ndege JOHN
JF-Expert Member
- Aug 5, 2015
- 25,030
- 61,298
siku hizi kila ukiingia mtandaoni unakutana na maudhui yanayowagawa wanaume na wanawake. Huku wanaambiwa wasioe, kule wanaambiwa wasiolewe. Huku wanaume wanatajwa kuwa shida, kule wanawake wanatajwa kuwa shida.
Kila siku ni vita. Ukienda kwenye comments ni matusi na lawama tu. Wengine wanafundisha jinsi ya kuachana, jinsi ya kumkomoa mwenzi wako au kwanini usiamini upande wa pili. Maudhui ya kuunganisha watu yamekuwa machache kuliko ya kuwagombanisha.huku sio kutofautina mawazo huku ni kiwango cha uadui.
Cha kushangaza ni kwamba visa vya talaka vinaongezeka, watoto wanalelewa na mzazi mmoja wanaongezeka, na watu wengi wameanza kuogopa hata kuingia kwenye ndoa. Wengi wanaona kama mahusiano siku hizi yamekuwa uwanja wa vita badala ya sehemu ya kujenga familia.Wengine wanasema bora kubaki single maisha yote. Kila siku ni mashambulizi, lawama na kubezana.
Swali langu ni moja tu, nani anafaidika na hali hii? Kwa sababu inaonekana kama kila siku kuna mfumo unachochea moto zaidi. Au labda ni mitandao ya kijamii ambayo inapenda ugomvi kwa sababu ugomvi unaleta views na engagement nyingi?
Maana ukiangalia vizuri, wanaume na wanawake wameishi pamoja tangu zamani. Leo hii ghafla kila upande unaonekana kama adui wa upande mwingine.