realMamy
JF-Expert Member
- Apr 28, 2024
- 7,450
- 19,184
Kuchelewa ni adui mkubwa wa mafanikio na afya. Watu wengi wameponzwa na kusema "baadaye".
Nitaenda baadaye hospitali, baadaye nitaomba msaada, baadaye nitaomba, baadaye nitarekebisha mahusiano yangu.
Lakini "baadaye" nyingi huwa haziji.
Unapokutana na shida ndipo unakumbuka watu na fursa ulizopuuza, na ndipo msemo huu unatokea.
Kuna wengi wanapoona dalili mapema za ugonjwa kama uvimbe mdogo,homa, au maumivu huamua kuvumilia na kutochukua hatua yoyote ile.
Wanasema "itaisha yenyewe" au "nasubiri mshahara kwanza".
Anapofika hospitali akiwa mgonjwa sana, daktari anamwangalia na kusema "Kama ungewahi kuja ungepona. Sasa hali imekuwa vibaya".
Hapo ndipo watu wengi hupoteza maisha ambayo yangeokolewa kama wangekwenda mapema.
Pia msemo huu unatumika kwa watu wanaohitaji msaada lakini wanachelewa kuomba. Kuna fursa za kazi, masomo, au biashara zinapita mbele yako.
Unaona lakini unapuuza kwa aibu au uvivu. Siku ukikosa na kwenda kuomba msaada ndipo unaambiwa "Kama ungewahi kunambia wakati huo ningekusaidia. Sasa nimekwisha saidia wengine". Hapo ndipo unaona kuwa kuchelewa kunagharimu.
Usiogope kuomba msaada mapema na usidharau dalili ndogo.
Fursa, afya na muda havirudi nyuma. Kama una tatizo zungumza mapema. Kama unaumwa nenda hospitali mapema.