Uchaguzi 2020 Kama Vyombo vya Habari vitaendelea kufanya hivi, CHADEMA Ikulu itakuwa ni ndoto

Kaka kama wanakuja tena kwa gharama zao tena kwa makubaliano chini ya kamati ya mawasiliano ya kitaifa anawapa dakika 15 waondoke, chombo gani kitacover mikutano na sera zako? Mchaw wa haya wanamjua . Umoja wa vyombo hvyo umeita chadema kuomba radhi lakini hadi leo bado hawajafanya hivyo. Kwa mazingira hayo hayo vyombo vingine Havana uhakika na usalama wa waandish wao na vyombo vyao huko chadema ndyo maana wanakwenda Kule wanakokuona kuko salama. Tena kumbuka maslahi ya kwanza ya vyombo vya habar ni usalama wa waandishi na vyombo vyao

Umejaribu kupima ni kwanini walifukuzwa na madai ya waliowafukuza kwako unadhani yalikuwa sahihi au walionewa? Maana hapa tunapaswa kuangazia pande zote mbili ili haki itendeke
 
Yaani bila hata kampeni mwananchi mwenye kujitambua unatakiwa ujue kuwa matatizo yote haya yaliyopo ni kwa sababu ya CCM

1. MAISHA DUNI
2. KILIMO SIO UTI WA MGONGO TENA
3. WAFANYAKAZI HOI
4. HIFADHI YA JAMII TAABANI
5. UHURU HAUPO TENA
6. ELIMU DUNI

Sasa unataka nani akuambie kuwa sasa mtoe CCM uweke kitu kipya. Hata ukiletewa media zote zikuonyeshe sera kama wewe mwenyewe hujielewi YATABAKI KUWA MAKELELE
Kaka ndege ilisha paaa hiii, kama hukupata ushindi 2015 wananchi this time wanaelewa wanachopaswa kufanya nini, wataznia sasa wemeonja harufu ya kuanza kutimia kwa ndoto za mwalimu huwaambii kitu tena kwa magu
 
Wakubwa kwa wadogo, itifaki imezingatiwa....

Nianze kwa kurudia kusema kuwa, mimi ni non aligned kwa maana ya kwamba "sifungamani na chama chochote cha kisiasa nchini. Hata kama sifungamani na upande wowote lakini bado katiba inaniruhusu kufanya yangu pale kwenye sanduku la kura mnamo tarehe 28 mwezi Oktoba 2020.

Ni takribani siku 11 sasa tangu kampeni za uchaguzi mkuu ziruhisiwe rasmi na Tume ya Uchaguzi Tanzania (NEC). Tathmini yangu kwa ufupi, naona mpambano mkali bado upo kama ule wa mwaka 2015 yaani ni vyama viwili vya CHADEMA na CCM ndivyo vinachuana vikali. ACT Wazalendo nao wapo kidogo japo sio kwa kiwango cha CCM na CHADEMA. Bado ni mapema sana kusema nani anaweza kutwaa mikoba ya nchi kwani siku za kampeni kuwashawishi wananchi zipo za kutosha. Baada ya hayo turudi kwenye mada kama heading inavyojitanabaisha.

Kama watu wengine, nami ni mazoea yangu kufuatilia matukio mbalimbali yanayojiri ndani na nje ya nchi kupitia vyombo vya habari hasa vya hapa nchini kwetu. Moja kati ya habari ambazo kwa sasa raia tunazifuatilia kwa ukaribu sana ni habari za uchaguzi mkuu wa bara na visiwani.

Hadi kufikia leo bado naona kasi ya kuoneshwa kwa matangazo ya mikutano ya upinzani kwenye vyombo vya habari vya nchi hii inazidi kupungua sana. Kwa Chama cha Mapinduzi kwao naona hali ipo vizuri maana vyombo vya habari vingi kila kukicha utaona ni wao tu japo vyama vingine pia vinahitaji kuuza sera zao kwa wananchi. Hii imenijengea maswali kadhaa ambayo majibu yake yanaweza kuwa wazi au yasiwe wazi.

