Hii hapa chini;
KAMA UPO CHINI YA MIAKA 40 USITUMIE PESA KUYAPATA MAPENZI YA WANAWAKE
Anaandika, Robert Heriel
Andiko hili ni Kwa utambuzi vijana, kuwafanya wajiamini na kujielewa.
Wakati wanawake wakihamishana Kupenda wanaume wenye pesa na kuwabagua wanaume wachanga ambao wapo kwenye umri wa utafutaji, Taikon nipo kuhamasisha vijana wakiume wajitambue na wasijigeuze Watumwa Kwa mambo ya ajabu.
Kimsingi Taikon huwezi kulamba pesa yake kisa umpe mapenzi, hilo halipo na sijawahi kufanya hivyo. Na Nina sababu ya kufanya hivyo.
i. Taikon siwezi kununua dhambi.
Taikon anajua uzinzi ni dhambi. Yaani dhambi nipate na pesa nitoe😀😀 labda sio Mimi. Nitatumia mbinu zingine lakini kamwe siwezi nunua dhambi ya uzinzi.
ii. Taikon siwezi nunua magonjwa.
Siku hizi kuna magonjwa mengi, Fungus, UTI na magonjwa ya zinaa alafu ati nitoe pesa kabisa kisa na mkasa utamu WA dakika chache. Labda sio Mimi.
Mimi ukiniita Mbahili Hilo sioni shida na wala haliniumizi Akili.
Kitakachoniumiza akili ni kukupa pesa wakati nawe unanitaka, nawe ulienjoi, na hapohapo naweza ambulia magonjwa. Labda sio Mimi.
iii. Siwezi nunua Mikosi.
Hakuna kitu kinachotia mikosi Kama Kufanya uzinzi.
Ni Bora nipate mikosi burebure alafu hiyo pesa ambayo ningekupa niitumie kuondolewa hiyo mikosi.
Vijana jiaminini. Umri wa kutafuta pesa tafuteni pesa,
Msije mkajidanganya kuwa ninyi pekee ndio mnashida na hao wanawake hata wao wanashida na ninyi tena Sana. Sema wao wamefanikiwa kuwaaminisha kuwa wanaweza kuvumilia ilhali sivyo.
Tumieni mdomo wenu unatosha.
Wasiwatishie kuwa sijui pisikali utaziita Shemeji hakuna kitu kama hicho. Mbona wengine pesa hatutoi na pisikali tunachapa.
Nachojaribu kusema ni kuwa usiwe mtumwa kisa mapenzi, wanawake wasikuendeshe, na wala Usitafute pesa kuwafurahisha. Tafuta pesa Kwa ajili yako.
Hudumia Mkeo pekee tuu
Na Kama unataka kuhudumia wanawake WA nje basi hakikisha umefikisha umri wa kutumia hizo pesa na uwe nazo. Miaka 45 huko ndio unaweza kufanya hivyo.
Sasa kijana miaka 30 unateswa na Mapenzi.
Yaani bila pesa huyapati mapenzi,
Hapo ngozi yako bado inanuru, Sura bado angavu, kiharufu cha uzee bado hakijatoka, ukivaa nguo zinakukaa na bado unatoa pesa. Ukiwa mtu mzima utatoa nini kama sio kutojitambua?
Pesa Acha watoe Baba zako wenyevage ya 45+ huko.
Mwanamke akikuzingua Kama hakutaki piga chini. Kama unatongoza wanakukimbia endelea kutongoza hivyohivyo usichoke utapata tuu.
Na sio ujitese kutoa pesa kisa unaogopa kuachwa.
Wewe Mpe hela alafu Sisi wahuni tukija hatutoi hata kiingilio Kama Staff. Na akizingua tunapiga makofi na bado atatung'ang'ania.
Kijana Mdogo unakuwa Kama jingajinga bhana!
KAZI yenyewe unayofanya ya shurba bado uhangaishwe na wanawake. Ujinga tuu!
Wazazi hasa Sisi wababa tunapaswa kuwafundisha Vijana wetu kujitambua tangu wakianza kubalehe.
Unakuta kakijana kanalalamika ati kameliwa nauli😂😂 Yaani Kama jinga hivi! Unawezaje Kudate na mtu ambaye hata Nauli Hana? Au ndio akili kisoda.
Ishi kama Superstar. Hela hutoi na huduma muhimu unapata. Sio uishi Kama mtumwa huko ni kujidharau.
Usiwe na huruma za kijinga na watoto wakike. Shauri yako, mwanamke WA kumuonea huruma kidogo ni Mama yako, binti yako na Mkeo. Hawa wengine cheza Kama upo kwenye Filamu.
Vijana mjitambue.
Kama unashindwa Jambo dogo Kama hilo kumshawishi mwanamke akupe mapenzi yake bila kumpa pesa utaweza kweli mambo makubwa kwenye Familia yako😀.
Au ndio ninyi baadaye mkio mnalalamika lalamika ndoa zinawasumbua au wanawake hawaeleweki?
