Kama wanawake hawakupendi na huna hela jifunze kupiga Saxophone, utawakimbia

Kama wanawake hawakupendi na huna hela jifunze kupiga Saxophone, utawakimbia

mdukuzi

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2014
Posts
20,925
Reaction score
51,688
1729879120190.png

Hiki kidubwasha ni hatari sana,nuliwahi kuishi nchi fulani sitaitaja jina,sikuwa na kazi ya kufanya,nikajiunga bendi ya wajamaica tukipiga Jazz na Salsa kwenye mahoteli makubwa,mimi nilikuwa napiga hiki kidude,nilikuwa nagombaniwa na wanawaje mpaka nikapata mshangazi wa kizungu.

Baada ya kurudi nchini nilijiunga kwaya ya kanisani ile ya praise and worship.,nilifanya mageuzi makubwa ya kwaya,sehemu ya vinanda nilitoa nikarepkace na sauti ya saxophone,
1729887683757.png
1729887683757.png

Hizi saxophone ziko aina tatu Altor Tenor na Saprano..mimi hupendelea hizo mbili za mwanzo.nimesahau kuna bass pia

Msichanganye saxophone na tarumbeta,trumpet,ni vitu tofauti kabisa
Sasa wakati wa nyimbo za kuabudu huwa nakipuliza kwa misifa na unavyojua makanisa ya kilokole asilimia kubwa huwa ni wakina mama,...kuna siku nilikipuliza nikakuta kanisa zima wanalia kwa hisia kama wamefiwa,kucheki jirani yangu kuna dada vinyweleo vimemsimama.
Ni vile sina pepo la uzinzi ningemaliza kondoo wa bwana

Sema bei yake imechangamka,hakipungui laki saba.

Mimi nilizaliwa nilikikuta nyumbani,kule upareni janisa la kKKT zamani hakuna ibada bila kwaya ya matarumbeta,nadhani wajerumani wamisionari ndio waasisi wa tarumbeta makanisani.

Kama mpenzi wako amenuna au umemkasirisha mpigie taratiibu lazima akusamehe.

Wanawake wanapenda sana wanaume wenye talent hasa ya muziki,ila katika wasanii wote wapiga saxophone wanavutia sana wanawake
NB sifundishi wala siuzi saxophonenaomba mniekewe,kwa sasa niko babati nalima ngano

Watoto wa 2000 endeleeni kutafuta hela,Umri wenu bado mdogo na kizazi chenu hamjui kupiga ala za muziki,uzi huu ni kwa wazee wakiokata tamaa ya utafutaji na wako lonely
 
Nilivyoanza kusoma nilihisi kama hili ni tangazo, kuwa hapo baadae utasema unafundisha kupiga hiko kidude
Mpaka nmemaliza kusoma sjajua ulitaka kutupa nini nini ilikiwa lengo la hii post yako au tujifunze tupate mademu/wanawake?
Mwamba amekoroga koroga uziii mwisho akaja kujipata hapo kwenye kwaya ya kanisa plus hiyo saxophone yake.

Mimi nadhani wikiendi imeingia ndiyo maana jamaa amechanganya madawa
 
😆😆😅😅😅😅😅😅

Amaaa kweli, mambo ni mengi sana ila sio yote yanayokuhusu.

Yaani umekaa zako umetulia mtu anakuja kukuambia habari za masaxophone na wanawake kuvutia 🤯🤯🤯😄
Kwamba sipati mademu,sasa mbinu ya kivita ni kuwa mpigaji wa hilo parapanda 🎷 ndiyo nitawakula hadi niwakinai.

Wallahi Duniani maajabu hayaishi.
 
Back
Top Bottom