Pre GE2025 Kama Upinzani unataka mafaniko ya kweli 2025, Iachane na Urais, Ujikite Serikali za Mitaa, Ubunge na Udiwani, Urais labda 2030!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Ushauri wako ni wa kijinga , Tumeupuuza
 
Hapa nimekupata vizuri, unapodai CCM kama chama imeshazoea figisu, na japo Samia sio mtu wa figisu, lakini CCM kama chama kitamlazimisha afanye hizo figisu..

Sasa kwa msingi huo, unaposema Chadema haijajipanga na haijipangi, naona unamaanisha Chadema watafute njia nyingine ya kufanya nje ya huu mfumo wa kipuuzi wa uchaguzi uliopo sasa..
 
Tangu ulipoamua kuwa mwanachama wa ccm umekuwa ukitoa hoja zisizoeleweka sana
Sasa ndugu Mayalla kwa nini waliamua kuipiga marufuku mikutano ya vyama vya upinzani?Waliogopa nini?
Na kwa nini hawataki katiba mpya?Nadhani majibu unayo.
 
Mambo ya upinzani yanakuhusu nini wewe wakati unajua vyema kwamba ccm wamebaki kuiba kura kila uchaguzi unapofanyika sasa wamekwambia hiyo 2030 ndio hawataiba.
Mama anatosha sio? Nadhani mwanzozuri ni kuwa na wabunge wengi naadiwani wengi ili kuleta chamoto Bungeni namna ya kuiwajibisha serikali ilete maendeleo kwa wananchi.
 
Paskal nature can not be recreated or destroyed. Tume ya uchaguzi kwa uumbaji ni huru- haiwezi kuwa shirikishi na tukabaki salama. Tuache kuwachekea hawa wanasiasa (winner take all VS bad loser) waliopoteza chembe ya kuaminiana kati yao. Paskali hebu fikiria TFF iwape Yanga na Simba watafute waamuzi wa mechi yao- nakuapia hiyo mechi haitachezwa.
 