Nimekuwa nikiwaza, labda media zinahitaji pesa kubwa ili kurusha matangazo hivyo kusababisha cost kubwa ambazo vyama vya upinzani vimeshindwa kumudu?

Nimekuwa nikiwaza, labda vyombo vya habari vinaona kampeni za CCM ndizo zina mvuto sana kwa watazamaji wao kuliko zile za upinzani?

Nimekwenda mbali zaidi nikawaza labda kuna shinikizo kutoka mamlaka fulani kuzuia kuonesha matangazo ya vyama vya upinzani?

Maswali yote hayo yamenijia baada kufuatilia tangu kampeni zianze na niliwaona TBC1 pekee ambao walirusha ufunguzi wa kampeni za CHADEMA japo kwa kukatakata matangazo. Leo nimefuatilia UTV, TBC1, Star Tv na Channel 10 wote wanarusha matangazo ya kampeni za mgombea wa CCM Dr. JPM akiwa Simiyu. Clouds wao hawana muda kabisa naona ni muziki tu labda bado wamejawa woga baada ya ban ya wiki moja.

Hii imenipa kitu kwenye fikra zangu na kuja na huu uzi kwenu CHADEMA kama mambo yataendelea kuwa hivi, hakika kushinda uchaguzi huu litakuwa ni jambo gumu sana kwenu. Nadiriki kusema hivi kwa sababu vyombo vya habari vina nguvu sana ya kueneza sera iwe mjini na vijijini. Kutembelea mikoa na wilaya pekee bado haitoshi kwa sababu zifuatazo;

i. Sio wakazi wa eneo husika wote hupata nafasi ya kuhudhuria mikutano ya kampeni.

ii. Mara nyingi mnatembelea sehemu za mijini tu na sio vijijini ambako ili sera zenu zienee vema yapaswa media ziwabebe.

iii. Media zinaheshimika sana kwa jamii yaani mtu anaamini sana kitu anachokisikia kwenye radio/TV kuliko source nyingine.

Kwa kusema hayo, naomba CHADEMA mtafute njia mbadala ili muweze kujinusuru na hili. Ogopa sana mtu anatembea kila mtaa akinadi sera zake huku wewe media zikikukaushia tu. Nasikia hadi matamko ya vyama vya waandishi wa habari vikiwataka muombe radhi, tafadhali fanyeni kila muwezalo habari zenu zipate airtime ila tofauti na hapo bado nafasi ya kushinda kwenu ni 20%.

Nafasi mliyobakiza ya kuwabeba kidogo ni huku online ambako nako sio wote wanaowapa support ipasavyo. Wapo wanaowaunga mkono wengi na wachache wanaowapinga lakini kumbuka kuwa idadi ya watumiaji wa hii mitandao ni ndogo sana kuliko wasiotumia.

Yangu ni hayo na ninawatakia kila la kheri, naomba kuwasilisha....
 
Unadhani hizo hatua watazichukua wapi na katika mazingira gani kama serikali ndiyo anaviminya?
Wakati ile sheria mbovu unaletwa walipaswa kupinga.

Vyombo vya habari vinavyolialia haviwezi kuwa sehemu ya ukombozi wa ukandamizaji wa jamii.

Jamii inahamasishwa na vyombo vya habari kama wanakerwa na haya yanayoendelea walipaswa watumie fursa ya uchaguzi kuungana na jamii kupinga ukandamizaji huu.

Kama wameamua kuwa kimya na kuungana na unyanyasaji huu then hawana maana hata ya kuendelea kuwepo.

Wananchi watajipigania wenyewe hata kama vyombo vya habari vimejaa wanafiki na waoga.
 
Kwa mujibu wao wanadai hao waliofukuzwa hawaweki content zote
TBC ni taasisi ya serikali, inawajibu wa kufuata sheria na kulinda maudhui. Sasa mtu anaongea mambo ambayo kwa usalama wa nchi ni hatari, unadhani wao watafanya nini?.
Lakini ni simple walipe matangazo itv , azam na startv.
 