Kipimo cha kijana kujitambua ni kutotumia jasho lake kupata Mwanamke ambaye wengine wanampata bure. Huo ni ujinga!
Embu fikiria unaenda Coco beach sehemu ambayo hakuna kiingilio alafu wewe ulipishwe nawe ulipe wakati wenzako wanaingia bure, huo Kama sio ushamba ni nini?
Nyie wote ni Vijana, wote mnahitaji utamu iweje wewe ulipie.
Kwa watu wazima ni sawa kulipia Kwa sababu hakuna ulinganifu.
Yaani Mzee mtu mzima wa miaka 45+ atoke na binti wa 20+ lazima hapo pesa itoke.
Au jimama la miaka 40+ atoke na kijana wa miaka 30 hapo lazima jimama lilipie.
Ni aibu Kwa kijana wa kike kutoka na Mwanaume Mzee bure.
Na ni Dharau Kwa kijana kutoa pesa Kwa Msichana wanaolingana asiye mkewe.
Yaani huko ni kujidharau, kutojitambua na matumizi mabaya ya Mali, jasho, nguvu na akili. Ni kutojielewa.
Wakati unabisha unapaswa ujiulize, wakati wewe unalipia huduma hiyo Kwa wanawake kufanya zinaa na kujiweka katika hatari ya kupata UKIMWI mbona wengine wanapata Huduma hiyo bure? Alafu jitathmini.
Yaani pesa yako mwenyewe ikusumbue, ikupe UKIMWI,
Ikupe Fangasi, ikupe UTI.
Ikuletee matatizo. Bado ujione upo Sawa kichwani!
Ujinga tuu!
Alafu unamuomba Mungu akubariki upate pesa ili ukanunue dhambi😂😂
Hivi upo serious kweli wee!
Watu wa hivi sio ajabu ni ngumu kuwasaidia hata wazazi wao kisa ujingaujinga.
Biblia inasema usikubali Mtu awaye yeyote akadharau ujana wako.
Wala usikubali kujidharau.
Nasisitiza Kama umeamua kufanya dhambi, fanya Kwa akili basi, ni Bora ulipwe kufanya dhambi itaonekana ulilipwa kuliko ununue dhambi na magonjwa Kwa ujingaujinga usio na MAANA.
i. Vaa!
ii. Jipende na Pendeza!
iii. Jiamini!
iv. Jifunze kuongea Kwa ushawishi!
v. Jifunze saikolojia ya kujihusisha na wanawake( mind games)
vi. Jitegemee.
Uwe na uwezo wa kujilisha, kujivalisha na kuishi mahali pako mwenyewe.
Furahia maisha Kwa kufanya uyapendayo.
Ukijiepusha na Dharau, kujidharau na kudharauliwa.
Huwezi MPA pesa demu ambaye wengine tunapiga bure bhana! Embu jiongeze boya wewe!
Hutosifiwa popote pale nakuhakikishia.
Tunza mama Yako, Mkeo, na binti zako.
Ukifikisha 45+ ndio uanze kutunza wanawake wengine Kama utakuwa na hizo pesa.
Mwisho! Sikupangii maisha Kama utaamua kuwa Boya kuwa Boya.
Ni Yule Mtibeli
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Thanks Quote Reply
Report
Reactions:
kelvin01, Logbook, No retreat no surrender and 7 others
[IMG alt="Lumbi9"]https://www.jamiiforums.com/data/avatars/m/252/252927.jpg?1662746509[/IMG]
JF-Expert Member
Hahaha mzee wa kutoa mada kutokea kwenye comments
Thanks Quote Reply
Report
Reactions:
kp kipanya44 and dronedrake
[IMG alt="sadex"]https://www.jamiiforums.com/data/avatars/m/556/556453.jpg?1663062898[/IMG]
Member
Unaonekana mtaaalaam maaana umejifunza saikolojia ya kuandika uzi wa kuhamasisha .....
Thanks Quote Reply
Report
Reactions:
kp kipanya44
[IMG alt="Kanungila Karim"]https://www.jamiiforums.com/data/avatars/m/377/377471.jpg?1646661468[/IMG]
JF-Expert Member
Pata hela tujue tabia zako
Thanks Quote Reply
Report
Reactions:
kp kipanya44
[IMG alt="Championship"]https://www.jamiiforums.com/data/avatars/m/562/562446.jpg?1649285866[/IMG]
JF-Expert Member
Mapenzi ya kweli hayapatikani kwa fedha.
Thanks Quote Reply
Report
Reactions:
kp kipanya44
[IMG alt="jokotinda_Jr"]https://www.jamiiforums.com/data/avatars/m/664/664323.jpg?1657539246[/IMG]
JF-Expert Member
Aliye soma yote atupe summary plz 🙏
Thanks Quote Reply
Report
Reactions:
kp kipanya44 and dronedrake
[IMG alt="Bufa"]https://www.jamiiforums.com/data/avatars/m/75/75950.jpg?1659169461[/IMG]
JF-Expert Member
Tafuta hela mengine yote utazidishiwa. Pesa inaokoa nguvu na muda.
