Kama Wakenya wameweza, sisi tunashindwa kwenda kujifunza kwao?

Acha utani mkuu[emoji3]
Wametuzidi wakati hawawezi kula bila sisi?
Kenge wewe
 
Nakubaliana na wewe kwa baadhi ya hoja zako
Ila la kulia lia hapana
Kweli kila nchi ina tamaduni zake lakini kwenye biashara nafikiri wote tuanongea lugha moja kwani biashara zilianza zamani sana Kama Silk Road
Toka China mpaka India mpaka Africa wote lugha moja ya biashara
Leo tumepata mazao mengi kutoka nje ambayo yalikuwa sio asili yake Africa bali yameletwa na watu, na sisi pia ya kwetu iwe mbegu, wanyama na hata ndege wamepelekwa sana nje ya nchi

Hakuna anaekata tamaa mkuu bali ni lazima kuwe na sheria zinazoeleweka na pia ukihitaji kujua kitu ufikie sehemu haraka na kujua bila kuzungushwa kwa uroho wa baadhi

Mimi nina kazi yangu na pia ni mfanyabiashara nje ya nchi
Nina tamani sana kupata bidhaa toka nyumbani maana tunaelewana lugha na ni rahisi kujua vingi
Kuna wakati nilikuwa nahitaji Vanilla pods na nilikuwa na soko ingawa mpaka sasa ninalo ila sio kubwa
Nikatafuta wauzaji nikakosa grade I na bei wanapanga hovyo hivyo nikaamua kuingia kwenye mtandao Madagascar. Nilipata kampuni moja genuine nakuwasiliana nao na kununua bila mimi kwenda nikapokea mzigo wangu hapa nilipo hao ni wahindi Madagascar
Sio kupenda wazungu au wengine hapana wao wako straight ana biashara unajiridhisha unasoma profile ya kampuni na kujua kama ina sifa basi
Siku hizi unaweza fanya biashara ya moja kwa moja na hata bongo zipo ila tunataka uaminifu zaidi na waache tamaa
Ukitaka leo gemstones ukiuliza tu tayari unaambiwa yapo jichanganye sasa
Mkuu changamote bado nyingi ila tunajivuta sana

Yapo mapungufu mengi na tunakatishana tamaa
 
Mkuu umewahi kuagiza mizigo kwenye malori na ukafika salama kila wakati?
Unaagiza mzigo packaging kwanza umefungiwq yale maboksi waliopokelea wao mizigo wakayachana halafu unafungiwq na katani huku bidhaa zinafika bolt zimemwagika kwenye lorry
Yaliyonikuta huko ni mtihani labda hujaingia kwenye biashara
Sio tunawasifia wazungu hilo neno usilitumie sana kwani tunajua fika wako mbali
Kuhusu elimu sio kila kitu elimu kubwa bali kuna mambo mengi binadamu tunafanya
Kwanza tuwe wachapa kazi na kuaminiana maana uaminifu ni muhimu sana halafu ukweli pia
Sisi wengi ni waizi, uaminifu zero, uongo na ujanja kwenye biashara hata makazini ni kawaida
Sasa nikisema ukweli hapo utasema nisilie hovyo hapana mkuu
Pia uongozi unasema ni mgumu
Sawa lazima uwe mgumu kwa sababu anategemewa mmoja tu aongoze lakini cha muhimu tunachoshindwa ni kufuata Sheria kama zilivyotungwa
Namuona Waziri wa kilimo anamuhoji Afisa wa kilimo anaeishi mjini wakati kapangiwa kazi kijijini tangu 2012 yupo mjini anakula mshahara tu
Sasa mimi nisilalamike nimekuwa nani
 
Wakenya ni aggressive sana kwenye biashara, pia lugha na elimu yao bora inawapa ujasiri wa kuingia popote duniani.
 
Ishu ni Ujuzi, mtaji, connection ya hayo masoko na mifumo ya serikali ndio inakwamisha
HILI NDILO TATIZO LA SEREKALI YENYE WATUMISHI WENYE URASIMU MKALI NA RUSHWA, WATUMISHI WAKE HAWAKO KATIKA KUSAIDIA AU KUWEZESHA BALI WAPO KWA KUKWAMISHA ZAIDI. (Roho mbaya tu)
Wakati mwingine si vibaya kuwashawishi wakenya hao kufungua makampuni hayo hapa Tanzania, hii itasaidia kuwapa ujasiri watanzania wengi, kuyavuta hapa ni kimkakati tu.
 
Sahihi
 
Uoga na uchawi wa watz wenyewe,kwani wakenya wanategemea Serikali.
Mwenye Nia akwamishwi,mbona wapo wabongo kibao wanafanya export kupitia Serikali hii hii
 
Wabongo hawajawekeza sana kwenye exports industry zaidi wamewekeza kwenye import industry
 
Uoga na uchawi wa watz wenyewe,kwani wakenya wanategemea Serikali.
Mwenye Nia akwamishwi,mbona wapo wabongo kibao wanafanya export kupitia Serikali hii hii
Kwa aliyefanikiwa akiusema ukweli wake na njia alizopita mpaka kufanikisha utabaki mdomo wazi, kwa tanzania sio rahisi.
 
Umasikini ni faida kwa ccm
 
Hata Israel walishawahi kuja SUA kujifunza kilimo lakini sasa hivi Tanzania ndio tunaenda kwao kujifunza kilimo cha kisasa my country.
Chai hii! Walikuja lini SUA kujifunza kilimo cha kisasa? Acha uongo sema walikuja kutuelekeza namna ya kufundisha kilimo.
 
Waziri wa mipango na uwekezaji alikuwa mkufunzi wa elimu na saikolojia!
 

Tulipata soko la nanasi mpingo nje, ile nchi nanasi zake mbaya hazina ladhq vidogoo vya njano!! Tulipopeleka sample yetu walizipenda saana!! Shida ikaja kwenye vibali mara rushwa mara utaratibu tulishindwa sisi!! Ila wakenya wananunua wanabrand kwao wanapeleka kwa urahisi saana!!

Tanzania huwezi kutoa biashara kupeleka nje, we tafuta ujanja wako toka nje nunua matakataka lete Tanzania uuze....!! Simple!

Hii nchi tungeamua kuwa serious kidogo tu, hakuna kijana angekosa kazi!! Midege na mimeli ya biashara ingemwagika nchini hatari!!

Watu wanalima wanakosa soko, ukisema usafirishe nje shida! Aliyetulaani alishakufa
 
Kuna haja ya kuwa na kampuni ambayo italipia vibali vyote na kusimamia ubora wa bidhaa na kutafuta masoko ya nje. Commission % inakuwa source of revenue.
 
Hatuwezi, Tanzania ni kichwa cha mwendawazimu

Wakenya ni Wajanja, Wasomi na wana connections nje ya nchi yao

Pia Nchi yao ni rafiki na inawa favour wafanyabiashara ila Tanzania ni nchi ya hovyohovyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…