Nadhani anataka chadema iingie msituni
 
Hunaga jipya bro, vinginevyo ungeanzisha chama upate hiyo nafasi.
Mkuu Tindo , kwanza ni kweli sina jipya kwasababu in reality, there is nothing new under the sun!, hivyo jipya litoke wapi?. Nianzishe chama cha nini wakati Tanzania kwa chama kweli cha siasa ambacho ni chama as chama, tunacho kimoja tuu!, the one and only!, humu ndimo nilimo.
Ww ni motivational speaker fulani ambaye huna achievement yoyote unayoweza kuonyesha.
Mimi sio motivational speaker, mimi ni mwandishi tuu wa habari wa kujitegemea kwa kujitolea, ila ni kweli sina any achievement yoyote ya Kuonekanika ninayoweza kuonyesha, ila kalamu yangu ina ncha kali, baadhi ya maswali yangu, hoja zangu na maandishi yana waingia yawachoma na wana badilika ila watu hawaoni!, mimi ninayeandika na kushuhudia maandishi yangu yakileta mabadiliko chanya ni faraja tosha kwangu!. Kama utapata muda pitia hizi baadhi ya kauli umba zangu uone zilivyoleta matokeo chanya https://www.jamiiforums.com/threads...na-kauli-umba-ambazo-huumba-shuhudia.2013308/ ambayo japo hayaonekaniki kwa macho lakini matokeo yake yanaonekana.
Mtu mjinga tu ndio anaweza kufuata ushauri wako.
Ushauri wangu huwa ni ushauri wa bure, mama ni mtu mjinga tuu anayeweza kufuata ushauri wangu, hii inamaansha ushauri wangu ni wa kijinga!, then, angalia ushauri wangu hapa niliishauri nini CCM na Chadema https://www.jamiiforums.com/threads/ccm-imechokwa-chadema-haijajipanga.87532/ angalia nani alifuata ushauri wangu na akapata nini, na nani alipuuza na matokeo yake, sasa hapo nani mjinga?.
Ww ni mmoja ya waliowaingiza mkenge CDM wamchukue Lowassa, yule Mzee tapeli wa kisiasa.,
Hili la Lowassa naomba usinikumbushe litaniumiza kwasababu nili invest sana kwenye ushauri wa bure na matokeo nikuyakumbuka naumia mpaka kesho,
  1. Licha ya kumsupport Lowassa nilitoa angalizo hili https://www.jamiiforums.com/threads...e-rais-wetu-2015-rais-wetu-wa-2015-ni.800075/
  2. Mchakato wa CCM ulipoanza, nikapenyeshewa hii https://www.jamiiforums.com/threads/licha-ya-kukubalika-jina-la-lowassa-halitafika-hata-cc.827807/
  3. Na kweli Lowassa alichinjiwa baharini, baada ya kuchinjwa kwanza nilishauri https://www.jamiiforums.com/threads...ubali-matokeo-vunja-kambi-jisalimishe.883808/
  4. Kisha nikauliza https://www.jamiiforums.com/threads...-mwanzo-wa-safari-halisi-ya-matumaini.882751/ hivyo hapa ukisema niliwaingiza mkenge Chadema, hapa you would be right. I was very genuine when writing that ila it's very unfortunately Mungu aliisha panga.
  5. Baada ya uchaguzi nimewashauri https://www.jamiiforums.com/threads...tokeo-tushukuru-kwa-yote-life-goes-on.964000/
  6. Hivyo uamuzi wa Chadema kumchukua Lowassa was the best of the best kwa wakati huo Chadema had no one compared!. Hata 2025 Chadema has no one kushindana na mgombea wa CCM, hivyo rais wa 2025 ni mgombea wa CCM!.
Huu ushauri unaowapa wapinzani ungeutumia ww
Kuna baadhi ya ushauri mzuri nimewapa wapinzani, wakaufuata na ukawasaidia sana!.
Mfano
  1. Lissu ni mdogo wangu, nimemtangulia vidato pale Ilboru, ni mimi ndiye niliye mshauri Lissu agombee https://www.jamiiforums.com/threads...0-ameonyesha-uwezo-zaidi-ya-magufuli.1289828/ na labda hata zile pyu pyu ni ili kuzuia asigombee!.
  2. Akiwa ubelgiji Lissu aligoma kurudi bila kuhaikishiwa usalama wake na Siro, ni mimi tena niliye mshauri Lissu arudi https://www.jamiiforums.com/threads...aendelea-kukulinda-welcome-back-home.1712173/ lisu akapokea ushauri akakubali kurudi
  3. https://www.jamiiforums.com/threads...-njema-na-nchi-hii-mpeni-ushirikiano.1939827/ ushauri huu umefutwa wamewasilisha hoja mezani, wamesikilizwa sasa nao wanalamba asali!
  4. https://www.jamiiforums.com/threads...onde-msiandamane-mwenye-nguvu-mpishe.1088394/ Chadema walifuata ushauri huu na kuepusha shari
  5. https://www.jamiiforums.com/threads...nly-survival-do-or-die-msirudie-kosa.1813313/ Chadema imefuata ushauri huu
  6. https://www.jamiiforums.com/threads...ngukia-bali-angalia-pale-ulipojikwaa.1993155/ ushauri huu sasa unafatwa
  7. https://www.jamiiforums.com/threads...-19-ni-mashujaa-kuendelea-ubunge-wao.1815648/ Chadema wamekubali matokeo sasa wana survive
  8. https://www.jamiiforums.com/threads...tokeo-tushukuru-kwa-yote-life-goes-on.964000/ ushauri huu ulifuatwa
  9. https://www.jamiiforums.com/threads...-kuzira-je-si-tabia-za-kike-si-utoto.1011874/ ushauri huu unafuatwa sasa Chadema sio Chadema susa susa au Chadema zira zira, sasa ni Chadema kazi kazi huku kazi iendelee
  10. https://www.jamiiforums.com/threads/kuelekea-2015-chadema-kuchukua-nchi-kwa-kishindo-only-if.323057/ ilikuwa Chadema wachukue nchi, kwa kupuuza ushauri huu, Chadema inaendelea kupiga mark time!.
P
 
Kikubwa ni kujipanga ili hiyo 2030 wawe wako ktk position nzuri.
usiwakatishe tamaa na kumbuka wao wanajitambua vyema kabisa!
No siwakatishi tamaa bali nawaeleza ukweli. Mtu anayekueleza ukweli, anakusaidia sana, na kiukweli sio najisifu, bali ni kweli ninaisaida sana Chadema. Ukiwa na great expectations za kushinda, kumbe ni matumaini hewa, yule anayekuambia ukweli kuwa hayo ni matumaini hewa, hauwezi kushinda, huyu ndiye anakusaidia!, kukupunguzia impact ya matokeo!. Mfano hapa https://www.jamiiforums.com/threads...i-wenu-mkuu-sio-ccm-lazima-mbadilike.1356810/ https://www.jamiiforums.com/threads...wa-je-tunarejea-nchi-ya-chama-kimoja.1358762/
Matokeo ya ushauri huu ni hata baada ya Chadema kula mweleka uchaguzi wa 2020, walikubali matokeo kwa heshima na adabu bila vurugu yoyote.
P
 