Chadema haita pigiwa kura na vyombo vya habari bali itapigiwa kurs na Watanzania.
Hujaielewa hoja ya mtoa mada. Wapiga kura wale ambao hawana access ya u tube na mitandao mingine watawezaje kumsikia Lisssu au Sera za chadema bila kutumia vyombo vya habari vilivyo rahisi kusikika?
 
Wakubwa kwa wadogo, itifaki imezingatiwa

Nianze kwa kurudia kusema kuwa, mimi ni non aligned kwa maana ya kwamba "sifungamani na chama chochote cha kisiasa nchini. Hata kama sifungamani na upande wowote lakini bado katiba inaniruhusu kufanya yangu pale kwenye sanduku la kura mnamo tarehe 28 mwezi Oktoba 2020.

Ni takribani siku 11 sasa tangu kampeni za uchaguzi mkuu ziruhisiwe rasmi na Tume ya Uchaguzi Tanzania (NEC). Tathmini yangu kwa ufupi, naona mpambano mkali bado upo kama ule wa mwaka 2015 yaani ni vyama viwili vya CHADEMA na CCM ndivyo vinachuana vikali. ACT Wazalendo nao wapo kidogo japo sio kwa kiwango cha CCM na CHADEMA. Bado ni mapema sana kusema nani anaweza kutwaa mikoba ya nchi kwani siku za kampeni kuwashawishi wananchi zipo za kutosha. Baada ya hayo turudi kwenye mada kama heading inavyojitanabaisha.

Kama watu wengine, nami ni mazoea yangu kufuatilia matukio mbalimbali yanayojiri ndani na nje ya nchi kupitia vyombo vya habari hasa vya hapa nchini kwetu. Moja kati ya habari ambazo kwa sasa raia tunazifuatilia kwa ukaribu sana ni habari za uchaguzi mkuu wa bara na visiwani.

Hadi kufikia leo bado naona kasi ya kuoneshwa kwa matangazo ya mikutano ya upinzani kwenye vyombo vya habari vya nchi hii inazidi kupungua sana. Kwa Chama cha Mapinduzi kwao naona hali ipo vizuri maana vyombo vya habari vingi kila kukicha utaona ni wao tu japo vyama vingine pia vinahitaji kuuza sera zao kwa wananchi. Hii imenijengea maswali kadhaa ambayo majibu yake yanaweza kuwa wazi au yasiwe wazi.

Nimekuwa nikiwaza, labda media zinahitaji pesa kubwa ili kurusha matangazo hivyo kusababisha cost kubwa ambazo vyama vya upinzani vimeshindwa kumudu?

Nimekuwa nikiwaza, labda vyombo vya habari vinaona kampeni za CCM ndizo zina mvuto sana kwa watazamaji wao kuliko zile za upinzani?

Nimekwenda mbali zaidi nikawaza labda kuna shinikizo kutoka mamlaka fulani kuzuia kuonesha matangazo ya vyama vya upinzani?

Maswali yote hayo yamenijia baada kufuatilia tangu kampeni zianze na niliwaona TBC1 pekee ambao walirusha ufunguzi wa kampeni za CHADEMA japo kwa kukatakata matangazo. Leo nimefuatilia UTV, TBC1, Star Tv na Channel 10 wote wanarusha matangazo ya kampeni za mgombea wa CCM Dr. JPM akiwa Simiyu. Clouds wao hawana muda kabisa naona ni muziki tu labda bado wamejawa woga baada ya ban ya wiki moja.

