View attachment 3135186
Hiki kidubwasha ni hatari sana,nuliwahi kuishi nchi fulani sitaitaja jina,sikuwa na kazi ya kufanya,nikajiunga bendi ya wajamaica tukipiga Jazz na Salsa kwenye mahoteli makubwa,mimi nilikuwa napiga hiki kidude,nilikuwa nagombaniwa na wanawaje mpaka nikapata mshangazi wa kizungu.
Baada ya kurudi nchini nilijiunga kwaya ya kanisani ile ya praise and worship.,nilifanya mageuzi makubwa ya kwaya,sehemu ya vinanda nilitoa nikarepkace na sauti ya saxophone,
Hizi saxophone ziko aina tatu Altor Tenor na Saprano..mimi hupendelea hizo mbili za mwanzo.nimesahau kuna bass pia
Sasa wakati wa nyimbo za kuabudu huwa nakipuliza kwa misifa na unavyojua makanisa ya kilokole asilimia kubwa huwa ni wakina mama,...kuna siku nilikipuliza nikakuta kanisa zima wanalia kwa hisia kama wamefiwa,kucheki jirani yangu kuna dada vinyweleo vimemsimama.
Ni vile sina pepo la uzinzi ningemaliza kondoo wa bwana
Sema bei yake imechangamka,hakipungui laki saba.
Mimi nilizaliwa nilikikuta nyumbani,kule upareni janisa la kKKT zamani hakuna ibada bila kwaya ya matarumbeta,nadhani wajerumani wamisionari ndio waasisi wa tarumbeta makanisani.
Kama mpenzi wako amenuna au umemkasirisha mpigie taratiibu lazima akusamehe.
Wanawake wanapenda sana wanaume wenye talent hasa ya muziki,ila katika wasanii wote wapiga saxophone wanavutia sana wanawake