Mpaka sasa watanzania wengi tupo njia panda maana hatujui kama waliokuwa wanachama wa CHADEMA 19 ambao walivuliwa uanachama na chama chao bado ni wabunge halali au la?
Jana gazeti la mwananchi limemnukuu spika wa bunge la JMT akisema wabunge wote aliowaapisha ni wabunge kamili na wakati wa vikao vya bunge ukifika wabunge hao wahudhurie vikao,maana bunge litawapa haki sawa bila kujali uchache wao.
Binafsi kauli ya spika Ndugai inaonyesha wazi kuwa bado anawatambua wanachama 19 wa CHADEMA ambao walifutwa uanachama wao. Na kwa mantiki hii ni wazi wanayo nafasi ya kuzama bungeni,kuhudhulia vikao,na kutimiza haki yao ya kuwakilisha wanawake huko bungeni.
Lakini pamoja na Spika kuwatambua hao akina mama 19, pamoja na wabunge wa ACT Wazalendo aliowaapisha je, kamati kuu ya Chadema iliyowavua uanachama ni kamati isiyo na mamlaka ya kuwavua uanachama?
Je, pamoja na kuwavua uanachama hawa akina mama 19 bado ni wabunge halali? Mbona Spika bado anawatambua? Kamati kuu ya Chadema ni mbwa anaebweka lakini hawezi kug'ata? Maana soon akina mama hawa wataingia mjengoni tena kwa mbwembwe na kupigiwa makofi,kama ndio hivi kwa nini kamati kuu ya Chadema isingekaa kimya na kuacha hawa akina mama waendelee! Maana ni aibu tupu kwa Kamati kuu kutokuwa na mamlaka ya kumvua uanachama mwanachama wa chama chake
Wanachama na wafuasi wa Chadema ni wakati wa kutambua kamati kuu ya CHADEMA huenda haina meno au kuna sehemu Chadema kama chama chenu kina makosa,ndio maana uhalali wa hawa akina mama Spika bado anautambua. Najua mnaumia lakini kuweni wapole, maumivu yenu yanamanufaa kwa taifa letu.