Hii imenipa kitu kwenye fikra zangu na kuja na huu uzi kwenu CHADEMA kama mambo yataendelea kuwa hivi, hakika kushinda uchaguzi huu litakuwa ni jambo gumu sana kwenu. Nadiriki kusema hivi kwa sababu vyombo vya habari vina nguvu sana ya kueneza sera iwe mjini na vijijini. Kutembelea mikoa na wilaya pekee bado haitoshi kwa sababu zifuatazo;

i. Sio wakazi wa eneo husika wote hupata nafasi ya kuhudhuria mikutano ya kampeni.
ii. Mara nyingi mnatembelea sehemu za mijini tu na sio vijijini ambako ili sera zenu zienee vema yapaswa media ziwabebe.
iii. Media zinaheshimika sana kwa jamii yaani mtu anaamini sana kitu anachokisikia kwenye radio/TV kuliko source nyingine.

Kwa kusema hayo, naomba CHADEMA mtafute njia mbadala ili muweze kujinusuru na hili. Ogopa sana mtu anatembea kila mtaa akinadi sera zake huku wewe media zikikukaushia tu. Nasikia hadi matamko ya vyama vya waandishi wa habari vikiwataka muombe radhi, tafadhali fanyeni kila muwezalo habari zenu zipate airtime ila tofauti na hapo bado nafasi ya kushinda kwenu ni 20%.

Nafasi mliyobakiza ya kuwabeba kidogo ni huku online ambako nako sio wote wanaowapa support ipasavyo. Wapo wanaowaunga mkono wengi na wachache wanaowapinga lakini kumbuka kuwa idadi ya watumiaji wa hii mitandao ni ndogo sana kuliko wasiotumia.

Yangu ni hayo na ninawatakia kila la kheri, naomba kuwasilisha.
Lisu ni mpango wa Mungu ili kusudi lake litimie
 
Watapataje kusikia sera za wagombea wao kama wanapigwa pin?
kura ipo moyoni, nani kakwambia kura zipo kwenye TV?
kuna walioumizwa na uongozi mbovu wa wajumbe, mwenyekiti wa kijiji Diwani au hata kutomuona Mbunge. kuchoka na mtindo mmoja wa utawala, kumkomesha fulani na mashabiki wake
Hao wanaoshinda kwenye TV ndio wale wasio na vichinjio, ukiwawekea Man U na Liverpool jioni uwamalizie Barca na Madrid hawapigi kura siku hiyo
wapo machinga na mangi hawaachi maduka yao eti Jumatano wakapige kura
kura na mgombea unaye moyoni mwako HABADILIKI
usiwe km bendera, leo uwe na utakaowapigia kura
 
TBC ni taasisi ya serikali, inawajibu wa kufuata sheria na kulinda maudhui. Sasa mtu anaongea mambo ambayo kwa usalama wa nchi ni hatari, unadhani wao watafanya nini?.
Lakini ni simple walipe matangazo itv , azam na startv.

Unaweza kuwa ushauri mzuri
 
kura ipo moyoni, nani kakwambia kura zipo kwenye TV?
kuna walioumizwa na uongozi mbovu wa wajumbe, mwenyekiti wa kijiji Diwani au hata kutomuona Mbunge. kuchoka na mtindo mmoja wa utawala, kumkomesha fulani na mashabiki wake
Hao wanaoshinda kwenye TV ndio wale wasio na vichinjio, ukiwawekea Man U na Liverpool jioni uwamalizie Barca na Madrid hawapigi kura siku hiyo
wapo machinga na mangi hawaachi maduka yao eti Jumatano wakapige kura
kura na mgombea unaye moyoni mwako HABADILIKI
usiwe km bendera, leo uwe na utakaowapigia kura

Nimekuelewa vizuri.
 
Pamoja na support zote za media naona bado hao wasiopata coverage wanatikisa sana sasa hapo ndio panajengeka hofu kuu
Kuwabania chadema ndiyo kuwaongezea nguvu na umaarufu
Kupambana ni lazima
Hakuna dikteta ambae atakuletea USHINDI umewekwa kwenye kisahani, wakisindikizwa na matarumbeta. Tuendelee kusimama imara ili tuuchukue. Patakuwa na vitisho na majaribu mengi.
1599232166657.png
 
Back
Top Bottom