Asante mkuu kwa somo zuri.
Nina kitu cha kuongezea hapo, ni rahisi sana kusema acha uvivu, acha kutumia pesa ovyo, anza kuweka akiba n.k
Ila ni ngumu kuacha uvivu au kutumia pesa ovyo kwa kuambiwa tu na mtu. Kuna haja sasa ya kuanzisha somo la ni jinsi gani mtu unaweza kuacha hizo tabia. Mbinu gani zitumike kuacha hizo tabia.
Kanuni kuu ya kuacha tabia fulani ni kuireplace hiyo tabia na tabia nyingine, let's say unataka kuacha tabia ya ulevi ni lazima uwe na tabia mbadala ya kucover nafasi ya ulevi.
Mfano ukiwa na hamu ya pombe, badala ya kunywa pombe ukifika bar anza tabia ya kuagiza juice kubwa zile na ukiweza kufanya hivyo mara kadhaa kwa mwezi ni mwanzo mzuri katika kubadili tabia usiyoitaka.
NB: Kubadili tabia sio jambo dogo hata kidogo.