Kama Wabunge wote walioapishwa na Spika ni halali; Je, Kamati Kuu ya CHADEMA haina meno?

Kama Wabunge wote walioapishwa na Spika ni halali; Je, Kamati Kuu ya CHADEMA haina meno?

Idugunde

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2020
Posts
7,748
Reaction score
10,288
Mpaka sasa watanzania wengi tupo njia panda maana hatujui kama waliokuwa wanachama wa CHADEMA - 19 ambao walivuliwa uanachama na chama chao bado ni wabunge halali au la?

Jana gazeti la mwananchi limemnukuu spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akisema wabunge wote aliowaapisha ni Wabunge kamili na wakati wa vikao vya Bunge ukifika Wabunge hao wahudhurie vikao, maana Bunge litawapa haki sawa bila kujali uchache wao.

Binafsi kauli ya Spika Ndugai inaonyesha wazi kuwa bado anawatambua wanachama 19 wa CHADEMA ambao walifutwa uanachama wao. Na kwa mantiki hii ni wazi wanayo nafasi ya kuzama Bungeni, kuhudhulia vikao na kutimiza haki yao ya kuwakilisha Wanawake huko Bungeni.

Lakini pamoja na Spika kuwatambua hao akina mama 19, pamoja na Wabunge wa ACT Wazalendo aliowaapisha. Je, Kamati Kuu ya CHADEMA iliyowavua uanachama ni Kamati isiyo na mamlaka ya kuwavua Uanachama?

Je, pamoja na kuwavua Uanachama hawa akina Mama 19 bado ni Wabunge halali? Mbona Spika bado anawatambua? Kamati Kuu ya CHADEMA ni mbwa anaebweka lakini hawezi kug'ata? Maana soon akina Mama hawa wataingia mjengoni tena kwa mbwembwe na kupigiwa makofi kama ndio hivi kwa nini Kamati Kuu ya CHADEMA isingekaa kimya na kuacha hawa akina Mama waendelee. Maana ni aibu tupu kwa Kamati Kuu kutokuwa na mamlaka ya kumvua uanachama Mwanachama wa chama chake

Wanachama na wafuasi wa CHADEMA ni wakati wa kutambua kamati kuu ya CHADEMA huenda haina meno au kuna sehemu CHADEMA kama chama chenu kina makosa ndio maana uhalali wa hawa akina Mama Spika bado anautambua. Najua mnaumia lakini kuweni wapole, maumivu yenu yanamanufaa kwa Taifa letu.
 
Kama kusoma hujui, huwezi hata kuangalia picha? Mbona inajulikana kuwa kwa mujibu wa katika hawa si wabunge tena! Amesema msekwa. Kinacho tokea ni mwendelezo wa kuelezea kuwa nchi inaendeshwa kidikiteta. Na hili linatuvua nguo kama nchi, ni aibu.
Je, kama taratibu za kuwafukuza hazijafuatwa mpaka sasa?
 
Je kama taratibu za kuwafukuza hazijafuatwa mpaka sasa?
Natamani CHADEMA waonyeshe hadharani barua ya kuwafukuza uwanachama hao wabunge 19 waliyoipeleka kwa Spika na Tume ya Uchaguzi.

Kauli ya Mwenyekiti Mbowe kuwa milango ya kuomba radhi ipo wazi inawezekana maana yake ni kwamba Chama hakitapeleka barua kwenye vyombo husika mpaka kwanza ili kuona kama watakuja kuomba radhi. Wakishapeleka barua hakuna tena ku reverse maamuzi.
 
Natamani CHADEMA waonyeshe hadharani barua ya kuwafukuza uwanachama hao wabunge 19 waliyoipeleka kwa Spika na Tume ya Uchaguzi. Kauli ya Mwenyekiti Mbowe kua milango ya kuomba radhi ipo wazi inawezekana maana yake ni kwamba Chama hakitapeleka barua kwenye vyombo husika mpaka kwanza ili kuona kama watakuja kuomba radhi. Wakishapeleka barua hakuna tena ku reverse maamuzi
Kauli ya spika mpaka sasa ni wabunge halali. Jambo ambalo linaloonyesha hawajafukuzwa kihalali au taratibu hazijafuatwa.
 
