapiga sana hela barabarani humo
Si washakalilishwa hao kua mwalimu hana hela, askari hana hela wenye hela ni wafanyabishara na wafanyakazi wa tra, ndicho kitu kipo akilini mwao.
Si ajabu hata yeye hana ila ndo ivo anajiona anazo kisa sio kada tajwa.
 
Mtoa maada kwa upande wangu kichwa cha habari ni sahihi, sema maelezo yake aliyotoa ndio sio sahihi.

Kwanza ajaweza kutofautisha kufanya kazi kwa kujiajili ama kwa kuajiliwa. Ukiongelea waalimu hao ni waajiliwa na boda boda ni kujiajili.

Sasa kutokana na maelezo yako unaposema kuna kazi za kimasikini ni sawa. Ila kwa upande wa kujiajili naomba niseme kwa Msisitizo HAKUNA KAZI YA KUJIAJILI AMBAYO NI YA KIMASIKINI. HAMNA ALIEJIAJILI UKASEMA ANAFANYA KAZI YA KIMASIKINI.

Mfano wew umetolea mfano wa Boda boda mpaka umenichekesha, kwamba boda ni kazi ya kimasikini? Je wajua boda anaingiza mshahara sawa na msomi wa darasan kabisa. Pengine akazidi kabisa? Usipagawe na nguo nzuri nzuri wanazovaa wasomi hamna kitu huko. Usirubunike na magari na nyumba za mikopo. Hamna kitu hapo.

Kwa upande wangu mim kazi za kimasikini ni za kuajiliwa ambazo hazihitaji elimu ya makaratasi, mfano kubeba zege, kazi za viwandani, n.k ila wauza matunda, boda boda, bajaji, karanga, wauza chips, mama ntilie n.k achana nao kabisa ni MATAJILI WA BAADAE HAO.
 
Mkuu uzi kama huu ukiutoa useme pia wewe ni nani na unamiliki biashara gani kwa tanzania na umeajiri watanzania wangapi, ili kuepusha kuchukua ushauri wa kitajiri kwa maskini kama sisi.
✅✅👏
 
Hatari sana
 
Mkuu uzi kama huu ukiutoa useme pia wewe ni nani na unamiliki biashara gani kwa tanzania na umeajiri watanzania wangapi, ili kuepusha kuchukua ushauri wa kitajiri kwa maskini kama sisi.
Yeye amesema ni mkurugenzi wa FAO
 
Hahaaa, Mungu akusamehe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…