EP MEDICS COSMETICS STORE
JF-Expert Member
- Oct 18, 2015
- 2,826
- 4,593
Wanasema ukiwa mtu wa kutembea na kila mwanamke unajiletea mabalaa/mikosi wakimaanisha unakaribisha umaskini kwenye maisha yako, mbona kuna watu nawafahamu ni wanabadilisha wanawake kila kukicha, miaka nenda rudi, ila bado kipesa wako vizuri, na navowafahamu pesa zao si za kishirikina.
Hio stereotype imetoka wapi
Kitu chochote kikisemwa sana jua kinaukweli, jambo lolote lina kanuni ya muda kuleta matokeo hivyo hao unaowajua wanafanya uzinzi na Bado wapo vizuri kiuchumi wape muda utapata majibu baada ya kuanza kushuka kiuchumi.
nakubaliana na wewe mkuu
Sex is overrated,zinaa sio nzur mbali na kupoteza fedha na muda…inavutia majanga pia kwenye maisha na kizazi chako…moja kat ya kaz kubwa tunapaswa kuifanya binadamu n kujizuia,kujitawala,kujithibiti na kujiweza….
Kufanikiwa au kutofanikiwa kwa mtu haina mahusiano yeyote na dhambi zake na sio uzinzi tuu, ni haina mahusiano na dhambi yeyote ile.Kuna muda,jipe muda kama siyo yeye hata kizazi chake hakitakuwa salama.
Dhambi au matendo mema ni kwa ajili ya kuonesha utii kwa Mungu, upendo kwa Mungu, binadamu na jirani na mwisho ni kwa ajili ya mbio za uzima wa milele pekee, HAKUNA CHA ZAIDI YA HAYO.
Mungu sio mjinga namna hiyo, hata kwa logic ya kawaida tuu, ingekuwa kufanikiwa kwa mtu kuna mahusiano na dhambi zake (mf uzinzi), basi binadamu tungekuwa wanafiki sana na tungempenda Mungu kinafiki tuu, yaani tungetii maagizo ya Mungu na kuacha dhambi ili tufanikiwe kwenye mambo yetu, NA SIO KWA SABABU YA UPENDO WA DHATI KWA MUNGU, kiifupi utii wa amri za Mungu ingekuwa ni kwa ajili ya kufukuzia mafanikio ya kidunia tu basi, kwani ni nani asiyetaka maisha mazuri ya mafanikio hapa duniani ?, hivuo formular ya hayo mafanikio ingekuwa ni kutofanya dhambi basi.
Binafsi nawakubali sana na kuwaamini matajiri wacha Mungu, wacha Mungu wa kweli walio-masikini ni wachache sana, wengi wao ucha Mungu wao ni kwa ajili ya mafanikio kwenye mambo fulani fulani ya kidunia sasa Mungu sio mjinga kiasi ichoo.