Kama Vera Sidika kawa hivi, mpango ushafeli

Kama Vera Sidika kawa hivi, mpango ushafeli

Hii kitu inawezekana ni Photoshoot,Clout Chasing au Bwana ake anatoa wimbo maana Wasanii wanatabia za kuchocha sana[emoji2]

Na kama ni kweli basi nimpe pole na nimpongeze kwa kuwa mkweli..

Wamama/wadada tuna la kujifunza kwenye hili...
 
Inategemeana na Dr aliye kufanyia, kumpata Professional ni gharama na wenyewe wana standard zao za ujazo kwa kila kalio. Ila MDr wa Black Market wao hawana hizo standard,wana ongeza tu as long umewapa hela.

Umeona kina Kim kardashian wameamua kujipunguza na kutoa hizo butt kuwa wale tofauti maana kila mtu anafanya umeona sasa hivi walivyokonda
 
Huyo dada hata rangi alibadili, alikuwa mweusi tii kama kikaangio cha chips
 
Kuna documentary nilikuwa na itizama National Geographic, hizi surgery zikifanywa na madaktari wa kuungaunga ni too risks.

Ila dada zetu hawa sikii na hawambiwi.Kuna dada mmoja yeye nae anabonge la shape,ila lilikuwa limeanza kutengeneza rangi ya brown,yy aliandika mpaka kitabu cha hayo madhara na akawa ana watembelea wasichana wanaotaka kuongeza makalio na kuwasihi wasijaribu hiko kitu.

Mwengine nae alikuwa analipwa kwa zile appearance kwenye maclub nae likianza tako lilianza kubadilika rangi ,bahati nzuri wali muwahi wakaondoa matoxic yote kwenye makalio.


Nakumbuka miaka ya nyuma Maria Sarungi alikuwa na kipindi chake kinaitwa Changamoto, kuna mdada mmoja alimwalika kwenye kipindi chake nae anabonge la tako ,mpaka limekuwa kelo na anasikia maumivu kwenye mgongo.

Nasikia dada zangu siku hizi wanakimbilia Uturuki, sasa huko hao madaktari ni certified au ndio mafundi Maiko. Manake wasiwaige akina Kardashian wale wenzao wanaenda kwa maproffessional na hela wanayo.
Duh[emoji848]acha tuone watakavyokua yetu macho
 
Back
Top Bottom