CHADEMA wanajua tabia ya wafuasi wao kuwa hawatumii akili sawasawa.

Spika aliwaambia kama wana nia ya kuwatoa hao wabunge basi waende mahakamani ili mahakama itengue, la pili wapitie tume, lakini pia walitakiwa kuandikia bunge barua ya kuwafukuza ubunge, ila wamekaa kimya na kuanza kupokea ruzuku.

Sasa mashabiki watabaki wanatangatanga wasione mlango wa kuingia kama vipofu.

Huyo ndo master Mbowe bhana.
 
Hamna kamati pale.

Hawana nguvu ta kubishana na serikali. Na sasa hivi Dunia nzima wanampongeza jpm kwa ushindi halali, sasa sijui watashitaki kwa nani😂😂😂😂😂 labda wakashtaki India😂😂
 
Sipika aliwaambia kama wana nia ya kuwatoa hao wabunge basi waende mahakamani ili mahakama itengue
CCM walipomvua Sophia Simba uanachama walifungua kesi mahakamani ili kumvua ubunge?
 
Chadema wanajua tabia ya wafuasi wao kuwa hawatumii akiri sawasawa,
Sipika aliwaambia kama wana nia ya kuwatoa hao wabunge basi waende mahakamani ili mahakama itengue, la pili wapitie tume, lakini pia walitakiwa kuandikia bunge barua ya kuwafukuza ubunge, ila wamekaa kimya na kuanza kupokea ruzuku.
Sasa mashabiki watabaki wanatangatanga wasione mlango wa kuingia kama vipofu.
Huyo ndo master mbowe bhana.
CHADEMA kama chama, mahakamani waende kufanya nini wakati wamefanya maamuzi kikatiba ya kuwavua uanachama? Hapo COVID-19 ndio waende mahakamani kupinga kuvuliwa uanachama.
 
Hapo ndipo umuhimu wa mahakama unaonekana.

Mahakama huru ingeulizwa hili ingetoa hukumu na maelekezo juu ya kadhia hii.

Bunge na serikali wametekeleza sheria, sasa Ni nafasi ya mahakama kutafsiri sheria na kujibu swali, je, CHADEMA, Bunge na Serikali, ni nani yupo sahihi? Je, Wabunge hao wana uhali? Kama hawana uhalali, basi mahakama itoe maelekezo na yatekelezwe. Kama Wabunge ni halali, basi iseme pia.

Walioweka mihimili mitatu Bunge, Serikali na Mahakama/Judiciary walikuwa na maana yao.
 
Katiba Katiba Katiba, wabunge hao 19 kwa mujibu wa katiba siyo wabunge tena mara baada ya kukosa sifa ya kuwa wanachama wa cdm.

Hayo mengine ni mbwembwe na kujiona kuwa wao wapo juu ya sheria zinazo liongoza taifa la Tanzania na dunia inajua hivyo
 
Hazira kama hizi ndio zinawapatia maumivu.

Hapo kisicho na meno ni katiba. CHADEMA wameshawafukuza kwa upande wao wamemaliza. Ni juu ya wengine kuangalia katiba inasema nini ambalo sio jukumu la CHADEMA. Post hii umeamua kuileta na Id hii, ile mpya iko likizo?
 
Hapo kisicho na meno ni katiba. CHADEMA wameshawafukuza kwa upande wao wamemaliza. Ni juu ya wengine kuangalia katiba inasema nini ambalo sio jukumu la CHADEMA. Post hii umeamua kuileta na Id hii, ile mpya iko likizo?
Sio kweli bosi, katiba ni sheria mama.
 
Ukitaka kujua CHADEMA ni wasanii, ruzuku yao ya November wameshachukua, nyumbu endeleeni kupiga mayowe tu, ndio maana Ndugai anapata nguvu sana.
Kama kweli hawa jamaa hawafai ni matapeli wa kisiasa.
 
Back
Top Bottom