Thanks Quote Reply
Report
[IMG alt="ROBERT HERIEL"]https://www.jamiiforums.com/data/avatars/m/481/481793.jpg?1631734053[/IMG]
JF-Expert Member
Wengine hela hawana na tabia zao tunazijua
Thanks Quote Reply
Report
Reactions:
kp kipanya44, dronedrake and Kanungila Karim
[IMG alt="ROBERT HERIEL"]https://www.jamiiforums.com/data/avatars/m/481/481793.jpg?1631734053[/IMG]
JF-Expert Member
Huwezi pata pesa ukiwa na akili za kijinga
Thanks Quote Reply
Report
Reactions:
kp kipanya44
[IMG alt="ROBERT HERIEL"]https://www.jamiiforums.com/data/avatars/m/481/481793.jpg?1631734053[/IMG]
JF-Expert Member
Kichwa cha habari kinajitosheleza
Thanks Quote Reply
Report
Reactions:
kp kipanya44
[IMG alt="ROBERT HERIEL"]https://www.jamiiforums.com/data/avatars/m/481/481793.jpg?1631734053[/IMG]
JF-Expert Member
Shida Vijana wa siku hizi wanajidharau nachakuja namna lazima wadharaulike
Thanks Quote Reply
Report
[IMG alt="ROBERT HERIEL"]https://www.jamiiforums.com/data/avatars/m/481/481793.jpg?1631734053[/IMG]
JF-Expert Member
Hahaha
Thanks Quote Reply
Report
Reactions:
kp kipanya44 and Jana Ulirudi Usiku
[IMG alt="ROBERT HERIEL"]https://www.jamiiforums.com/data/avatars/m/481/481793.jpg?1631734053[/IMG]
JF-Expert Member
😀😀😀
Thanks Quote Reply
Report
Reactions:
kp kipanya44 and Jana Ulirudi Usiku
[IMG alt="pilato93"]https://www.jamiiforums.com/data/avatars/m/232/232814.jpg?1655539444[/IMG]
JF-Expert Member
Kuna watu wanavipaji vya kuandika
Thanks Quote Reply
Report
Reactions:
kp kipanya44, Jana Ulirudi Usiku, Tit 4 Tat and 1 other person
[IMG alt="Ulongupanjala"]https://www.jamiiforums.com/data/avatars/m/135/135472.jpg?1626097076[/IMG]
JF-Expert Member
Wengine wanasema kuchunwa pesa kwa mwanaume ni sunna!!
Vijana hongeni tu pesa zenu mkifika uzee hamna kitu mmebaki na pumbu tu,fanyeni saving na kuanzisha miradi mambo ya kuhonga na kumwagilia moyo yamerudisha nyuma vijana wengi sana.
Thanks Quote Reply
Report
Reactions:
Jana Ulirudi Usiku
[IMG alt="Maghayo"]https://www.jamiiforums.com/data/avatars/m/251/251293.jpg?1628171539[/IMG]
JF-Expert Member
Kijogoodi njoo huku wewe mbwiga
Thanks Quote Reply
Report
Reactions:
kp kipanya44
[IMG alt="ROBERT HERIEL"]https://www.jamiiforums.com/data/avatars/m/481/481793.jpg?1631734053[/IMG]
JF-Expert Member
Thanks Quote Reply
Report
Reactions:
kp kipanya44
[IMG alt="dronedrake"]https://www.jamiiforums.com/data/avatars/m/191/191330.jpg?1542273159[/IMG]
JF-Expert Member
hakuna uchi bila pesa X 3
labda unyetuke
Thanks Quote Reply
Report
Reactions:
kp kipanya44
[IMG alt="EINSTEIN112"]https://www.jamiiforums.com/data/avatars/m/515/515866.jpg?1656593949[/IMG]
JF-Expert Member
Tumeanza lini kupangiana matumizi😅😅😅
Thanks Quote Reply
Report
Reactions:
Cunch, ROBERT HERIEL and dronedrake
[IMG alt="ROBERT HERIEL"]https://www.jamiiforums.com/data/avatars/m/481/481793.jpg?1631734053[/IMG]
JF-Expert Member
Kwa mtu aliyeyajulia mapenzi ukubwani upo sahihi.
Thanks Quote Reply
Report
Reactions:
kp kipanya44, Jana Ulirudi Usiku and dronedrake
1 of 3
Next Last
BoldItalicMore options…
Insert linkInsert imageMore options…
UndoMore options…
Preview
Font sizeText colorFont familyListAlignment
- Align left
- Align center
- Align right
- Justify text
Paragraph formatStrike-throughUnderlineInline spoilerInline code
SmiliesQuoteInsert videoMediaInsert tableInsert horizontal lineSpoilerCodeSubscriptSuperscript
RedoToggle BB codeRemove formattingDrafts
Write your reply...
Post reply
Attach files
Similar Discussions
Share:
FacebookTwitterRedditWhatsAppEmailLink
10 Reactions
Reply
View attachment 2355534