Kama Wakenya wameweza, sisi tunashindwa kwenda kujifunza kwao?

Kama Wakenya wameweza, sisi tunashindwa kwenda kujifunza kwao?

Equity na KCB Bank kitambo wanatoa Letter of Credit na collateral management. Mtu akiwa na mzigo wake umeandaliwa vizuri anaenda bank mzigo unakuwa Chini ya Collateral akitaka ku export anafanya process zote za export huku Bank ikihudumia ila mwisho wa siku original documents kama Bill of Lading, Packing List,Quality Certificate,Certificate of Origin,Export permit zinakabidhiwa Benki na wanawekeana condition au mkataba baada ya siku 60 ukilipa pesa documents zote utakabidhiwa na mzigo unakuwa umefika nchi husika na unauzwa.
"Somo" muhimu sana kulifuatilia🙏🙏🙏
 
Lugha ni kisingizio.
Mbona wachina wanasoma kwa kichina na wanaongea kwa kichina, ila wanazalisha bidhaa wanauza dunia nzima? Vipi kuhusu, Japan, Korea, Uturuki?



Lugha sio sababu
Duh..
Mkuu akilindogo,
Hata Nyerere alisema English ndo Kiswahili cha dunia.
Huko mitandaoni tunakutana na pop ups nyingi za wachina wakiuza bidhaa zao, na ni Kiingereza wanatumia tena kwa ufasaha.

Pili, usilinganishe Mandarin na Kiswahili, ile ni lugha kubwa inazungumzwa na watu zaidi ya 1 billion, wa nchi yenye uchumi mkubwa
 
Duh..
Mkuu akilindogo,
Hata Nyerere alisema English ndo Kiswahili cha dunia.
Huko mitandaoni tunakutana na pop ups nyingi za wachina wakiuza bidhaa zao, na ni Kiingereza wanatumia tena kwa ufasaha.

Pili, usilinganishe Mandarin na Kiswahili, ile ni lugha kubwa inazungumzwa na watu zaidi ya 1 billion, wa nchi yenye uchumi mkubwa
Okay
 
Inasemekana, kuna wakati Wakenya walikuwa wanakuja Tanzania, nafikiri Gairo, kununua viazi mviringo na kwenda kuvifsafisha, kuvigrade, na kuvifanyia packaging kisha kuvisafirisha kwenda sokoni Dubai.

Inasemekana, Wakenya hua wanavifuata vitunguu Tanzania, si kwa ajili ya kuviuza Kenya, bali nchi za nje hasa Dubai.

Inasemekana, hata Wachimbaji wadogo wa madini ya Tanzanite, kwa miaka ya nyuma, walikuwa wanapendelea zaidi kuuza madini yao Kenya kuliko nchini. Inaonekana kulikuwa na cha ziada walichokuwa wanakipata huko, vinginevyo, wasingejihatarisha kiasi hicho kutorosha madini mpaka Kenya.

Inasemekana, miaka ya nyuma , Kenya ilikuwa ikisafirisha Tanzanite nyingi zaidi kuliko Tanzania, nchi pekee duniani Tanzanite inakopatikana.

Inasemekana, miaka ya nyuma, Wakenya walikuwa wakifuata parachichi nchini Tanzania. Kipindi hicho, parachichi zilikuwa na bei nzuri, lakini walipoacha kufanya hivyo, wakulima wa Tanzania wakaambulia maumivu. Na hayo maparachichi, Wakenya walikuwa wakienda kuyasafirisha kwenda "ng'ambo".

Inavyoonekana, Wakenya wako vizuri zaidi kwenye biashara za "Kimataifa" kuwazidi Watanzania.

Wakenya ni "ndugu" zetu, kama wao wameweza, kwa nini sisi tushindwe?

Haitakuwa jambo jema endapo tutaamua kwenda kujifunza kwao?

Binafsi ninafikiria nimtafute Mkenya aliye vizuri kwenye hilo eneo ili nimfanye "mentor" wangu.

Tanzania tuna fursa nyingi sana. Tunachohitaji ni IDEA EXPLOSION!
Tanzania ni nchi ya ajabu sana nipo huku ujerumani nakutana na watanzania wenzangu na wakenya lakini watanzania wenzangu wananiangusha sana we acha tu. Yaani mtanzania ananuka shida lakini bado anaishi kama mtoto wa billgate.
 
Ikitokea Kenya wakaacha kununua machungwa Tanzania,yataozea shambani .
 
Back
Top Bottom