Kama uzuri wa sura, umbo, ngozi na mguu ndiyo vigezo vyako muhimu kwa kuoa basi umepotea sana

Ok mkuu nakubaliana na wewe asilimia 100%. Naomba nitangulize hofu ya Mungu kama kigezo cha kwanza , then IQ na vingine. Ila kuhusu uchawi ukichunguza zaidi kwa majirani na ndugu wa karibu wa binti wanaweza kukupa hint.
 
Ok mkuu nakubaliana na wewe asilimia 100%. Naomba nitangulize hofu ya Mungu kama kigezo cha kwanza , then IQ na vingine. Ila kuhusu uchawi ukichunguza zaidi kwa majirani na ndugu wa karibu wa binti wanaweza kukupa hint.
Mi nakushauri uokoke na uwe serious na wokovu.

Mi nimeona watu wamelazwa muhimbili na waliokuwa wanatoa msaada sana na kupeleka chakula na kumsaidia sana mgonjwa ni wachawi waliomloga. Wanamsindikiza afe haraka, sasa we fikiria kama kuna dokta mchawi humo pia inakuwaje. Wodi za wazazi ndio zaidi sasa.

Naona wewe bado umri mdogo changamoto za dunia hii huzijui.

Unadhani wachawi ni mafala hawana elimu.

Kwenye kundi hilo wapo pia wachungaji, ma injinia, wazungu,walimu wakurugenzi, wabunge na wafanya biashara n.k.

Uchawi ni " spirit" inayofanya kazi kupitia ndani ya mtu. Hivyo kupitia milango mitano ya fahamu ambayo ni " physical faculties" huwezi kumbaini mchawi. Wapo wachawi wadogo "wanga" ambao mara nyingi utasikia kadondoka sehemu fulani. Hao unaweza kubahatika kupata stori zao.

" Spirit" ya uchawi unaweza kuisambaratisha na " Holy Spirit" ambayo inatokana na Mungu. Sababu Mungu amekuumba wewe na huyo mchawi nguvu ya Mungu ni Super Power ambayo mchawi au majini hayafui dafu. Ndio maana walokole tunatamba sana. Ila mchawi ana uwezo wa kujua mlokole feki na genuine.
Mchawi pia ana uwezo wa kujua kuna kijana ana piga piga "chabo" anataka apate hint anataka kuoa ila anaogopa wachawi anapita pita hapa. Basi utakuta unasetiwa unaungia mzima mzima, kichwa na miguu.

Hii kwenda kwa waganga kupata kinga ni kujidanganya sababu kwa waganga nao ni ma witch, hakuna super kinga ambayo hio ukiwa nayo basi wachawi watakimbia, inakuwa ya muda tu ina expire.

Kinga ambayo ni 100% na hakuna ku expire ni Jesus.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…