Eti walikula Mweleka! Hiivi ninyi SUKUMA GANG huwa mnatumia nini kufikiri??Kilichotokea mwaka huo sitokuja kukisahau kualika Wanajeshi kutoka Rwanda na Burundi kusimamia usalama wa uchaguzi mkuu ilikuwa ni halali?Hayo mambo endeleeni kuyashabikia lakini vizazi vinatofautiana sana bahati nzuri au mbaya mnapeleka watoto wenu International Schools hawa watakuja kuwaumbua na kalamu zenu mtazitupa chini maana hawa hawana uvumilivu.
 

Nimecheka kwa nguvu, eti uliwahauri CDM kumchukua Lowassa. Unachofanya ww ni sawa na wafanyacho wanafunzi kwenye maswali ya multiple choice. Unakuta mtu hatujui jibu, ila ananyanyua kalamu juu na kushusha kwenye jibu, hapo kalamu itakapotua anafanya ndio jibu. Akipatia jibu anajifanya anajua.

Unachoongea ni kubashiri, ndio maana unaweka mabandiko mengi tofauti tofauti, ikitokea bandiko lako moja likashabihiana na litakalotokea, unasema uliwahi kusema! Huu uhuni upo pia kwenye ilani ya CCM, wameweka list ya mahitaji yote ya wananchi. Ikitokea wakatekeleza chochote katika hiyo list, wanasema wanatekeleza ilani yao.

Halafu kwa kukusaidia tu, ujue kuanzia leo, CCM sio chama cha siasa bali ni kikundi cha dola kilichojivika koti la chama cha siasa. Hivyo wakati unakisifia ili kikutoe kimaisha, usiwe mbali na ukweli huu.
 

Usijekuta unaona uchaguzi wa 2020 ulikuwa ni uchaguzi. Ule haukuwa uchaguzi, bali yalikuwa ni maenesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura. Uchaguzi uko Kenya boss. Kwahiyo ukiongelea uchaguzi ule inabidi uongee kwa kujificha. Na ukitaka kujua haukuwa uchaguzi, ingia kwenye tovuti ya tume ya uchaguzi uone kama kuna matokeo.
 
Mama anatosha sio? Nadhani mwanzozuri ni kuwa na wabunge wengi naadiwani wengi ili kuleta chamoto Bungeni namna ya kuiwajibisha serikali ilete maendeleo kwa wananchi.
Kutawaliwa na chama hicho hicho kwa zaidi ya nusu karne inaonyesha ni kiasi gani wananchi katika nchi hiyo walivyo mbumbumbu.

Na nafuu kama chama hicho kingekuwa kina chaguliwa kihalali na wananchi lakini sasa hawa wanajitangaza wenyewe kwamba wameshinda pasipo hata uchaguzi kufanyika. Bure kabisa.
 
Mkuu Geofre Maseta , kiukweli wewe ni mtu muhimu sana kwa Chadema, kwasababu unatumia kitu kinachoitwa "the power of positivism", ikitokea wewe ukawa ni powerful kweli, then 2025 Chadema wanatinga Ikulu yetu!.
Hapa sikuulizi hiyo nguvu kubwa ni nguvu gani na itatoka wapi, ili usitoe siri za mipango mkakati kwa adui, I just wish you all the best!.
2025 ccm wataingia na mazoea Yale yale kuwa ushindi ni lazima kumbe zilonga mbali na zitendwa mbali...2025 goli liko wazi kweli kweli.. tushindwe wenyewe tu
Kuna kosa nimeisha linote, hii ya kudhani 2025 goli liko wazi kwa sababu unadhani kipa ni demu, hivyo ukipiga mashuti makali, badala ya kubana, ataacha na atapanua na nyie kuingiza kiulaini!. 2025 you will be surprised!. Kipa wa 2025 sio demu!.
P
 
Very fact.
 
Pambaneni na sheria mbaya za vyombo vya habari.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…